Songambele
JF-Expert Member
- Nov 20, 2007
- 4,710
- 2,587
Mwaka wa uchaguzi mdogo hata magroup ya whatzapp yameshaanza kuundwa huku mitaani kuhakikisha wembe ni ule ule. Ujumbe huu ndio wa kumpa Zitto and etal mnapokuwa mnasubiria tarehe ya tume wenzenu wanakuwa washatoka kambani.Hapa Iringa kuna harakati zinaendeshwa na kundi la baadhi ya wana CCM kuwashawishi waalimu kujiorodhesha na kuingizwa kwenye Kanzi Data (Data Base) ya chama hicho kwa ahadi kwamba kipekee maslahi yao yatashughulikiwa.
Waalimu wanaoingizwa kwenye kanzi data hiyo inasemwa kwamba watakuwa wanaitwa "waalimu Wazalendo" na lengo ni kupanga uungwaji mkono toka kada hiyo ya waajiriwa wa serikali.
Inawezekana mifumo ya kupandisha madaraja na mishahara kwa waalimu iko hivi ilivyo sasa lengo likiwa ni atakayekuwa upande wa CCM atafaidika na atakayekuwa kinyume na CCM atakwamishwa.
Sent using Jamii Forums mobile app