Mkuu Paskal huwa naheshimu sana michango yako hapa JF na nje ya JF, lakini kwa hili unalosema kwa uhakika namna hii sina budi kukupinga. Mambo sio rahisi kiasi hicho. Utakuwa uchaguzi mgumu sana kwa mara ya kwanza kwa kiongozi aliyeko madarakani.
Sababu kuu ni kama mbili tatu hivi. Kwanza upinzani mkubwa wa chini kwa chini ulioko ndani ya chama chake. Kwa mara ya kwanza tunaona mwenyekiti wa chama anayepingwa na vigogo wa ndani ya chama kwa uwazi na kwa siri pia.
Sababu nyingine ni hali ya maisha na mateso wapatayo wananchi, na kama hali hii itaendelea hivi hakika labda atumie jeshi kujibakisha madarakani. Lakini lakujiuliza ni jee ushawishi huo ndani ya vyombo hivyo anao?
Tuachie hapo tusije pimwa mkojo bure, tukakutwa na UTI
Mkuu kwanza asante kwa kuheshimu michango yangu ndani ya jf na nje ya jf, pili kutofautiana kwa hoja ni kitu very heathy kwenye mjadala, na hapa umeweka hoja za msingi kabisa kuhusu 2020 ndani ya CCM.
Kitu cha kwanza ambacho tukubaliane ni kuwa japo haikuandikwa popote, lakini kwa 2020, Magufuli hana mpinzani ndani ya CCM, ndiye mgombea wa CCM uchaguzi wa 2020 kwa sababu hakuna mwana CCM yoyote anaruhusiwa kuchukua fomu kumpinga!, huu ndio utaratibu wao wa CCM.
Kama by now CCM tayari inayo mgombea wa 2020 ambaye ni seating president, ataingia kwenye uchaguzi akiwa na presidential status, rights na all the presidential privileges, ikiwemo press, ving'ora, wasaidizi, msafara, magari ya umma ambayo yatabadili namba kuwekwa private number plates ili ku hoodwink wafadhili, then mtu huyu aje ashindane na mgombea yoyote, kutakuwa na ushindani kweli au igizo za ushindani?!.
Nchi za Scandinavia, incumbent akigombea, wanam scarp all his privileges, isipokuwa ulinzi, hivyo wagombea wote wanaingia kwenye uchaguzi wakiwa wanalingana, the playing field is level, watu wanashindana katika ushindani sawia, hivyo msindi anapatikana kwa haki. Uchaguzi wetu, mgombea mmoja anakuja na kingora akisindikizwa na dola kwa gharama za serikali, anashindana na mgombea with nothing, huu ni ushindani usio sawia, the playing ground is not level, unategemea nini?. Nasisitiza 2020 hakuna uchaguzi wa rais, tuna igizo la uchaguzi wa rais!.
Tukija kwenye wapiga kura, hivi unajua wapigakura wa Tanzani huwa wanachagua nini?. Mfikirie Magufuli wa 2020 anayeingia kugombea huku nyuma akiwa na track record yake ya
- Tanzania ya viwanda
- Barabara za juu kwa juu
- Treni ya umeme ya SGR
- Miondombinu ya mabarabara
- Miondombinu ya majengo
- Serikali ikiwa Dodoma
- Bomba la mafuta
- Uchumi wa gesi
- Nchi ya uchumi wa kati
- Ushindi wa vita vya rushwa-Tanzania bila rushwa
- Ushindi wa vita vya ufisadi-Tanzania bila ufisadi
- Elimu bure
- Tasaf itaongezewa uwezo kugawa zile njuluku double
- etc, etc,kuna mtu wa kushindana naye?.
Soma bandiko hili kwa makini, halafu lifikirie kwa real life scenario ya 2020
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020 ...
Paskali