Kama anafaa au hafai, ni lazima watu wakumbuke.
Ili, kama anafaa, kwa kadiri anavyofaa, mazuri yake yadumishwe, na kama hafai, kwa kadiri asivyofaa, mabaya yake yaepukwe.
Pinga hoja, usipinge mtu kuzungumziwa. Kama wanachakachua historia, weka sawa. Lakini usiseme kwa nini mnamuongelea Magufuli mtu kashafariki. Mtu akifariki si mwisho wa kuongelewa. Kuna wengine wanaona ndiyo mwanzo wa kuongelewa, kwa sababu kumuongelea mtu maisha yake kabla hajayamaliza anaweza kubadilika, akifariki ndiyo hawezi kubadilika.
Kwa nini unaona watu kukumbusha historia ni jambo baya as long as kinachokumbushwa ni kweli?
Rais Mwinyi ametuachia somo kwamba maisha ya mtu ni hadithi, ishi ili hadithi yako iwe nzuri watu wakihadithia ulivyoishi, usiache aibu.
Sasa watu wakisimulia hadithi za mtu tatizo liko wapi?
Umeshindwa kufikiri kidhahania kwamba hayo mazuri ya huyo mtu yanaweza kuwapa darasa wengine la kuyafuata, au kama mabaya, yanaweza kutoa darasa la kuyaepuka?
Unataka mtu akifa asizungumziwe tena?
Rais aliyeongoza mamilioni ya watu akifa asizungumziwe tena?
Unaelewa kuna simulizi wa Wafalme waliokufa maelfu ya miaka, wa Kirumi, Kiyunani, Mafarao wa Misri, mpaka leo watu wanazisimulia kujifunza kutokana na maisha yao?
Watu wanaandika habari za Caesar, Augustus, Nero, Caligula, Alexander the Great, Darius, Rameses, Ptolemy, Genghis Khan, Napoleon, Washington, Hitler, Martin Luther King Jr., Kennedy.
Mpaka leo.
Wewe unashangaa habari za Magufuli kafariki juzi hapo? Hata watu hawajamuandikia biographies za maana za kuchambua maisha yake.
If anything Tanzania hatujamuongelea vya kutosha Magufuli. Hatujamuongelea kwa kina kuchambua mazuri na mabaya yake, tuepuke mabaya yake yasijirudie na mazuri yake tuyaenzi na kuyaendeleza.