Tetesi: CCM inaorodhesha walimu wazalendo

Ukweli ni kwamba adui namba moja wa maendeleo Tanzania ni CCM
 
Hapa Iringa kuna harakati zinaendeshwa na kundi la baadhi ya wana CCM kuwashawishi waalimu kujiorodhesha na kuingizwa kwenye Kanzi Data (Data Base) ya chama hicho kwa ahadi kwamba kipekee maslahi yao yatashughulikiwa.

Waalimu wanaoingizwa kwenye kanzi data hiyo inasemwa kwamba watakuwa wanaitwa "waalimu Wazalendo" na lengo ni kupanga uungwaji mkono toka kada hiyo ya waajiriwa wa serikali.

Inawezekana mifumo ya kupandisha madaraja na mishahara kwa waalimu iko hivi ilivyo sasa lengo likiwa ni atakayekuwa upande wa CCM atafaidika na atakayekuwa kinyume na CCM atakwamishwa.
 
Attachments

  • 1546611866347.png
    1546611866347.png
    71.8 KB · Views: 18
Kama Wewe Ni Mwalimu Mzalendo jiunge Kwenye hiyo data base Tatizo liko wapi?
Timieni akili kufikiri, viungo vingine vina kazi zake… Kuna tofauti kati ya uzalendo na uanachama wa CCM...

Hivi mnadhani nje ya CCM hakuna wazalendo?
 
'Rais anaweza kutoka Chama chote lakin Rais Bora lazima atoke ccm'-Mwl Nyerere

Hayo sio Maneno ya Pohamba ya Baba Na Muasisi wa Taifa hili kishakwambia hivyo Mie Nani niongeze walau nukta
 
Soon Serikali/ccm inaorodhesha Wafanyakazi wote Serikalini ambao ni Wanachama wa chama hicho kisha watafuatiwa na Wakulima, Wafanyabiashara, Wavuvi na Wanafunzi wote wa elimu ya juu.

Hapa Iringa kuna harakati zinaendeshwa na kundi la baadhi ya wana CCM kuwashawishi waalimu kujiorodhesha na kuingizwa kwenye Kanzi Data (Data Base) ya chama hicho kwa ahadi kwamba kipekee maslahi yao yatashughulikiwa.

Waalimu wanaoingizwa kwenye kanzi data hiyo inasemwa kwamba watakuwa wanaitwa "waalimu Wazalendo" na lengo ni kupanga uungwaji mkono toka kada hiyo ya waajiriwa wa serikali.

Inawezekana mifumo ya kupandisha madaraja na mishahara kwa waalimu iko hivi ilivyo sasa lengo likiwa ni atakayekuwa upande wa CCM atafaidika na atakayekuwa kinyume na CCM atakwamishwa.
 
'Rais anaweza kutoka Chama chote lakin Rais Bora lazima atoke ccm'-Mwl Nyerere

Hayo sio Maneno ya Pohamba ya Baba Na Muasisi wa Taifa hili kishakwambia hivyo Mie Nani niongeze walau nukta

Hizo ni fkra zako za kipopoma.
 
'Rais anaweza kutoka Chama chote lakin Rais Bora lazima atoke ccm'-Mwl Nyerere

Hayo sio Maneno ya Pohamba ya Baba Na Muasisi wa Taifa hili kishakwambia hivyo Mie Nani niongeze walau nukta
Inahusiana nini na nilichokiandika?
 
Hapa Iringa kuna harakati zinaendeshwa na kundi la baadhi ya wana CCM kuwashawishi waalimu kujiorodhesha na kuingizwa kwenye Kanzi Data (Data Base) ya chama hicho kwa ahadi kwamba kipekee maslahi yao yatashughulikiwa.

Waalimu wanaoingizwa kwenye kanzi data hiyo inasemwa kwamba watakuwa wanaitwa "waalimu Wazalendo" na lengo ni kupanga uungwaji mkono toka kada hiyo ya waajiriwa wa serikali.

Inawezekana mifumo ya kupandisha madaraja na mishahara kwa waalimu iko hivi ilivyo sasa lengo likiwa ni atakayekuwa upande wa CCM atafaidika na atakayekuwa kinyume na CCM atakwamishwa.
Hapo unajiunga tu. Moyo wako ndiyo utakuwa unajua upo wapi,kwenye kura unapiga upinzani,ukiwa pembeni kampeni kwa wapinzani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
'Rais anaweza kutoka Chama chote lakin Rais Bora lazima atoke ccm'-Mwl Nyerere
CCM imekuwa kama Kokoro, inabeba kila uchafu. Haya pia ni maneno ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
 
Back
Top Bottom