Tetesi: CCM kaeni Chonjo, mwanaume anakuja. Msikimbie chama chetu!

Watanzania wana nidhamu ya woga, anaweza kushinda kwa Kishindo. Na tusipokuwa makini uchaguzi kweli usifanyike.

Naona hata akina Mbowe wameonesha dalili za kuufyata; wamemwachia TL pekee apambane...

Ni lazima tuanze kuidai katiba mpya na Utawala wa sheria siyo haya maamuzi yanayofanywa Kimungu Mtu.. Otherwise tumtegemee DAB kama next Presdent after Padlocks...
 
Waswahili walisema kutesa kwa zamu hivyo ni zamu yake na amepata kibali machoni pa Mfalume hivyo nikupoteza muda kujaribu kumzuia maana kama mfalume aishivyo ndivyo naye ataishi.
Yusuph akiwa mtumwa na mgeni ktk nchi ya Misri hata shule hakuna rekodi hivyo sidhani hata alijua kusoma na kuandika jina lake achilia mbali barua ya kiofisi lakini alipopata kibali machoni pa Mfalume wa Misri(Farao) hakuna aliyemzuia kuwa Waziri ktk Taifa lililokuwa na wasomi na kustarabika ktk karne hizo.
Hivyo mtu akipata kibali machoni pa Mfalume siyo rahisi kuzuia hatima yake AS LONG AS THE KING IS IN POWER lolote linawezekana.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heri ahamie huko kwani wananchi sio wa Dar tu bali TZ nzima tumechoka kusikia matusi, dharau au kiburi.
 
Chama kitakuwa vipande na itaniuma sana
 
Mkuu kwanza asante kwa kuheshimu michango yangu ndani ya jf na nje ya jf, pili kutofautiana kwa hoja ni kitu very heathy kwenye mjadala, na hapa umeweka hoja za msingi kabisa kuhusu 2020 ndani ya CCM.

Kitu cha kwanza ambacho tukubaliane ni kuwa japo haikuandikwa popote, lakini kwa 2020, Magufuli hana mpinzani ndani ya CCM, ndiye mgombea wa CCM uchaguzi wa 2020 kwa sababu hakuna mwana CCM yoyote anaruhusiwa kuchukua fomu kumpinga!, huu ndio utaratibu wao wa CCM.

Kama by now CCM tayari inayo mgombea wa 2020 ambaye ni seating president, ataingia kwenye uchaguzi akiwa na presidential status, rights na all the presidential privileges, ikiwemo press, ving'ora, wasaidizi, msafara, magari ya umma ambayo yatabadili namba kuwekwa private number plates ili ku hoodwink wafadhili, then mtu huyu aje ashindane na mgombea yoyote, kutakuwa na ushindani kweli au igizo za ushindani?!.

Nchi za Scandinavia, incumbent akigombea, wanam scarp all his privileges, isipokuwa ulinzi, hivyo wagombea wote wanaingia kwenye uchaguzi wakiwa wanalingana, the playing field is level, watu wanashindana katika ushindani sawia, hivyo msindi anapatikana kwa haki. Uchaguzi wetu, mgombea mmoja anakuja na kingora akisindikizwa na dola kwa gharama za serikali, anashindana na mgombea with nothing, huu ni ushindani usio sawia, the playing ground is not level, unategemea nini?. Nasisitiza 2020 hakuna uchaguzi wa rais, tuna igizo la uchaguzi wa rais!.

Tukija kwenye wapiga kura, hivi unajua wapigakura wa Tanzani huwa wanachagua nini?. Mfikirie Magufuli wa 2020 anayeingia kugombea huku nyuma akiwa na track record yake ya
  1. Tanzania ya viwanda
  2. Barabara za juu kwa juu
  3. Treni ya umeme ya SGR
  4. Miondombinu ya mabarabara
  5. Miondombinu ya majengo
  6. Serikali ikiwa Dodoma
  7. Bomba la mafuta
  8. Uchumi wa gesi
  9. Nchi ya uchumi wa kati
  10. Ushindi wa vita vya rushwa-Tanzania bila rushwa
  11. Ushindi wa vita vya ufisadi-Tanzania bila ufisadi
  12. Elimu bure
  13. Tasaf itaongezewa uwezo kugawa zile njuluku double
  14. etc, etc,kuna mtu wa kushindana naye?.
Soma bandiko hili kwa makini, halafu lifikirie kwa real life scenario ya 2020
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020 ...

Paskali
 
Mkuu Utandu, hata wakikimbia chama wote, watu wa Kanda ya Ziwa pekee wanatosha kumrejesha Magogoni.

P.
Mayala ni wewe wazungumza haya? haipendezi na haikupendezi kauli hii kutoka kinywani mwako. Raisi ni wa watanzania wote na sio wa kanda Fulani. Ujumbe gani hasa unataka kutufikishia.
 
Sawa mkuu P, lkn wewe ni kioo cha jamii kulingana na taaluma yako.Hupaswi kushabikia ukanda hadharani.Tuipinge dhana hii kwa nguvu zote kwa mustakabali wa umoja wetu tulioachiwa na baba wa Taifa.
Mkuu Nisamehe, kiukweli, ukanda, udini na ukabila ni sumu mbaya sana katika jamii yetu, na mimi kama mwanahabari, nina wajibu wa kuelimisha umma kuhusu madhara ya hivi vitu kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo kuitumia jf.

Tafuta muda uzisome mada zangu hizi, na ukiweza pia karibu uchangie
Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ni ...
Tuhuma Za Ukabila: Wasukuma Sii Miongoni Mwa Makabila Yenye ...
Tupende, tusipende: Tanzania inanyemelewa na udini! | Page 42 ...
Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi! | Page 4 ...
Makabila makubwa vs Makabila madogo | JamiiForums | The Home of ...
Tanganyika, Sera ya MAJIMBO na kushindwa kwa hoja za CCM ...
Ni kweli kuna makabila yasiyotakiwa kutoa rais wa nchi? | Page 7 ...
Mkuu wa Mkoa wa Arusha na ukabila; Ukemewe na kila mmoja wetu ...


Paskali
 
Mkuu huo ndio ukomavu unaotakiwa. Tumeelimishana na kukubaliana kwa hoja.
Endelea kutupa mambo muhimu humu jf bila kuegemea itikadi za siasa. Tuipiganie nchi yetu kwa kuelimisha wasiojua,
kukosoa watendaji wanapokosea kiustaarabu na kukemea pale haki kwa wengine inapokosekana.
Ubarikiwe mkuu Paskali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…