Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
CCM inazindua rasmi kampeni za uchaguzi ujao siku ya Jumamosi katika viwanja vya jamhuri mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Magufuli anatarajiwa kutikisa kitovu hicho cha nchi mji wa Dodoma na vitongoji vyake kwa hotuba yake ilopangwa maalum kwa siku hiyo.
Katibu wa CCM wa mkoa wa Dodoma bi Pili Mbanga amethibitisha habari uzinduzi wa kampeni hiyo na kusisitiza kwamba uzinduzi huo utakuwa ni wa aina yake.
Uzinduzi wa Jumamosi utakuwa ni wa mara ya kwanza kwa CCM kuanzisha kampeni ndani ya makao makuu ya Chama Cha mapinduzi na makao makuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa tume ya Uchaguzi NEC uzinduzi wa kampeni kiufundi ulianza tarehe 26 August 2020, hivyo wagombea wote walopitishwa kugombea nafasi mbalimbali ikiwemo nafasi ya uraisi wa JMT wanaruhusa ya moja kwa moja kuanza kampeni.
Vyombo mbalimbali vya habari vimealikwa kuhudhuria uzinduz huo na kuuonyesha moja kwa moja kutoka Dodoma.
Televisheni au "Telly" ya Taifa TBC inatarajiwa kurusha matangazo ya uzinduzi huo yatakayoonekana nchi nzima, moja kwa moja yaani "Live" kutoka mjini Dodoma.
CCM mwaka huu inaingia katika kampeni bila kutegemea sana migogoro ya wapinzani ambayo iliwanufaisha kwa kiasi kikubwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.
Mpaka sasa ni jambo lisilo ubishi kwamba CCM inajiamini kwa aina ya serikali ilounda ambayo imejikita katika kutekeleza kwa vitendo miradi mingi ya maendeleo ambayo haihitaji mtu kuitafuta bali yote yaonekana wazi.
Miundombinu mbalimbali kama madaraja na maboresho na ujenzi wa reli mpya, mradi wa umeme vijijini na kufikiwa kwa malengo ya ukusanyaji kodi ni miongozi mwa sera za CCM ambazo iliziahidi ingezitekeleza na imefanya hivyo.
Wananchi wa Tanzania hivi sasa wanasubiri kumsikia Rais John Magufuli atazungumzia masuala yepi siku ya Jumamosi huku akiomba kuendelea na miaka mingine mitano ya kuiongoza Tanzania.
Ni siku ya Jumamosi tarehe 20, August 2020 ndio itakayotoa khasa makusudio ya CCM kutaka tena kuongoza nchi hii kupitia kampeni zake zitakazoichukua kuzunguka tena katika mikoa mbalimbali.