CCM imemlipia faini ya Tsh. Milioni 30 mwanachama wake Dkt. Vincent Mashinji. Atoka gerezani

CCM imemlipia faini ya Tsh. Milioni 30 mwanachama wake Dkt. Vincent Mashinji. Atoka gerezani

Screenshot_20200311-151905.png
 
Attachments

  • Screenshot_20200311-151857.png
    Screenshot_20200311-151857.png
    141.3 KB · Views: 1
Kwasababu hiyo hela itakayolipwa kutokana na adhabu walopewa wahusika ni ya serikaki hivo kunauwezakano hiyo hela kwaajili ya kumlipia Mashinji haijalipwa na hizo karatasi za kutuonesha kuwa wamelipia inawezakuwa wame zi counterfeit ili iinekane nao wamelipa wakati yawezekana hakuna hata sent ilokuwa deposited to account.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam kimemlipia faini ya Shilingi Milioni 30 mwanachama mpya wa chama hicho Vincent Mashinji aliyekutwa na hatia kwenye makosa kadhaa kwenye Hukumu iliyotolewa jana ya kesi iliyokuwa ikimkabili pamoja na viongozi wa Chadema akiwemo Freeman Mbowe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam.

Akizungumzia hatua hiyo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Humphrey Polepole, amesema kiasi hicho cha fedha kimechangwa na wanachama wa chama hicho ili kumtoa kada huyo aliyelala gereza la Segerea baada ya zoezi la kulipa adhabu hiyo jana kushindikana kwasababu ya muda.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akionesha risiti ya malipo leo Jumatano Machi 11, 2020 alipofika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kulipa faini ya milioni 30 ya mwanachama wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji.
Ulifeli hesabu. 350,000,000/= - 30,000,000/=????
 
Nigrastratatract,

Kwa chama tawala kupelekeshwa na Chama kikuu cha upinzani kiasi cha kufanya ushabiki na ushamba mwingine usio na heshima ya chama chenyewe ni jambo la kuogopesha sana.

Yaani Mashinji ana thamani kubwa kuliko wanachama mamilioni wa CCM wanaohangaika na madeni na wengine wako gerezani kwa kukosa laki moja tu? Halafu wanaona wame score point....!!!

Kweli CCM kimeshikwa na wa kuja wasioelewa heshima iliyopo katika ya chama tawala na vyama shindani. Yaani wanashushwa chini kwenye vitukio vya kipuuzi puuzi tu utadhani hawana serikali ikulu?

Too bad for the fate of our nation.
 
Sasa kimada chako ukitoe Bukoba_Dar afu kimekumbwa na dholuba Fulani lazima ukisaidie kuonesha uanaume wako😂. Mashinji jiandae kulipa hizi pesa either ulale kwa waganga au ujitoe kuwa chizii kuropoka.
 
mzee pole2 kiasikinachochangwa na uma ni sh.350,000.000/=ambazo ni faini ya viongozi wote waliotiwa hatiani pamoja na huyo wako yuko kwenye hesabu sasa hizo zimechangwa kupitia a/c ipi ili na wengine wachangie ????
 
kiasi hicho kiko atakatwa kwenye hesabu za usajili hongera zake
 
Tulitarajia hili tangu jana
Hawana jipya,walitaka apige magoti vizuri zaidi na ahitimu kuwa full puppet wao.Walishajiandaa mapema hats kabla ya hukumu yenyewe,walikuwa wanzugatu.

Hii ni kampeni live, ili wapinzani wenye mashauri waunge mkono juhudi yaishe mifano ipo.
 
Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam kimemlipia faini ya Shilingi Milioni 30 mwanachama mpya wa chama hicho Vincent Mashinji aliyekutwa na hatia kwenye makosa kadhaa kwenye Hukumu iliyotolewa jana ya kesi iliyokuwa ikimkabili pamoja na viongozi wa Chadema akiwemo Freeman Mbowe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam.

Akizungumzia hatua hiyo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Humphrey Polepole, amesema kiasi hicho cha fedha kimechangwa na wanachama wa chama hicho ili kumtoa kada huyo aliyelala gereza la Segerea baada ya zoezi la kulipa adhabu hiyo jana kushindikana kwasababu ya muda.

View attachment 1384052
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akionesha risiti ya malipo leo Jumatano Machi 11, 2020 alipofika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kulipa faini ya milioni 30 ya mwanachama wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji.

UPDATE: Dkt. Mashinji atoka gerezani baada ya kulipa faini ya Tsh. Milioni 30

View attachment 1384213

Dkt. Mashinji akiwa ndani ya gari baada ya kutoka gerezani

Akizungumza baada ya kutoka jela, Dk Mashinji amesema, “ sikutegemea wana CCM watanilipia faini, sikutegemea wangelifanya jambo hili kwa uzito kama huu maana hadi jana familia yangu ilikuwa inaendelea kutafuta fedha ili kunitoa.”

“Ila leo wana CCM Mkoa wa Dar es Salaam wamejiunga kwa pamoja na kunilipia faini, nashukuru nipo chama dume kwa ajili ya kutoa mchango wangu kwa Taifa.”
Polepole anafanya maigizo makubwa mno wanacheka yaani wanaona aibu kwa maigizo ya kitoto wanayoyafanya bila aibu najua kabisa wakienda nyuma ya Camera wanacheka kwa ujinga walioufanya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom