LGE2024 CCM: Lazima mkubali mambo yanabadilika na humuwezi kuwadanyanya watu siku zote

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Hoja gani ujanja ujanja leo huku watu hawajatokea kituoni ila Sanduku limejaa kura nimecheka sana
Hahhaha mara mtu anakamatwa na kura tayari zishapigwa! Unajiuliza kazipata wapi huyu? Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni
 
“Viongozi wabaya ni wale wanaochaguliwa na raia wema wasioshiriki kupiga kura.” ~ George Jean Nathan
 
CCM ni chama kikubwa chenye historia kubwa ndani ya nchi na nje ya nchi lakini nashauri yafatayo!

CCM kwenye chaguzi kuanzia 2019 imekuwana na woga kushindana na vyama vingine na kupelekea watu wengi kuona zoezi la uchaguzi halina maana

CCM itambue kizazi kinabadilika na kusema kweli watu wengi wanataka mabadiliko yatayotoka ndani ya CCM au ndani ya upinzani kwa maana ya watu kuchoka kuwa chini ya chama kimoja na hiyo ni hulka ya binadamu kwa asili!

CCM kujiandaa kwa miaka ijayo kwa maana wahenga wanasema huwezi kuwadanganya watu muda wote,Nasema hayo kwa maana haitawezekana miaka yote kuwa na uchaguzi wa namna hii na mapungufu yake kwa maana sio asili ya mambo!

CCM inapaswa kutoogopa kabisa ushindani kwa sababu hata nchi zilizoendelea vyama hutawala kwa sera nzuri zinazokubalika na wananchi si kwa kufanya figisu au ujanja ujanja wa kisingizio cha watu kukosea kujaza fomu. Kuogopa uchaguzi ni ishara ya chama kuchoka na kuongeza chuki katika jamii.

CCM itambue viongozi wengi wanaopita bila kupingwa kwa maana ya kukosa wapinzani hawawezi kukijenga chama katika jamii kwa maana viongozi watokanao na uchaguzi kama huo huwa sio chaguo la wananchi.

CCM ina faida kubwa moja ina mtaji wa vipaji vingi vya uongozi na wachama wengi katika vijana,watu wa makamo na wazee.Kitu hichi kinaifanya CCM kuwa ni chama imara ila kinapungukiwa na viongozi shupavu wa kushindani.

CCM itambue ushindani halali ndo pekee utaifanya CCM kuwa imara na sivinginevyo maana ushindani huleta ushindi halali na kuheshimika na jamii!

CCM ikumbuke kabla ya 2015 wanachama walikuwa wanaogopa kutembea wakiwa wamevaa nguo za kijana kwa maana zomea zomea ilikuwa nyingi sana.

CCM hamjachelewa kuruhusu Ushindani kwa maana ushindani katoka uongozi ni kama damu katika mwili bila ushindani kinachofata ni mauti!

Niwatakie pole wote waliopata changamoto katika kipindi hiki cha uchaguzi!

Mungu awabarikini nyote!

View: https://youtu.be/doU05kVEoz0?si=Q8-XtN2cXCOHqHHs

CCM inazikwa taratibu na wenye tamaa ya madaraka. Wao watapita CCM itabaki ikiwa taabani kwa kashfa mbalimbali.
 
kwa aina ya upinzani ulivyo,

na kwa namna CCM inavyotumia sayansi na tecknologia ya siasa kujiimarisha,

hakuna dalili wala ishara, kwamba eti siku moja CCM itashindwa uchaguzi na chama kingine cha siasa kushika hatamu.

gubu na makasiriko ya kushindwa uchaguzi haziwezi kubadilisha chochote au kuudhoofisha CCM imara uliyojipanga kushindwa kushika hatamu tena na tena 🐒
 
nawapongeza polisi kwa kuimarisha amani kipindi hiki cha uchaguzi

pia nawapongeza wanachama wenzangu wa chama cha mapinduzi kwa ushindi wa kishindo maeneo mengi nchi hakika watanzania wameonyesha ukomavu kisiasa kwa kuchagua kilicho bora
 
CCM inapaswa kutoogopa kabisa ushindani kwa sababu hata nchi zilizoendelea vyama hutawala kwa sera nzuri zinazokubalika na wananchi si kwa kufanya figisu au ujanja ujanja wa kisingizio cha watu kukosea kujaza fomu. Kuogopa uchaguzi ni ishara ya chama kuchoka na kuongeza chuki katika jamii.
Figisu ni hatua ya mwisho ya mtu aliyefeli....akiishiwa hii mbinu basi anaondoka mazima maan hana option nyingine
 
Back
Top Bottom