Pre GE2025 CCM kufanya mkutano mkuu Januari 18 na 19 Dodoma, kumpata mrithi wa Kinana
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla amesema mkutano mkuu wa chama hicho utafanyika kati ya Januari 18 na 19, 2025 jijini Dodoma.
IMG_2329.jpeg
Katika mkutano huo utakaoongozwa na mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan kutafanyika uchaguzi wa makamu mwenyekiti-bara kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Abdulrahman Kinana.

"Maandalizi yote yamekwisha fanyika na kukamilika na tunajiandaa kupokea wajumbe wote wa mkutano mkuu. Karibuni sana Dodoma," amesema Makalla, leo Jumanne, Januari 7, 2025 alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.
 
Ndio kwenda kutangazwa kwa February Marope, au?
 
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla amesema mkutano mkuu wa chama hicho utafanyika kati ya Januari 18-19, 2025 jijini Dodoma.
View attachment 3194853
Katika mkutano huo utakaoongozwa na mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan kutafanyika uchaguzi wa makamu mwenyekiti-bara kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Abdulrahman Kinana.

"Maandalizi yote yamekwisha fanyika na kukamilika na tunajiandaa kupokea wajumbe wote wa mkutano mkuu. Karibuni sana Dodoma," amesema Makalla, leo Jumanne, Januari 7, 2025 alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.
Ndio kumziba nlomo JM wampe Makamu ? Basi sawa muda utasema yoote
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hayawi hayawi sasa yamekuwa.Mambo mazuri hayataki haraka,kwa kila jambo na majira yake na wakati kwa kusudi maalum chini ya Mbingu.

ile kiu ya Manilioni ya mamilioni ya Wafuasi, wakereketwa, wanachama na watanzania wa vyama vyote hapa Nchini kutaka kujua jina la Makamu Mwenyekiti wa CCM.atakaye chukua nafasi ya, watanzania ni Ndugu kanali Abadrihamani kinana inakwenda kukatwa na kupata majibu kuanzia wiki ijayo.

katika mkutano mkuu maalumu Utakao ongozwa na Mwenyekiti wetu wa CCM ambaye ndiye Rais wetu Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka ,jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini,shujaa wa Afrika na nuru ya wanyonge.

Mpaka sasa baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo na katibu wa Itikadi, uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Mheshimiwa sana CPA Amos Gabriel Makalla imeonyesha mitaani kote habari hiyo kuteka hisia za watu na mijadala yote ya kisiasa kutawaliwa na habari hiyo.

Hii ni kutokana na CCM kuwa ndio chama kilichobeba matumaini ya mamilioni ya watanzania na hatima ya Taifa letu. Ambapo pia ndio chama kinacho aminika na kupendwa , kukubalika na kuungwa mkono na wengi.

Tofauti na vyama kama CHADEMA ambavyo uchaguzi tu wa Mwenyekiti umekiacha chama kikiwa vipande vipande na kilichogawanyika mapande mapande,huku kila upande ukirusha maneno , vijembe na taarabu utafikiri watoto wa kidato cha tatu wanaosutana kwa umbeya.

Sasa wanashindana kutoa siri za chama na kudhalilishana hata kama walinunuliana vyakula migahawani.ni kama wanajenga mnara wa Babeli. Maana ni kama wamechanganyikiwa na kupigwa upofu wa akili na macho. Wakati wanafanya hayo upande wa pili CCM inaendelea kujikita katika kilele cha upendo katika mioyo ya mamilioni ya watanzania kwa kuendelea kuwasikiliza na kutatua kero zao. Halafu mwisho wa siku utasikia upinzani kama CHADEMA wanajibetua midomo na kusema wameibiwa kura.
IMG-20250107-WA0028.jpg

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla amesema mkutano mkuu wa chama hicho utafanyika kati ya Januari 18 na 19, 2025 jijini Dodoma.
View attachment 3194853
Katika mkutano huo utakaoongozwa na mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan kutafanyika uchaguzi wa makamu mwenyekiti-bara kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Abdulrahman Kinana.

"Maandalizi yote yamekwisha fanyika na kukamilika na tunajiandaa kupokea wajumbe wote wa mkutano mkuu. Karibuni sana Dodoma," amesema Makalla, leo Jumanne, Januari 7, 2025 alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.
View attachment 3195063
 
Attachments

  • IMG-20250107-WA0016.jpg
    IMG-20250107-WA0016.jpg
    142.4 KB · Views: 7
CCM itapata pigo kubwa sana mwaka huu, pigo moja tu, pigo takatifu, pigo lililonyooka.
 
