Pre GE2025 CCM kugawanyika kabla ya Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kasheku kashaingia Sema anaPush Hoja kwa chini chini..
Miongoni mwa hao Watu wapo Mawaziri na wengine sema aliyetusaliti Ni mmoja tu alikuw Kiungo Muhimu sana Makonda..

Sasa Ametusalitu halafu anataka Kutoa siri za Kambi...

Nakuhakikishia Kabla ya Uchaguzi wa Mtaa utagundua Mengi sana..

Hata wanaopush Ajenda ya Muungano sio Upinzani..
Upinzani ni Chombo tu cha Kutoa Sauti ila Mic haipo CHADEMA wala ACT
 
Ni uchambuzi mzuri sana tena una akisi mambo mengi ndani ya chama chetu cha mapinduzi. Kosa ambalo Dkt Samia (wakati mwingine nj vigumu pia kumlaumu kwa sababu ya mazingira) ni kuonesha waziwazi kumtwezwa Dkt Magufuli utu wake kwa kauli na kejeli ambazo ni kawaida watu kupigana vijembe ila tu shida ni mazingira ya kifo cha Dkt Magufuli ni kama yale ya vijijini watu kutishiana kuuana na mwisho wa siku mtu anakufa na jamii inaamini aliyemuua ni yule anayesherehekea kifo cha mhusika. Dkt Samia alikosa strategic thinkers kwa upande wa siasa namna ambavyo alitakiwa aenende na kuishi na makunfi yote bila kuyakwaza. Matokeo yake alijitahidi kulifurahisha kundi moja lile la 2025 na kulisagia kunguni kundi la Dkt Magufuli na kibaya kauli zenye dhihaka dhidi ya Dkt Magufuli ni nyingi sana zilizowahi kutolewa na serikali yake. Kilio cha Makonda kwenye kaburi la Dkt Magufuli kiligusa sana watanzania kwa kuona aha kumbe CCM inamkubali Dkt Magufuli. Pamoja na yote, Dkt Magufuli alizidiwa na makundi ya uharifu ndani ya uongozi wake. Yaani mfano suala la BOT na Bureau de change, watu wake waliona fursa ya kuonea hata wale innocent na matukio mengine.
 
Ngoja tusubiri yetu MAJICHO
 
CDM kama ni wajanja.. watumie mwanya huu mapema wasimtweze sana Magufuli ili wamtumie kupata kura siasa ni sayansi na kwenye siasa hakuna adui wa kidumu. Wakubali kuishi na shetani kimkakati wavune kura na kupata watakacho. suala la Katiba,Muungano na uzanzibar,Raslimali zetu yote ni kaa la moto kwenye uchaguzi huu na ni kete au agenda muhimu kwa CDM watanganyika kwa sasa wanaanza kuelewa
 
Yote 100, lakini moja kubwa ni kwamba ccm itaendelea kushika Dola! Huo ndio ukweli, watu mtafanya uchambuzi na kuleta utabiri wa kila aina ila ccm, itaendelea kushika madaraka!
 
Umeona mbali sana !
Ukweli ni kwamba na mimi pia ni katika wale ambao hatukubaliki kutokana na misimamo yetu ya kukataa Chama kuwa kama kokoro !

Hivyo tumeamua kujibanza kwa mhe Samia !

Ngoja tusubiri tuone ! šŸ™šŸ™šŸ™
 
CCM tayari imegawanyika. Ni suala la wakati tu ili kila kundi lipate kiongozi wake.
 
Hawa ni manyangau, watakaa na kuulizana: sasa tunakosana ili chadema ichukue nchi tutakula wapi? Then watakuja na solution ya kugawiana vyeo na hivyo kuwa kitu kimoja.......go deep in thinking.....
 
CCM imekuwa kama gunia la viazi toka Njombe. Ngunia limebeba vikubwa, vibovu, vidogo, visivyokomaa na vinavyotaka kuota
 
CCM ilishagawanyika kiitikadi,

Kifo cha Magufuli was catalysist ya CCM kuwahi kufa, bila Jeshi kuingilia Wakina Bashiru na Polepole ni zaidi ya Putin kwenye Ujamaa Kikwete angenyongwa na Washirika wake.

Pia hii chance bado ipo, Wajamaa bado wananguvu na wakiingia Madarakani tena lazima kinga ya Rais itolewe
 
Hawa ni manyangau, watakaa na kuulizana: sasa tunakosana ili chadema ichukue nchi tutakula wapi? Then watakuja solution ya kugawiana vyeo na hivyo kuwa kitu kimoja.......go deep in thinking.....
Imeshatokea kwingineko na inaweza ikatokea kwao pia !
Hawana uwezo wa kuwagawia vyeo watu wao wote !
 
Imeshatokea kwingineko na inaweza ikatokea kwao pia !
Hawana uwezo wa kuwagawia vyeo watu wao wote !
Tatizo kubwa Wana CCM wanaishi kimazoea sana. Wanajiaminisha kuwa Kila wakati watasuluhishana ili wagawane madaraka.

Kumbe wakati huu hawana msuluhishi kati yao.

Kama balozi Karume tu aliwapelekesha kule Zanzibar, jee hawa wa Tanganyika watawaweza??
 
Hizi ndoto huwa naziota nikishiba mihogo ya kuchoma na maji ya Kandoro.
 
Mimi naombea isiishie kwenye kugawanyika tu! Badala yake ingekufa kabisa.
Haiwezekani kikundi cha watu wachache waishi kama vile wako peponi, halafu kundi linalobakia la watu wengi waishi kama vile wako jehanamu.
 
Wasigawanyike tu ila wagawame,fito,nyasi,mbao,bati na hata nyasi ili kila mmoja afe na chakeee🤪
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…