Wakuu!
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, na Mwenza wa Urais wa chama hicho, Emmanuel Nchimbi, akizungumza na Wanahabari leo Agosti 11, 2025 katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba amesema, "Tukipokea kila aina ya mchango tutaainisha inapotoka."
"Lakini hatutapokea michango inayodhalilisha utu ama heshima ya Taifa. Tutapokea kila aina ya mchango kutoka kwa Watanzania. Atakayechanga Tsh.500, Tsh. 1,000, Tsh. Milioni moja wote tutapokea. Hata wale ambao hawana mapenzi na CCM tunawaomba na nyie mtuchangie."
Dkt. Nchimbi amesema maandalizi ya kampeni yanahitaji nguvu ya kifedha, ikiwemo ununuzi au ukodishaji wa magari, uchapishaji wa vipeperushi, mabango, tisheti, kanga, mafuta na gharama nyinginezo.
"Kwakuwa kila chama kinachoenda kwenye uchaguzi kinakuwa na maandalizi ya kampeni, na CCM inafanya hivyo na moja ya maandalizi muhimu kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kuwa na nguvu ya fedhaā, amesema Dkt. Nchimbi.
Amefafanua kuwa miezi michache iliyopita CCM ilitangaza idadi ya wanachama wake waliokuwa zaidi ya milioni 12, hatua iliyosababisha hamasa kubwa ya kutaka kuchangia kampeni. Hadi kufikia asubuhi ya Jumatatu, chama hicho kimefikisha wanachama waliosajiliwa kidijiti zaidi ya milioni 13.19.
"Sasa kutokana na hamasa ya wanachama wetu tumesema sasa tuwashirikishe sasa katika uchangiaji. Kwahiyo Kamati Kuu ya CCM iliamua tufanye harambee ya kutafuta fedha ambayo tunakusudia kuifanya keshoā¦katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan"
Harambee hiyo inatarajiwa kushirikisha wanachama wa CCM kutoka maeneo mbalimbali nchini pamoja na wadau wa chama hicho, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kukabiliana na ushindani wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.