Pre GE2025 CCM mnataka hayati Magufuli agombee 2025?

Pre GE2025 CCM mnataka hayati Magufuli agombee 2025?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Baada kufa shujaa, wafuasi wake wameshindwa kumpachika mtu wao kwa sababu za kikatiba, maana Katiba iliwabana.
Sassa wameona Katiba ya CCM inawpa nafasi kuweka mtu wao.
Kwakuwa nafasi hiyo ipo waachwe watumie haki yao
 
Kimsingi,

Magu amefariki, ila viatu vyake kiuongozi hakuzikwa navyo,

Sa100 alipovitest alikiri wazi kuwa havimtoshi, ni vikubwa mno😀

Hiyo ndiyo sababu ya kelele za wananchi, wanataka apatikane mtu wa kuvivaa viatu vile na kuifikisha Tanzania Ile aliyoiona Magu,

Tanzania Tajiri yenye Kutoa misaada Kwa nchi maskini za Ulaya.
 
Bado hujajibu hoja... Kukumbuka yaliyopita hakuwezi kuwa Sawa na Harakati za kuonesha huyu ndiye anafaa.
Kama anafaa au hafai, ni lazima watu wakumbuke.

Ili, kama anafaa, kwa kadiri anavyofaa, mazuri yake yadumishwe, na kama hafai, kwa kadiri asivyofaa, mabaya yake yaepukwe.

Pinga hoja, usipinge mtu kuzungumziwa. Kama wanachakachua historia, weka sawa. Lakini usiseme kwa nini mnamuongelea Magufuli mtu kashafariki. Mtu akifariki si mwisho wa kuongelewa. Kuna wengine wanaona ndiyo mwanzo wa kuongelewa, kwa sababu kumuongelea mtu maisha yake kabla hajayamaliza anaweza kubadilika, akifariki ndiyo hawezi kubadilika.

Kwa nini unaona watu kukumbusha historia ni jambo baya as long as kinachokumbushwa ni kweli?

Rais Mwinyi ametuachia somo kwamba maisha ya mtu ni hadithi, ishi ili hadithi yako iwe nzuri watu wakihadithia ulivyoishi, usiache aibu.

Sasa watu wakisimulia hadithi za mtu tatizo liko wapi?

Umeshindwa kufikiri kidhahania kwamba hayo mazuri ya huyo mtu yanaweza kuwapa darasa wengine la kuyafuata, au kama mabaya, yanaweza kutoa darasa la kuyaepuka?

Unataka mtu akifa asizungumziwe tena?

Rais aliyeongoza mamilioni ya watu akifa asizungumziwe tena?

Unaelewa kuna simulizi wa Wafalme waliokufa maelfu ya miaka, wa Kirumi, Kiyunani, Mafarao wa Misri, mpaka leo watu wanazisimulia kujifunza kutokana na maisha yao?

Watu wanaandika habari za Caesar, Augustus, Nero, Caligula, Alexander the Great, Darius, Rameses, Ptolemy, Genghis Khan, Napoleon, Washington, Hitler, Martin Luther King Jr., Kennedy.

Mpaka leo.

Wewe unashangaa habari za Magufuli kafariki juzi hapo? Hata watu hawajamuandikia biographies za maana za kuchambua maisha yake.

If anything Tanzania hatujamuongelea vya kutosha Magufuli. Hatujamuongelea kwa kina kuchambua mazuri na mabaya yake, tuepuke mabaya yake yasijirudie na mazuri yake tuyaenzi na kuyaendeleza.
 
Kwa hiyo na wewe umeamua uungane nao kwa kuja kutangaza hapa jukwaani?
Hawa watu wasiompenda Magufuli wanaoumizwa anapoongelewa Magufuli mimi nawashangaa sana.

Kwanza sielewi wanaumizwa na kipi. Wanaona wivu Magufuli akiongelewa?

Pili, kama kweli hawampendi Magufuli, presumably na CCM, mimi ningetegemea wafurahie wana CCM kumuongelea Magufuli ambaye amefariki (kwa sababu hawezi kugombea kwenye uchaguzi) na wao waitumie fursa hiyo kumnadi mgombea wao.

Sasa, badala ya wao kumnadi mgombea wao, na wao wanajiunga kumuanzishia uzi Magufuli.

Hapo ndipo swali lako linakuwa na uzito.

Mtu anaponda watu kumuongelea Magufuli. Badala ya yeye kuanzisha uzi wake atuambie habari za mgombea wake, anaunga tela kuanzisha uzi wa kumuongelea Magufuli.

This is a contradiction.
 
Miafrika pasipo kuipelekesha kama punda kwa mijeledi na fimbo akili hazikai sawa, tunahitaji kama JPM anyooshe hizi ngedere kwa miaka kama 40 hivi.
Mkuu,

Hapo huwezi kujenga chochote cha maana. Utatumia nguvu kubwa na gharama nyingi sana kujenga kitu artificial sana ambacho kikipigwa na upepo kidogo tu kitavunjika.

Hayo ndiyo mambo aliyotaka kufanya Nyerere kulazimisha watu waende kwenye vijiji vya Ujamaa, badala ya kuwavutia waende wenyewe kwa kuona faida.

