Kwa Nini CCM imefika mwisho.
Haitavuka 2030.
Zama zimebadilika,wanawake wamejiunga kwa wingi katika harakati za kudai haki,kwa kupaza sauti zao.
Kwa miaka mingi, wanawake ndio walikua wanaiunga mkono CCM kwa wingi,lkn Sasa hivi hali imebadikika.
Ongezeko kubwa la Vijana waliotimiza umri wq kupiga kura.
Bahati mbaya Kwa CCM Hawa ndio wanaoichukia CCM na Hawa ndio kundi la wanaodai mambadiliko.
kimsingi hawana historia na hawavutiwi na CCM.
Hawa ndio wanaotaka mabadiliko kwa njia zozote zile.
Ukiwanyima haki zao kwa amani watazitafuta kwa nguvu.
Tumeona.
Nina uhakika Uchaguzi ujao utakuja wakati tuna katiba mpya na tume huru ya uchaguzi,vitu ambavyo ni kitanzi kwa CCM.
Hakuna njia na namna yoyote ambayo CCM wataweza kuvitumia kukikwepa kikombe hiki Cha kuruhusu katiba mpya na tume huru ya Uchaguzi.
Makosa haya ndio yanaenda kuikomesha CCM kua chama tawala.
Na ikitoka haitarudi Tena.
Mkuu Livan,
Lee Van free , kwanza nakuunga mkono kwenye hoja hii, maana hata mimi niliandika humu
https://www.jamiiforums.com/threads...ccm-wajinga-karibu-wote-watakuwa-wamemalizika.
Ila ili hili liwezekane kutokea, lazima kwanza haya mambo matatu yatokee
1. Tanzania tubadili katiba kutoka hii katiba ya chama kimoja ya CCM ya mwaka 1977 into katiba mpya ya vyama vingi.
2. CCM isibadilike kwenda na wakati, iendelee kubweteka ushindi wa kishindo wa mazoea unaotokana na mbeleko ya dola na kufanya mambo (kwa mujibu wa Nape)
3. Kuwepo kwa credible opposition to check out CCM.
Kwenye bandiko lile nilltoa
Angalizo: Nimesema ni mwanzo wa mwisho wa CCM, sijasema ni mwisho wa CCM!. Hivyo kipindi chote hiki kutoka sasa hadi hiyo 2030, CCM haitajikalia tuu hivi hivi tuu kusubiria kufa kibudu, CCM wakati wote itakuwa busy kutekeleza ilani yake ili muda wa uchaguzi ulifika, CCM iibuke na kusema tuliahidi, tumetekeleza, hivyo kuzidi kujiimarisha ili kuendelea kutawala milele!.
Wengi wa wajinga wajinga waliokuwa wanaichagua CCM kwa mazoea tuu, most of them will have been long gone! na masikini wa kutupwa wenye kuweza kuuza kura yao kwa T-shirt na kofia, na shibe ya siku moja, watakuwa wamepungua!, mimi mwenyewe will be at 60s!.
Hata hivyo sio wote wanaiochagua CCM ni wajinga wajinga, kuna wengine wenye akili zao timamu, wanaichagua CCM kwa sababu hakuna alternative, hatuna any serious, credible opposition to choose from, upinzani uliopo ni upinzani uchwala. Wapinzani hawana hoja, wanatumia hoja za nguvu, badala ya nguvu za hoja, wamekalia siasa za matukio!.
Wapinzani mtanisamehe kuwaita Upinzani Uchwala, kwa sababu huu ndio ukweli wenyewe!. CCM ilikwisha chokwa siku nyingi ila kukosekana kwa upinzani imara kumewakatisha tamaa waliowengi na kuamua kutokupiga kura, badala ya kupoteza muda!, kwa sababu haoni cha kuchagua!.
Upinzani uliopo ni upinzani wa kupinga kila kitu, kupayuka, kutukana na kuhamasisha chuki, na uvunjifu wa amani kwa kutumia hoja za nguvu, badala ya kutumia nguvu za hoja, Upinzani wa kweli ni upinzani wenye hoja mbadala. Upinzani huu tulionao, bado haujaonyesha ukomavu wa kutosha kuaminiwa na kukabidhiwa ikulu yetu, hivyo japo CCM ni Li Zimwi, hili ndilo zimwi Watanzania walijualo!.
Hivyo wale wote wenye hasira na CCM, nawashauri washushe pressure zao, kwa sasa kwa siasa za Tanzania, mpango mzima ni CCM, uchaguzi wa 2020, karibu majimbo yote yaliyokuwa yanashikiliwa na upinzani, yatarejeshwa CCM, na Tanzania kuwa nchi ya chama kimoja, kwa miaka 10, kuanzia 2020 hadi 2030.
Hiki ni kipindi cha upinzani kujijenga upya, kwa kuhakikisha, tunabadili sheria ya uchaguzi, kuutoa ujinga wa kudhaminiwa na vyama na kuruhusu wagombea binafsi, tunasawazisha uwanja wa mchezo wa siasa kwa kutengeneza a level playing field, ili kufanya uchaguzi katika ushindani sawia, na kuifanyia maboresho Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo japo ni Tume Huru ila sio Inclusive, hivyo Tume itafanywa more inclusve ili kuwapata viongozi wasio na vyama, na makamishna, wajumuishe wawakilishi wa vyama vikubwa angalau toka vyama vitatu vikuu. Na hapa sasa ndio tutaona kuibuka kwa upinzani wa kweli ambao utaanza tena 2030!.
Sasa kwa vile 2030 is just around the corner huku bado hatuna any credible opposition to check out CCM, hivyo kama Uchaguzi wa 2030 tutakuwa na katiba mpya, na Tume huru ya uchaguzi, mshindi wuchaguzi wa 2030 ,bado ni CCM!.
Tena mimi nimeshauri twende na huyu
Kwa Kauli Kama Hizi, Kiukweli Kabisa,Huyu Mtu, Atamsaidia sana Rais Samia,Taifa na Watanzania. Mnaonaje kama 2030 Twende Naye Kwa Utaratibu Ule Ule ?
P