LGE2024 CCM Imeshinda kihalali na kuvuna kile ilichopanda, CHADEMA haikujipanga

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kubalini ukweli kuwa hamkujipanga katika uchaguzi huu na kwamba mnapaswa kujipanga upya hapo mwakani.
 
Kubalini ukweli kuwa hamkujipanga katika uchaguzi huu na kwamba mnapaswa kujipanga upya hapo mwakani.
Wewe chawa usidhani kila anayekosoa upuuzi wa ccm ni chadema. Unapumbaza ufahamu wako wa kutofautisha jema na baya kwa sababu ya njaa zako tu. Wizi wa kura ccm ni wa muda mrefu ila umezidishwa na sababu ni wananchi wengi kuikataa ccm. Kama hujui hilo pole sana.
 
CCM tunapita kihalali na kwa haki.ndio maana unaona wananchi wakishangilia ushindi mitaani kote.
 
Tufute upinzani. Wa nini na chama tawala ndo pekee kinachohitajika?
Kama mnataka kufuta upinzani futeni maana hauna chochote çha maana. ufuteni tuu kàma chama tawala ndo pekee kinachohitajika.
 
Mimi sitokuja kupiga kura mpaka tupate chama cha upinzani chenye nia ya dhati ya kuwapambania watanzania.

Sio awa wa sasa hoja zao ni kuzusha taarifa mjini tweeter.
Watanzania wapi hawa au wengine? Kama mnategemea vyama vya upinzani ndio viwaletee mabadiliko basi mko nyuma sana na mtakuwa dissapointed, wananchi pambaneni wenyewe
 
Ukiona chama kinakaa madarakani kwa chaguzin za kihayawani, ujue chama hicho kiko nje ya wakati.
 
Binafsi huwa nawashangaa upinzani hii nchi na Imani yao ya kutoboa.
Serikali iliyopo madarakani ndio mzimamizi wa mchakato mzima wa uchaguzi Sasa inawezekanaje ikajipiga mama kupitia mchakato huo?
 
CCM tunapita kihalali na kwa haki.ndio maana unaona wananchi wakishangilia ushindi mitaani kote.
Ipi mantiki yako? Cdm na ccm ni watu na wote ni wananchi au ni uongo? Ccm wakishangilia ni wananchi pia na Cdm walioyakataa matokeo ni wananchi pia na hiyo ndio mantiki. Hakuna kitu kinachoitwa wananchi katika ujumla wao wakiwa na mitazamo inayofanana. Kinachopingwa ni dhuluma ya wazi kabisa ambayo kila mfuatiliaji wa siasa ameona kupitia video mbalimbali mitandaoni.

Mambo kama hayo ndio unachangia umaskini wako na kizazi chako lakini kwa kuwa huna vision huwezi kuyaona hayo. Ccm ni wezi wa kura kama unakataa na huku nafsi yako ikiujua ukweli basi wewe ni mfuasi wa ibilisi. Kwenye mambo ya haki za watu hupaswi kuwa mpumbavu.
 
Mr Lucas Mimi nipo neutral sio CCM wala sio mpinzani.
Kwa Hali niliyoiona hamna chochote Cha kujivunia maana mlicheza faulo tangu wakati wa kupitisha majina kwa kuwakata isivyo halali wapinzani wenu karibu nchi nzima so ushindani haukuwepo kwavile mlikuwa mkiogopa kushindwa iwapo haki ingefanyika mngeanguka vibaya sana au ingekuwa 50/50.
Mathalani Hapa mtaani kwetu vituo vilikuwa vyeupee watu wengi hawakupiga kura sababu waliowataka sio waliopitishwa kugombea
 
Hivi unafahamu ya kuwa maeneo mengi sana CHADEMA ilikuwa haina wagombea baada ya kukosa wagombea? Unajua ilifika wakati ikawa inawaomba watu wagombea ambao ukiwaangalia walikuwa hawakubaliki kabisa.dosari huwa zinakuwepo na ni kawaida katika uchaguzi.lakini ukweli ni kuwa upinzani haukujipanga na umepoteza kabisa ushawishi.embu niambie Mbowe alianza lini kupiga kampeni za uchaguzi huu?
 
Fact
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…