LGE2024 CCM: Lazima mkubali mambo yanabadilika na humuwezi kuwadanyanya watu siku zote

LGE2024 CCM: Lazima mkubali mambo yanabadilika na humuwezi kuwadanyanya watu siku zote

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

sambulugu

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2021
Posts
4,485
Reaction score
8,562
CCM ni chama kikubwa chenye historia kubwa ndani ya nchi na nje ya nchi lakini nashauri yafatayo!

CCM kwenye chaguzi kuanzia 2019 imekuwana na woga kushindana na vyama vingine na kupelekea watu wengi kuona zoezi la uchaguzi halina maana

CCM itambue kizazi kinabadilika na kusema kweli watu wengi wanataka mabadiliko yatayotoka ndani ya CCM au ndani ya upinzani kwa maana ya watu kuchoka kuwa chini ya chama kimoja na hiyo ni hulka ya binadamu kwa asili!

CCM kujiandaa kwa miaka ijayo kwa maana wahenga wanasema huwezi kuwadanganya watu muda wote,Nasema hayo kwa maana haitawezekana miaka yote kuwa na uchaguzi wa namna hii na mapungufu yake kwa maana sio asili ya mambo!

CCM inapaswa kutoogopa kabisa ushindani kwa sababu hata nchi zilizoendelea vyama hutawala kwa sera nzuri zinazokubalika na wananchi si kwa kufanya figisu au ujanja ujanja wa kisingizio cha watu kukosea kujaza fomu. Kuogopa uchaguzi ni ishara ya chama kuchoka na kuongeza chuki katika jamii.

CCM itambue viongozi wengi wanaopita bila kupingwa kwa maana ya kukosa wapinzani hawawezi kukijenga chama katika jamii kwa maana viongozi watokanao na uchaguzi kama huo huwa sio chaguo la wananchi.

CCM ina faida kubwa moja ina mtaji wa vipaji vingi vya uongozi na wachama wengi katika vijana,watu wa makamo na wazee.Kitu hichi kinaifanya CCM kuwa ni chama imara ila kinapungukiwa na viongozi shupavu wa kushindani.

CCM itambue ushindani halali ndo pekee utaifanya CCM kuwa imara na sivinginevyo maana ushindani huleta ushindi halali na kuheshimika na jamii!

CCM ikumbuke kabla ya 2015 wanachama walikuwa wanaogopa kutembea wakiwa wamevaa nguo za kijana kwa maana zomea zomea ilikuwa nyingi sana.

CCM hamjachelewa kuruhusu Ushindani kwa maana ushindani katoka uongozi ni kama damu katika mwili bila ushindani kinachofata ni mauti!

Niwatakie pole wote waliopata changamoto katika kipindi hiki cha uchaguzi!

Mungu awabarikini nyote!

View: https://youtu.be/doU05kVEoz0?si=Q8-XtN2cXCOHqHHs
 
Naona Aisha kakomaa hadi kieleweke...

Hao wasimamizi wa uchaguzi walivyokula ganzi, kama watu vile...
 
Kwan wamemdanganya nan ndugu nyosha maelezo
Kama hujaona hadaa tangu zoezi la uandikishaji wapiga kura,kuengua wapinzani kwa vigezo visivyokubalika kisheria na kikanuni na kuingiza kura fake kabla hata zoezi la upigaji kura kuanza basi wewe ni mpumbavu.
 
Back
Top Bottom