Ili ajenge Ccm ya Matarajio atakapoondoka 2030 Mkutano huo ajaliwe haya Maono amteue Makamu wake kutoka Kanda ya Ziwa.

Mlale Unono 🇹🇿🙏
 
Wajumbe Mkutano Mkuu CCM Waitwa Dodoma; CCM Kufanya Mkutano Januari 18 & 19, 2025

MKUTANO Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unatarajia kufanyika Januari 18 hadi 19 mwaka huu ukiwa na ajenda tatu ikiwemo kuziba nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara.

Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya CCM katika ukumbi wa White House jijini Dodoma leo, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, amesema mkutano mkuu huo utakuwa na ajenda tatu.

Alizitaja ajenda hizo hizo ni kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa akishika nafasi hiyo Ndugu Abdulrahman Kinana,kupokea kazi za Chama kuanzia mwaka 2022 hadi 2025 pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji Ilani ya uchaguzi ya CCM.

Ameeleza kuwa taarifa hizo za utekelezaji ilani ni kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ)

Kuhusu mchakato wa kumrithi Kinana, amesema mrithi wa nafasi hiyo anatarajiwa kupatikana baada ya kamati kuu kuwasilisha mapendekezo ya jina kwa halmashauri kuu kisha halmashauri kuu kuwasilisha jina hilo kwa wajumbe wa mkutano mkuu kwa ajili ya kupigiwa kura.

"Kumekuwa na uvumi, unaona vichwa vya habari kwamba CCM patashika, wafuatao watajwa kurithi nafasi ya Kinana, nani kati ya hawa atachukua nafasi ya Kinana, wengine wanakwenda mbali kuandika wafuatao kuchukua nafasi ya Kinana. Kila mmoja anaandika navyotaka.

"Nataka kusema kwamba, nafasi ya Makamu Mwenyekiti haigombewi, unaposema kinyang'anyiro kinatoka wapi wakati nafasi haigombewi wala haijazwi fomu?," alieleza.

CPA Makala alisisitiza: "Tutampata makamu mwenyekiti baada ya mapendekezo ya kamati kuu na halmashauri kuu, kisha jina la atakayeziba nafasi hiyo litawasilishwa katika mkutano kuu na hapo ndipo zitapigwa kura ya ndiyo au hapana."

"Hatukuwa kimya, Chama kinaongozwa kwa katiba, kina utaratibu wake, hatuwezi kuongozwa kwa hisia za watu. Kwa sasa Kamati Kuu imeona ndiyo muda muafaka kujaza nafasi hiyo," alisema.

CPA Makalla alibainisha kuwa mkutano mkuu utatanguliwa na vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, vinavyotarajiwa kufanyika Januari 16 mwaka huu.
 
Attachments

  • WhatsApp Image 2025-01-07 at 21.34.45.jpeg
    WhatsApp Image 2025-01-07 at 21.34.45.jpeg
    176.6 KB · Views: 4
Hongera sana Sophia Mjema.

Hapa wenye D 2 ndiyo wataelewa.
 
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla amesema mkutano mkuu wa chama hicho utafanyika kati ya Januari 18 na 19, 2025 jijini Dodoma.
Katika mkutano huo utakaoongozwa na mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan kutafanyika uchaguzi wa makamu mwenyekiti-bara kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Abdulrahman Kinana.

"Maandalizi yote yamekwisha fanyika na kukamilika na tunajiandaa kupokea wajumbe wote wa mkutano mkuu. Karibuni sana Dodoma," amesema Makalla, leo Jumanne, Januari 7, 2025 alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

POWER IS INVARIABLY PERSONAL, THERE IS NO GROUP POWER.

SAMIA ANA JINA LAKE TAYARI. HII YOTE NI KUZUGA/DANGANYA TOTO IONEKANE DEMOKRASIA IMECHUKUA MKONDO WAKE! NEVER KWA MAMLAKA ALIYONAO RAIS KWA KATIBA HII KUWA NA GROUP POWER.
 
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla amesema mkutano mkuu wa chama hicho utafanyika kati ya Januari 18 na 19, 2025 jijini Dodoma.
Katika mkutano huo utakaoongozwa na mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan kutafanyika uchaguzi wa makamu mwenyekiti-bara kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Abdulrahman Kinana.

"Maandalizi yote yamekwisha fanyika na kukamilika na tunajiandaa kupokea wajumbe wote wa mkutano mkuu. Karibuni sana Dodoma," amesema Makalla, leo Jumanne, Januari 7, 2025 alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.
 
