Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg Daniel Chongolo amewaagiza makatibu wa Wilaya zilizobainika kuwa na kasoro kwenye mchakato wa uchukuaji wa fomu katika uchaguzi ngazi ya shina kurudia uchukuaji huo maramoja,
Aidha, ameyataja baadhi ya maeneo yaliyobainika kuwa na changamoto hiyo kuwa ni pamoja na Wilaya ya Ubungo, Babati, Mbeya, na Tabora,
Katibu mkuu huyo amesema ni lazima haki itendeke ndani ya Chama kwa wanachama wote bila ubaguzi wa aina yeyote,
Maagizo hayo ameyatoa Aprili, 20, 2022 Dar es Salaam alipokuwa kwenye Mkutano wa Halmashauri ya CCM ya Wilaya ya Ubungo na Kinondoni,