CCM imemlipia faini ya Tsh. Milioni 30 mwanachama wake Dkt. Vincent Mashinji. Atoka gerezani

CCM imemlipia faini ya Tsh. Milioni 30 mwanachama wake Dkt. Vincent Mashinji. Atoka gerezani

Asante Mashinji, maana, kwa kurudi kwako CCM, hukumu imekuwa 'HAMBOHAMBO'!
👊 ✌️✌️✌️💥❣️
 
Kwa maelezo ya viongozi wa CHADEMA wamesema wanalipa faini ili wakitoka waanze mchakato wa rufaa. Tumeona pia CCM wamefanya hivyo kwa mwanachama wao mpya Dkt. Mashinji kwa kumlipia faini.

Je, viongozi wa CHADEMA wakikata rufaa, CCM watashangilia ushindi endapo Mahakama ya Juu ikitengua hukumu ya Mahakama ya Kisutu?

Naomba kuwasilisha.
 
Kwa maelezo ya viongozi wa CDM wamesema wanalipa faini ili wakitoka waanze mchakato wa rufaa tumeona pia CCM wamefanya hivyo kwa mwanachama wao mpya Dk mashinji kwa kumlipia faini na je viongozi wa CDM wakikata rufaa je na CCM watashangilia ushindi endapo mahakama ya juu ikitengua hukumu ya hakimu mkuu Simba.

Naomba kuwasilisha tujadili

Sent using Jamii Forums mobile app
Inafikirisha!
 
Chama kikongwe kama ninyi bado hamna watu wenye ujuzi wa kukisimamia na kuongoza chama chenu hadi leo kwa zaidi ya miaka 50 ni fedheha kubwa. Yaani mnashangilia kupata Mashinji kuja kuongoza chama chenu! Mnawalamba miguu watu waliowatukana na kuwakashifu ili waje wawaongoze.

Ni aibu kubwa hivi sasa kwa CCM nafasi zote nyeti kushikwa na waliokuwa wapinzani wenu kisiasa!

Shame on you! Wapinzani wenu mmewapa utendaji wa vijiji, udiwani, ubunge, ukuu wa wilaya, Uras, Ukuu wa mikoa, ukatibu Mkuu wa wizara zenu, uwaziri nk. Hivi wanachama wengi wa CCM ni vilaza kiasi hicho?

Halafu mnachekelea kama mazuzu!
 
Mtaji wa Mashinji wewe huujui.

Wanaoujua wametulia tuli.
 
Back
Top Bottom