CCM kutoa form ya Urais kabla ya kumpumzisha Ndugai ni kutoka na utu na aibu

CCM kutoa form ya Urais kabla ya kumpumzisha Ndugai ni kutoka na utu na aibu

Utaweza kuacha kufanya mtihani wa f4 au f6 kisa umefiliwa na mzazi wako ?

Maisha lazima yaendelee
Uzi unazungumizia zoezi la uchukuaji fomu lisitishwe kwanza tumpunzishe Spika Ndugai
 
Daah kwa hiyo mkuu utataka hata treni ya SGR isimame kwenda Dodoma mpaka mazishi yapite kisa wao walioidhinisha fedha za kujengwa wamekufa tutasimamisha kila kitu basi..
Kwani SGR mali ya umma, unalinganisha na ratiba ya ghafla ya kuchukua hiyo fomu
 
Kwani asipokuwepo ulomtaja hawezi kupumzishwa?
Sijamtaja mtu
Nimesema zoezi la uchukuaji fomu
Kwakuwa marehemu alikuwa Spika, MNEC na mwanachama mwaminifu ingekuwa busara tupumzishe baadaye tuje tuendelee na taratibu zingine ndani ya Chama
 
Nafikiri anafanya hivyo sababu ya kupunguza uvumi wa kuchukua form peke yake. Taarifa isiwe kubwa watu watakuwa na stori mbili za mazishi na fomu.
 
Spika wa bunge, mbunge na mwanachama wa CCM Bado hajazikwa, CCM mshatangaza kukabidhi fomu ya mgombea wenu pekee na asiyepingwa hiyo kesho

Job Ndugai na bunge lake ndo alitoa budget ya kujenga bwawa la mwalimu Nyerere, SGR na kivuko cha Busisi

Bila shaka inasemekana uchukuaji fomu utaambatana na hafla fupi

Hii siyo hekima, tulitegemea CCM na ukongwe wao watoe mwanga kumbe wanavurunda,

Kwa heshima na utumishi wa Job Ndugai isengefaa hilo tukio lenu mlifanye miwili wake ukiwa Bado mortuary

Kauli yake ya HII NCHI ITAPIGWA MNADA ndo Bado mna hasira nae vifuani kwenu

Mkija eti mnakemea walioshangilia kifo cha Ndugai kumbe Kwa matendo yenu na nyie huko maofsini mnashangila kimya kimya
waache wafu wazike wafu wao masiisiiemu ukiyaambia ukweli tu imekula kwako na mtu alikuwa wakwao tena mkuu wa muhimili lakini hawana habari naye kisa alimwambia mama yao ukweli.
 
Spika wa bunge, mbunge na mwanachama wa CCM Bado hajazikwa, CCM mshatangaza kukabidhi fomu ya mgombea wenu pekee na asiyepingwa hiyo kesho

Job Ndugai na bunge lake ndo alitoa budget ya kujenga bwawa la mwalimu Nyerere, SGR na kivuko cha Busisi

Bila shaka inasemekana uchukuaji fomu utaambatana na hafla fupi

Hii siyo hekima, tulitegemea CCM na ukongwe wao watoe mwanga kumbe wanavurunda,

Kwa heshima na utumishi wa Job Ndugai isengefaa hilo tukio lenu mlifanye miwili wake ukiwa Bado mortuary

Kauli yake ya HII NCHI ITAPIGWA MNADA ndo Bado mna hasira nae vifuani kwenu

Mkija eti mnakemea walioshangilia kifo cha Ndugai kumbe Kwa matendo yenu na nyie huko maofsini mnashangila kimya kimya
Ona hii nyumbu. INEC imeshatoa ratiba ya vyama kuchukua fomu. Hiyo ratiba haiwezi kuahirishwa kwa sababu ya kufiwa. Muwe mnajielemisha kwanza kabla ya kuropoka.
 
Ona hii nyumbu. INEC imeshatoa ratiba ya vyama kuchukua fomu. Hiyo ratiba haiwezi kuahirishwa kwa sababu ya kufiwa. Muwe mnajielemisha kwanza kabla ya kuropoka.
Deadline ni lini?
 
Fomu zinatolewa na Tume,
 
Hujasikia tangazo la tume huru kuhusu kuchukua fomu? Tuwe logical kidogo tuache mihemuko
 
Hiyo fomu haitolewi na CCM, kule CCM Maza aliruka hizo process za fomu.

Anachukua fomu INEC.
 
Back
Top Bottom