Kilchompata Catherine kinaweza mpata mwanamke yeyote yule, hata Mimi nilianzisha mahusiano na mwanaume aliniambia Hana mke walishaachana. Na akawa haishi nae. Nikiwa na mimba ya miezi Saba mke alikuja kwangu na vyeti vya ndoa,,, mke ni mkatoliki, mume mkatoliki na Mimi mkatoliki.
Haraka Sana nilivunja hayo mahusiano simply because
1. nilijua kwa Sheria ya dini yetu ni ngumu Mimi KUISHI kwa amani.
2. Nilifikiria mistakabal wa watoto na familia ya yule baba.
3. Niliona ujinga Mimi KUISHI na mwanaume ambae ndoa yake Bado haijavunjika na mkewe Bado anampenda, na nliwaza mbali hivi akifa ntakua mgeni wa Nani mimi??? Mpaka Leo yule mwanamke tunaheshimiana na anamtambua mwanangu na wanae wananiheshimu na nilimpata mwanaume wangu ambae sio mume wa MTU na maisha yanasonga.
Sasa najiuliza kama Mimi raiya wa kawaida niliweza kufanya hivi, mbunge kwanini alishindwa kujitambua??? Na mbaya zaidi yeye ni mbunge wa Wanawake,,, yeye analo JUKUMU la KUTETEA WANAWAKE na maslahi yao,,, sasa amefanya nini??? Na sio kwamba hajijui, Kuna video inasambaa anaomba Mungu ili awe official Mrs madodo, anakua kabisa yeye sio official wife, why alete taharuki misibani??
Kibaya zaidi kinachonikera Mimi ni wale viongozi wa Wanawake wakiongozwa na mwenyekiti walishindwa kutumia busara na hekima na kufanya mambo kistaarabu?? Je waliwawaza wale watoto wadogo wa marehemu pale msibani??? JASMIN BACHU TOKA HADHARAN UTUTAKE RADHI WANAWAKE WA ARUSHA.
Vipi KUHUSU ile ibada??? Kwa nini hawakuheshimu?? Na mbunge kama anampenda marehemu na alitaka azikwe kwa heshima anafahami SHERIA za kanisa katoliki?? Hawaziki MTU MWENYE mitala, YAni they are very strict kwenye hili, sasa anajuaje waliogopa kumshirikisha Ili marehem azikwe kwa heshima???
Kamwe usiskilize blabla za mwanaume eti oo nimeachana na mke wangu kisa malaya na WEWE unashkilia Hicho unajiaminisha kwamba HUYU wangu.
CATHERINE NI MBUNGE MTUNGA SHERIA, WAKATI MWINGINE ANAWAJIBIKA KUSIMAMIA SHERIA. KUISHI NA MUME WA MTU TENA MWENYE NDOA YA KIKATOLIKI AMBAYO HAIVUNJIKA HAKUKUFANYI UWE MKE KAMILI NA UWE NA HAKI YA KUMZIKA MUME AKIFA.