CCM imemlipia faini ya Tsh. Milioni 30 mwanachama wake Dkt. Vincent Mashinji. Atoka gerezani

CCM imemlipia faini ya Tsh. Milioni 30 mwanachama wake Dkt. Vincent Mashinji. Atoka gerezani

Huko bado kiini macho, a.k.a utakatishaji unaendelea. Haiingii akilini wabunge wote haokukosa hizo fedha. Nyumbu wa Ufipa wanaendelea kutumika tu bila kujijua. Hata hivyo hiyo faini mabeberu watailipa. Hapa tunadanganywa tu kuwa wananchi wanachanga.
mabeberu mliowaandikia barua ya kuomba msamaha?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana Mkuu. Watz walishapewa jumla kuu ya Tshs Mln 350. Walichanga bila kumbagua mtu na hakuna Kiongozi yeyote wa Chadema aliyejitokeza kifanya marekebisho ya jumla kuu.

Tungemlipia kisha aje huko kwenu kuendelea kuunga juhudi. Lkn nakuhakikishia hakuna mtu aliyepatwa na aibu kama yule Muunga juhudi. Hivi unafahamu alichozungumza kule Segerea jana jioni?? Hata ww ungemhurumia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Alisemaje uyo snitch?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtazamo wako si wa wanaccm !
Wakukurupuka. Hivi huyu Mr Slow hajui kwamba mahakama hawapokei hela cash? Au nae ni kujaribu kuwadanganya Watanzania kwamba Ccm ina pendwa. Hivi ni mtu gani wa hali ya chini atakae mchangia Mashinji? Ni kitu gani amewafanyia Ccm hadi wana Ccm wawe na huruma kumtoa jela?

Kila kitu Ccm mnabaka hata visivyo bakwa. Kuanzia uchaguzi hata kutoa hela za chama kutudanganya ati ni wana Ccm wamechanga?

Ni nani asiye jua hata hii hukumu ina mkono wa Ccm? Ni nani asie jua kwamba hii kesi ni ya kubambikizwa? Ila Ccm kesheni mkiomba ili siku mbingu zitakapo funguliwa muone Watanzania wakisherehekea ushindi..

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtazamo wangu hizi drama za kuchangia pesa zinazofanywa na CCM na CHADEMA ni kitu ambacho hakipo sawa kimantik, kwani kama mahakama iliwakuta na makosa watuhumiwa na ikatoza faini ambayo ni kulipa ili ujutie kosa ulilofanya sasa hii ina maana gani kwa Taifa,. Ni kutuaminisha kuwa Mahakama kama muhimili pekee wa haki, inatoa hukumu batili ama inakuaje?, kiukweli mimi hainingii akilini ila ni mtazamo tu.
 
Hivi kweli chadema haina pesa mpaka watu wachangishwe? Hii ni dhurma nyingine wanachama na wapenzi wa chadema wanafanyiwa na watu wenye unafuu wa maisha.
tumeridhia kudhurumiwa na tumefanya kwa mahaba igizeni nyie CCM kuwafunga waliomba mangura sumu muone kama watachangiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM inaunda serikali,Serikali ikamshitaki Dr.Mashinji kwa kukiuka sheria za nchi,DPP akaendesha shauri usiku na Mchana,Mahakama ikamtia hatiani,CCM chini ya mwenyekiti ambaye ni Raisi inatoa fedha kumlipia faini Dr.Mashinji mvunja sharia.Aliyekabidhiwa sharia azilinde kama custodian akazivunja mwenyewe akajishitaki na kujilipia faini............Kiuongozi hii haikuwa sawa.Tafsiri ni kuwa Polisi,Mwanasheria Mkuu wa serikali,DPP,na serikali yote ilimwonea Mashinji na hivyo wameamua kukiri makosa kwa kumlipia faini.
 
hIII HUKUMU NA YA 6G
MKIENDELEZA UPUMBAVU WENU MNAOGA LE 8G
MWENDO WA 500M
MKIRUDI TUBAMALIZIA NA 750M
AMJATENGENEZA ZLE BARABARA ZA KIMARA NDANI NDANI NA BAKIZO TUKAREKEBISHA MASHIMO BJIA ZA SINZA HII NDIO KILICHOBAKIA
MWENDO WA GAWIO....
hapo umeshindwa kuficha ujinga wako kuandika tu haujui

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam kimemlipia faini ya Shilingi Milioni 30 mwanachama mpya wa chama hicho Vincent Mashinji aliyekutwa na hatia kwenye makosa kadhaa kwenye Hukumu iliyotolewa jana ya kesi iliyokuwa ikimkabili pamoja na viongozi wa Chadema akiwemo Freeman Mbowe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam.

