CCM inazidi kupoteza Fursa ya Kujijenga Upya Kupitia Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi

andazi

Member
Joined
Jun 7, 2025
Posts
63
Reaction score
269
CCM wanaendelea kufanya makosa makubwa sana kisiasa. Huu ulikuwa muda wao sahihi kabisa wa kutengeneza katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Kama wangefanya hivyo, wangejihakikishia nafasi ya kubaki kama chama kikuu nchini hata kama wangeondoka madarakani leo.

Kwa mfano, kule Marekani, vyama kama Republican na Democrat vinaendelea kushindana lakini vyote vina heshima na nguvu kwa sababu mfumo wa kidemokrasia ni huru na wa haki. Vivyo hivyo, CCM wangejenga heshima ya kudumu kama chama kinachoamini katika demokrasia, na hata kama wananchi wangeamua kuwatoa madarakani, tume huru hiyo hiyo ingewarudisha kwa kura za wananchi si kwa nguvu ya dola.

Lakini wanavyoendelea kupambana kubaki madarakani kwa njia zisizo za kidemokrasia, wanajiharibia wenyewe. Iwapo wananchi watafanikiwa kuwaondoa madarakani, basi kwenye asilimia 100% za kupotea kisiasa, CCM watakuwa na angalau 99.5% za kupotea kabisa kama ilivyotokea kwa vyama vingine vilivyong’ang’ania madaraka – mfano PPRD nchini DRC, Colorado na vingine vingi barani Afrika.

Kwa kifupi, hii ilikuwa nafasi ya CCM kujijenga kama taasisi ya taifa, lakini sasa wanaelekea kupoteza hadhi hiyo kwa kukosa kuona
 
..Mama angesikiliza ushauri wa Tundu Lissu na Chadema kwamba uchaguzi uahirishwe ili kutoa nafasi ya mabadiliko.
 
wakifikiria Mali walizo iba wachoka kabisa
 
Tupo pazuri wazee ,tumkaze tu buti ,hatuko mbali na ushindi
 
..Mama angesikiliza ushauri wa Tundu Lissu na Chadema kwamba uchaguzi uahirishwe ili kutoa nafasi ya mabadiliko.
Hivi rais wa nchi kama unafanya watu wako wa karibu, unaosikiliza ushauri kutoka kwao, ni watu kama Angela Kiziga, Steve Nyerere, Makonda, Salim mapete.... na mtoto wako Abdul, unaweza kufanya maamuzi ya busara? Ikulu imeingiliwa!
 
..Mama Abduli anaweza kurudi akawa katili pasikalike humu ndani.

..tujikumbushe kilichotokea Kenya chini ya Moi baada ya mapinduzi ya 1982 kufeli.

MK254

Itoshe kusema nimebaki kushangaa, sikudhani Watanzania wana huu ubavu, niliwaona waoga waoga na hii itakua imeshtua hata viongozi wa dola wote hadi hata mama mwenyewe, mama Samia alikosea kwenye hili kuachia Watanzania mpaka wafike hapa, maana tayari wameonja asali ya fujo na kuja kubadilika haitakua rahisi tena, hata haya yakija kuisha, hawatakua aina ya Watanzania mliowazoea tena.

Akubali kukaa na viongozi wa upinzani wabuni jopo la maridhiano, ibuniwe serikali ya mseto ya muda mfupi itakayowezesha katiba kutengenezwa upya kisha baada ya hapo ufanywe uchaguzi chini ya katiba mpya, ndicho tulichokifanya hapa kwetu Kenya mnamo mwaka wa 2008.

Japo naona kasoro moja mnafanya, ambayo pia sisi Wakenya tulifanya, hasira zenu elekezeni kwa serikali sio kwa watu wanaounga mikono CCM, hiyo ilikua haki yao kikatiba haikua makosa hapo. Sisi tulicharangana mapanga kisa misimamo ya kisiasa na ilikua kosa sana. Acheni kuchoma biashara za watu kisa walitenda walichoruhusiwa kikatiba.
 
Back
Top Bottom