kibori nangai
JF-Expert Member
- Jan 14, 2015
- 1,430
- 2,130
Kwani kamati hiyo ndio inatoa ithibatiiKamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Kilimanjaro inapaswa kukagua mradi wa ujenzi wa geti jipya la kuingia chuo cha polisi Moshi, na kujiridhisha kabla ya Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa hawajafika kuufungua. Hadi sasa, vyombo vya ndani vimefanya uchambuzi wa eneo hilo, lakini mradi huo haujakamilika. Usafi wa mazingira haupo katika kiwango kinachotakiwa, mitaro ya maji ya mvua bado haijajengwa, na kuna vumbi kubwa sana.
Aidha, ukuta wa mradi haujakamilika, na eneo hilo
halina huduma za maji wala umeme. Kuweka wazi, mradi unafunguliwa kwa kigezo gani ikiwa mazingira ni mabaya kiasi hiki?
Pia, thamani ya mradi kulingana na fedha zilizotumika haionekani kuwa sawa. Mandhari na mazingira ya eneo hili ni aibu kabisa.
Soma pia: IGP: Barabara za kuingia ndani ya Chuo cha Polisi Moshi Kilimanjaro,wajawazito wanashindwa kwenda kujifungulia zahanati ya chuo barabara ni mbovu.
Ni muhimu kutafakari hatua hizi kwa sababu kuna hatari ya kumjaribu Mheshimiwa Rais badala ya kumheshimu. Hali hii inaweza kupelekea aibu kubwa kwa chama na serikali.
Ni vyema kuchukua hatua za haraka ili kuhakikisha mradi huu unafikia viwango vinavyotakiwa kabla ya ufunguzi rasmi.
Wee Jeshi linautaratibu wake!
Hivyo acha kuropokaaa
Jeshi linautaratibu ushawai kusikia mkuu wa wilaya ameenda kwenye kambi yoyote