Attachments

  • 5922090-9996bee7eb09dbb87c6dad8817cfc87c.mp4
    16.1 MB

Mambo yanazidi hii si ndiyo siku ya mdahalo Chadema??
 
𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐌𝐊𝐔𝐔 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀

🗓️18 - 19 Januari, 2025 | 📍𝗗𝗼𝗱𝗼𝗺𝗮

𝗔𝗝𝗘𝗡𝗗𝗔 3;
1 𝑈𝑐ℎ𝑎𝑔𝑢𝑧𝑖 𝑤𝑎 𝑀𝑎𝑘𝑎𝑚𝑢 𝑀𝑤𝑒𝑛𝑦𝑒𝑘𝑖𝑡𝑖 𝑤𝑎 𝐶𝐶𝑀 𝑇𝑎𝑖𝑓𝑎

2 𝐾𝑢𝑝𝑜𝑘𝑒𝑎 𝑘𝑎𝑧𝑖 𝑧𝑎 𝑐ℎ𝑎𝑚𝑎 2022-2025

3 𝐾𝑢𝑝𝑜𝑘𝑒𝑎 𝑡𝑎𝑎𝑟𝑖𝑓𝑎 𝑦𝑎 𝑢𝑡𝑒𝑘𝑒𝑙𝑒𝑧𝑎𝑗𝑖 𝑤𝑎 𝐼𝑙𝑎𝑛𝑖 𝑦𝑎 𝑈𝑐ℎ𝑎𝑔𝑢𝑧𝑖 𝑦𝑎 𝐶𝐶𝑀 (2020/2025)

#𝐂𝐂𝐌𝐈𝐦𝐚𝐫𝐚
#𝐕𝐢𝐭𝐞𝐧𝐝𝐨𝐕𝐢𝐧𝐚𝐒𝐚𝐮𝐭𝐢
#𝐓𝐮𝐧𝐚𝐞𝐧𝐝𝐞𝐥𝐞𝐚𝐍𝐚𝐌𝐚𝐦𝐚
#𝐊𝐚𝐳𝐢𝐈𝐞𝐧𝐝𝐞𝐥𝐞𝐞
 
Attachments

  • 20250108_081053.jpg
    20250108_081053.jpg
    344.2 KB · Views: 4
  • 20250108_081055.jpg
    20250108_081055.jpg
    373.1 KB · Views: 4
MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU CCM YASHIKA KASI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ameongoza Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa kutembelea Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma ili kukagua maendeleo ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaotarajiwa kufanyika tarehe 18 na 19 Januari 2025.

Ukumbi huo, wenye uwezo wa kuchukua takriban watu 3,000, unakarabatiwa kwa kiwango cha juu ili kuhakikisha mazingira bora kwa mkutano huo muhimu. Mkutano huu utakuwa na agenda kadhaa, ikiwemo kumchagua Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), kufuatia kujiuzulu kwa Komredi Abdulrahman Kinana mwaka jana.

Balozi Nchimbi, akiwa ameambatana na Manaibu Katibu Mkuu wa CCM, John Mongella (Bara) na Dkt. Mohamed Said Dimwa (Zanzibar), pamoja na wajumbe wa Sekretarieti, alishuhudia kasi kubwa ya maandalizi hayo, huku akiwapongeza wahusika kwa jitihada zinazofanywa kuhakikisha kila kitu kinakuwa tayari kwa wakati.

Kwa mujibu wa Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, maandalizi ya mkutano huo yamefikia hatua nzuri. Alitangaza rasmi kuanza kwa maandalizi hayo jana, tarehe 7 Januari 2025, akibainisha kuwa mkutano huo utaongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan.
 
Attachments

  • IMG-20250108-WA0321.jpg
    IMG-20250108-WA0321.jpg
    975 KB · Views: 5
  • IMG-20250108-WA0322.jpg
    IMG-20250108-WA0322.jpg
    1.1 MB · Views: 4
  • IMG-20250108-WA0323.jpg
    IMG-20250108-WA0323.jpg
    1.5 MB · Views: 4
  • IMG-20250108-WA0324.jpg
    IMG-20250108-WA0324.jpg
    863.6 KB · Views: 4
  • IMG-20250108-WA0325.jpg
    IMG-20250108-WA0325.jpg
    973 KB · Views: 3
  • IMG-20250108-WA0326.jpg
    IMG-20250108-WA0326.jpg
    1.4 MB · Views: 5
  • IMG-20250108-WA0327.jpg
    IMG-20250108-WA0327.jpg
    953.8 KB · Views: 4
  • VID-20250108-WA0328.mp4
    10.2 MB
Back
Top Bottom