Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Tukio la Kutenguliwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu Alhaji Dr. Yahaya Nawanda baada ya tuhuma za kulawiti binti mwenye umri wa miaka 21 Mwanafunzi wa chuo kikuu cha SAUT Mwanza kwenye maegesho ya THE CASK BAR ni moja Kati ya matukio mengi yanayofanaywa na viongozi wateule wa Rais Kwa kutegemea kinga ya nafasi zào na hasa Chama wanachokitumikia.
Imekuwa kawaida maeneo mbalimbali Wakuu wa mikoa na wilaya kujimilikisha maeneo Kwa kudhulumu Wananchi masikini, kuweka Wananchi mahabusu Kinyume cha sheria lakini Kwa kutegemea kinga ya Chama wanaamini hawatachukuliwa hatua.
Mitaani, vijinini na maeneo mengi mikoani viongozi wa CCM wameelekezwa na viongozi wao kitaifa kwamba wao ni watawala wa Kila kitu. Diwani wa CCM anaweza kumkoromea OCD na akanywea. Mwenyekiti wa CCM wilaya anaweza kumpigia simu RPC àkamwamuru mtuhumiwa aachiwe hata kama anajua ana kosa naye akatekeleza. Ngazi ya DC na RCs ndo hatari zaidi maana wanajiita wenyeviti wa Ulinzi na usalama. Ni mara nyingi tunawasikia wanatishia Wananchi kwenye mikutano ya hadhara Kwa kosa la kuuliza maswali magumu.
Rais asipowaeleza waziwazi kwamba hatawabeba Wahalifu Kwa Kisingizio cha Kulinda Chama tutegemee mengi zaidi ya hili la Nawanda, Gekul na DED wa Mafia.