CCM imemlipia faini ya Tsh. Milioni 30 mwanachama wake Dkt. Vincent Mashinji. Atoka gerezani

CCM imemlipia faini ya Tsh. Milioni 30 mwanachama wake Dkt. Vincent Mashinji. Atoka gerezani

Mkuu anayewateuwa hawaangalii kwa jicho hilo unaloangalia wewe, yamkini hana Imani na wale wenye chama kwa hiyo akianza na safu hii mpya kutoka upande wa pili itamsaidia sana kumvusha anapopataka yeye maana unaponunua sehemu lazima unanunua na siri za mpinzani wako.

Na pia ni rahisi kupanga safu ya ushambuliaji ukiwa na wachezaji wageni pia unachanganya na wakongwe ni rahis sana kuwatawala wote kwa wakati mmoja, kwanza umewagawa (hawawezi kunena mamoja) pili wanachukiana wao kwa wao kitu ambacho kinafanya kazi kuwa rahisi sana kwa bw mkubwa kuwatawala wote kwa wakati mmoja[emoji4]

it’s a technical skills brother
 
Ccm imepoteza dira, imelewa madaraka...Haisimamii tena misingi ya taifa letu kupata uhuru.Uhuru Wa watu imetia kapuni
 
CCM wanategemeaga tamboo za Yohana tu, Yohana naeee anategrmeaga mkwala tu rakini hana kitu

Don't make a promise you can't fulfill...
 
Chama kikongwe kama ninyi bado hamna watu wenye ujuzi wa kukisimamia na kuongoza chama chenu hadi leo kwa zaidi ya miaka 50 ni fedheha kubwa. Yaani mnashangilia kupata Mashinji kuja kuongoza chama chenu! Mnawalamba miguu watu waliowatukana na kuwakashifu ili waje wawaongoze.

Ni aibu kubwa hivi sasa kwa CCM nafasi zote nyeti kushikwa na waliokuwa wapinzani wenu kisiasa!

Shame on you! Wapinzani wenu mmewapa utendaji wa vijiji, udiwani, ubunge, ukuu wa wilaya, Uras, Ukuu wa mikoa, ukatibu Mkuu wa wizara zenu, uwaziri nk. Hivi wanachama wengi wa CCM ni vilaza kiasi hicho?

Halafu mnachekelea kama mazuzu!
Yah naona umewapa kijembe Cha kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom