CCM ISIISHI KWA KUKARIRI. MABADILIKO NI LAZIMA.

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Kuna hoja za msingi zilizoibuliwa na taasisi na watu mbalimbali kwa nyakati mbalimbali kuhusiana na shetia mbaya za uchaguzi na Tume isiyo huru ya uchaguzi.

Tume ya jaji Nyalali mwaka 1991, ilitamka kuwa Tume ya uchaguzi siyo huru, sheria na kanuni za uchaguzi hazilindi uchaguzi kuwa huru na wa haki.

Mwaka 1995, report ya watazamaji wote wa kimataifa ilisema Tanzania ifanye mabadiliko haraka ya sheria ya uchaguzi kuwezesha uchaguzi kuwa huru, wa wazi na wa haki.

Tume ya Jaji Kisanga ilisema kuwa kunahitajika kufanya mabadiliko ya katiba ili kuwezesha kupatikana Tume huru ya Uchaguzi.

Tume ya Jaji Mark Bomani, ilielekeza kuwa ili nchi yetu kuwa na Uchaguzi ulio huru na wa haki, ni lazima kuundwe Tume huru ya Uchaguzi ambayo haitakuwa chini ya Rais.

Time ya Jaji Warioba, pamoja na mambo mengine, ilieleza kuwa wananchi wanahitaji katiba mpya, na kwenye katiba hiyo mpya, ilipendekezwa tuwe na Tume huru ya uchaguzi isiyo chini ya Rais.

Hayati Mkapa, naye alisisitiza kwenye kitabu chake, kuwa Tanzania iwe na Tume huru ya uchaguzi.

Kwenye mabadiliko ya sheria ya uchaguzi ya na muundo wa Tume ya Uchaguzi ua mwaka 2023, Chama cha wanasheria, Baraza la Maaskofu Katoliki, Shura ya Maimamu, vyama vya siasa (isipokuwa CCM), na taasisi mbalimbali, wote walipendekeza kuwa kuwepo na Tume huru ya Uchaguzi isiyoteuliwa na Rais directly au indirectly, wote walipendekeza jeshi la polisi lisihusike kwa namna yoyote ile kwenye shughuli za uchaguzi, watendaji wa tume ya uchaguzi, wasiwe watumishi wa Serikali.

Hayo maoni na mapendekezo yote ya wakati wote, CCM imeyatupilia mbali, na kuamua kuendelea kutumia Tume ya Rais kusimamia uchaguzi, kuwatumia polisi kama nyenzo muhimu ya kulazimisha ushindi wa CCM, na kuwatumia watumishi wa Serikali kwenye chaguzi ili waendelee kuelekezwa namna ya CCM kuweza kupora ushindi kwenye chaguzi.

Mtu mwenye akili timamu, unajiuliza, kiburi hiki cha CCM, kukatalia maamuzi ya wananchi, Taasisi za kimataifa, Taasisi za dini, Taasisi za wataalam mbalimbali; inapata wapi?

CCM inapoyakataa maoni na matakwa ya Watanzania, ina maana hiki chama kipo kwaajili ya watu gani?

Kwa vyovyote vile, CCM hii, inamaanisha, haipo kwaajili ya maslahi ya Watanzania walio wengi, ipo kwaajili ya maslahi ya kikundi fulani ambacho kinawaona watanzania wote ni wajinga na hawana uwezo wa kufanya chochote hata wakipuuzwa.

Kwa vile CCM imewapuuza Watanzania kwa miaka mingi, sasa imekomaa na kufuzu katika kuwadharau wananchi.

CCM isichofahamu ni kuwa ujinga huwa una mwisho. CCM itashangazwa na maamuzi ya wananchi wenye uelewa, wakati yenyewe siku zote imeamini kuwa Watanzania wana nadhiri ya milele na ujinga, woga na unyonge.

NO REFORM NO ELECTION ndiyo fimbo ya kugomea dharau ya CCM dhidi ya wananchi.

WITO
Kama huko CCM, kuna japo wachache wenye hekima, ambao akili zao hazijazikwa kwenye uovu wa kuwadharau Watanzania, wafante hima, kukutana wadau wote wa uchaguzi ili kufanyike minimum necessary reforms za kuwezesha uchaguzi huru na wa haki.

Baada ya uchaguzi, katiba ifumuliwe ili kupata katiba bora kwa Taifa letu.
 
Walizoea wapinzani wa Siasa za Ongeza Dau
 
Hakika wasipoondoka kwenye usingizi wa siasa za uovu, CCM itakuja kuondoka kwa aibu kubwa. Na ikiondoka kwa namna hiyo, itakufa na kupotea, kwa maana hata mtu kujulikana tu kuwa wewe ni mwanachama wa CCM, chama kitakachoonekana ni laana kwa nchi, itakuwa ni aibu kubwa ambayo hakuna atakayetaka kushikanishwa nayo.
 
Walizoea wapinzani wa Siasa za Ongeza Dau
Hizi Siasa za Lissu ndizo Watanzania walikuwa wakizisubiri kwa hamu kubwa NO REFORMS NO ELECTION NO UCHAFUZI YES UCHAGUZI HURU NA WA HAKI.
 
Back
Top Bottom