Akizungumzia hatua hiyo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Humphrey Polepole, amesema kiasi hicho cha fedha kimechangwa na wanachama wa chama hicho ili kumtoa kada huyo aliyelala gereza la Segerea baada ya zoezi la kulipa adhabu hiyo jana kushindikana kwasababu ya muda.

View attachment 1384052
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akionesha risiti ya malipo leo Jumatano Machi 11, 2020 alipofika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kulipa faini ya milioni 30 ya mwanachama wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji.

UPDATE: Dkt. Mashinji atoka gerezani baada ya kulipa faini ya Tsh. Milioni 30

View attachment 1384213

Dkt. Mashinji akiwa ndani ya gari baada ya kutoka gerezani

Akizungumza baada ya kutoka jela, Dk Mashinji amesema, “ sikutegemea wana CCM watanilipia faini, sikutegemea wangelifanya jambo hili kwa uzito kama huu maana hadi jana familia yangu ilikuwa inaendelea kutafuta fedha ili kunitoa.”

“Ila leo wana CCM Mkoa wa Dar es Salaam wamejiunga kwa pamoja na kunilipia faini, nashukuru nipo chama dume kwa ajili ya kutoa mchango wangu kwa Taifa.”
Wana CCM walijiunga lini? Au wanechota hazina pesa ya tra?
 
Pole sana Mkuu. Watz walishapewa jumla kuu ya Tshs Mln 350. Walichanga bila kumbagua mtu na hakuna Kiongozi yeyote wa Chadema aliyejitokeza kifanya marekebisho ya jumla kuu.

Tungemlipia kisha aje huko kwenu kuendelea kuunga juhudi. Lkn nakuhakikishia hakuna mtu aliyepatwa na aibu kama yule Muunga juhudi. Hivi unafahamu alichozungumza kule Segerea jana jioni?? Hata ww ungemhurumia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Alizungumza nini huyo huko segerea mkuu hebu tufahamishe wengine tupo maporini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam kimemlipia faini ya Shilingi Milioni 30 mwanachama mpya wa chama hicho Vincent Mashinji aliyekutwa na hatia kwenye makosa kadhaa kwenye Hukumu iliyotolewa jana ya kesi iliyokuwa ikimkabili pamoja na viongozi wa Chadema akiwemo Freeman Mbowe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam.

Akizungumzia hatua hiyo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Humphrey Polepole, amesema kiasi hicho cha fedha kimechangwa na wanachama wa chama hicho ili kumtoa kada huyo aliyelala gereza la Segerea baada ya zoezi la kulipa adhabu hiyo jana kushindikana kwasababu ya muda.

View attachment 1384052
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akionesha risiti ya malipo leo Jumatano Machi 11, 2020 alipofika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kulipa faini ya milioni 30 ya mwanachama wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji.

UPDATE: Dkt. Mashinji atoka gerezani baada ya kulipa faini ya Tsh. Milioni 30

View attachment 1384213

Dkt. Mashinji akiwa ndani ya gari baada ya kutoka gerezani

Akizungumza baada ya kutoka jela, Dk Mashinji amesema, “ sikutegemea wana CCM watanilipia faini, sikutegemea wangelifanya jambo hili kwa uzito kama huu maana hadi jana familia yangu ilikuwa inaendelea kutafuta fedha ili kunitoa.”

“Ila leo wana CCM Mkoa wa Dar es Salaam wamejiunga kwa pamoja na kunilipia faini, nashukuru nipo chama dume kwa ajili ya kutoa mchango wangu kwa Taifa.”
Sasa hapo ndipo utajua CCM kweli vichwa vimejaa utupu. Watu hawa ndio walishinikiza watuhumiwa washitakiwe na wakawa wanashangilia na kusema hawa ni waharifu. Mpaka leo bado wanasema hawa ni waarifu. Lakini bado hapo hapo wanakenua maneno wakisema tumemtoa huyu (si mharifu tena) na bado wanasema Mbowe na wenzake ni waarifu wanaombewa wafungwe. Kama si ujinga tuite ni kitu gani. Hawa hawa watakwambia ni watu wamekwenda shule. Mimi nadhani ukiwa CCM wankuondoa ubongo unabakiza fuvu tupu
 
Back
Top Bottom