Tatizo letu wengi tunaopenda kutumia nguvu badala ya akili.

Yani wewe kwa sababu tu una nyundo, kila tatizo unataka kulimaliza kwa kulipiga nyundo, hata ukuwashwa korodani tu unataka kuzipiga nyundo.

Huo mfumo wako wa mtu mmoja kukaa juu na mjeledi kulazimisha watu wafanye hivi na vile, wakati watu hawaelewi wanafanya hivi na vile kwa nini, siku huyo mtu akiondoka na alichotaka kujenga kinatoweka.

Asili ya watu ni kupenda uhuru, ukilazimisha kitu, hata kizuri, watakiona kibaya.
 
Tuliosoma falsafa na historia tumekutana na hoja kwamba mtu hafariki mpaka siku mtu wa mwisho anapoacha kumuwaza.

Yani ukimfikiria, ukimkumbuka, ukimtaja, anaendelea kuishi katika mawazo yako.

Labda wanataka Magufuli aendelee kuishi katika mawazo ya watu.

"No one is finally dead until the ripples they cause in the world die away, until the clock wound up winds down, until the wine she made has finished its ferment, until the crop they planted is harvested. The span of someone’s life is only the core of their actual existence."

Terry Pratchett, Reaper Man (Discworld, #11; Death, #2)

Falsafa za kishirikina hizi
 
Falsafa za kishirikina hizi
Hapana,

Wewe ndiye umejibana na kutoelewa muktadha na kulazimisha ushirikina.

Mimi siamini ushirikina. Ushirikina ni ujinga mtupu.

Lakini, hilo halinizuii kuelewa kwamba, ukimtaja Magufuli tu, kumbukumbu yake inaendelea kuishi kwenye mawazo.

Anakuwa si mtu aliyesahaulika kama babu wa babu wa babu wa babu wa babu yako ambaye hata jina humjui.

Sasa hapo ushirikina unaingiaje?
 
Watakuja watu mwaka 2064 hapa kutafuta habari za Magufuli na kuangalia watu walifanya maongezi gani miaka michache baada ya kifo chake.

Kwa niaba yao, nawaomba mziandike, mziandike sana, tena mziandike kwa usahihi.
Zenye makosa zirekebishwe, lakini msikose kuandika. Ikibidi hata makala ndefu za kisomi na vitabu.

Mimi nasikitika habari za mwaka 1984 hatujaziandika vizuri, nikisimulia maisha yalivyokuwa wadogo zangu wengine wanaona kama sinema vile.

Hiyo ilikuwa miaka 40 tu iliyopita.
 
📝🤝🔭🙏
 
Kama anafaa au hafai, ni lazima watu wakumbuke.

Ili, kama anafaa, kwa kadiri anavyofaa, mazuri yake yadumishwe, na kama hafai, kwa kadiri asivyofaa, mabaya yake yaepukwe.

Pinga hoja, usipinge mtu kuzungumziwa. Kama wanachakachua historia, weka sawa. Lakini usiseme kwa nini mnamuongelea Magufuli mtu kashafariki. Mtu akifariki si mwisho wa kuongelewa. Kuna wengine wanaona ndiyo mwanzo wa kuongelewa, kwa sababu kumuongelea mtu maisha yake kabla hajayamaliza anaweza kubadilika, akifariki ndiyo hawezi kubadilika.

Kwa nini unaona watu kukumbusha historia ni jambo baya as long as kinachokumbushwa ni kweli?

Rais Mwinyi ametuachia somo kwamba maisha ya mtu ni hadithi, ishi ili hadithi yako iwe nzuri watu wakihadithia ulivyoishi, usiache aibu.

Sasa watu wakisimulia hadithi za mtu tatizo liko wapi?

Umeshindwa kufikiri kidhahania kwamba hayo mazuri ya huyo mtu yanaweza kuwapa darasa wengine la kuyafuata, au kama mabaya, yanaweza kutoa darasa la kuyaepuka?

Unataka mtu akifa asizungumziwe tena?

Rais aliyeongoza mamilioni ya watu akifa asizungumziwe tena?

Unaelewa kuna simulizi wa Wafalme waliokufa maelfu ya miaka, wa Kirumi, Kiyunani, Mafarao wa Misri, mpaka leo watu wanazisimulia kujifunza kutokana na maisha yao?

Watu wanaandika habari za Caesar, Augustus, Nero, Caligula, Alexander the Great, Darius, Rameses, Ptolemy, Genghis Khan, Napoleon, Washington, Hitler, Martin Luther King Jr., Kennedy.

Mpaka leo.

Wewe unashangaa habari za Magufuli kafariki juzi hapo? Hata watu hawajamuandikia biographies za maana za kuchambua maisha yake.

If anything Tanzania hatujamuongelea vya kutosha Magufuli. Hatujamuongelea kwa kina kuchambua mazuri na mabaya yake, tuepuke mabaya yake yasijirudie na mazuri yake tuyaenzi na kuyaendeleza.
👍👏🤝🙏📝🔊🆒
 
Back
Top Bottom