Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Ikiwa kumesalia mwezi mmoja tu kufanyika kwa uchaguzi mkuu, hali ya CCM kwenye jimbo la Temeke ni dhoofuli hali, Mgombea wake aliyeshindwa kura za maoni na Abbas Mtemvu aitwaye Dorothy Kilave hawezi kushinda uchaguzi kwa vile hajulikani na wapiga kura wala hajulikani hata anakoishi, hana ushawishi wala hana hata uwezo wa kupiga kampeni.
Taarifa zingine zinaonyesha kwamba makundi na makovu ya kura za maoni ndio yaliyomteketeza, wapambe wa Mtemvu ambao ni 75% ya wanaccm wote wa jimbo hilo wamejiapiza kutomchagua mama huyo mjane aliyefiwa na mumewe miaka michache iliyopita kwa madai kwamba mama huyo ni chaguo la Makao Makuu na wao hawahusiki naye, hatima yake iko mikononi mwa Tume kwenye uchakachuaji.
Bali njia ni nyeupe kwa Mgombea ubunge wa CHADEMA.
Ambaye duru zinaonyesha kwamba ni mtoto halisi wa Temeke mwenye vinasaba vya Mtoni kwa Azizi Ally na Yombo Buza , maeneo yanayoaminika kuwa na wakazi wengi mno na wapiga kura , huku umaarufu wa Chama chake cha Chadema , chama kinachohubiri maendeleo ya watu na uhuru ukimbeba .