Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
- Thread starter
- #21
Kakosekana ndiyo maana Kampeni anafanyiwa Magufuli!!??Unatakiwa ufurahie wao kukosa mgombea 2025.
Sasa ukihuzunika, inatupa mashaka wengine.😀
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kakosekana ndiyo maana Kampeni anafanyiwa Magufuli!!??Unatakiwa ufurahie wao kukosa mgombea 2025.
Sasa ukihuzunika, inatupa mashaka wengine.😀
Kwamba Hayati Magufuli anamwagiwa sifa huko mitandaoni. Mie nilikuwa sijui ndo nimesikia toka kwako!Hapo nimetangaza nini...
Halafu naye ameungana nao kumfungulia Uzi kabisa!!!😀Kwamba Hayati Magufuli anamwagiwa sifa huko mitandaoni. Mie nilikuwa sijui ndo nimesikia toka kwako!
Kama anafaa au hafai, ni lazima watu wakumbuke.Bado hujajibu hoja... Kukumbuka yaliyopita hakuwezi kuwa Sawa na Harakati za kuonesha huyu ndiye anafaa.
Hawa watu wasiompenda Magufuli wanaoumizwa anapoongelewa Magufuli mimi nawashangaa sana.Kwa hiyo na wewe umeamua uungane nao kwa kuja kutangaza hapa jukwaani?
Kuna mahali nimesema anamwagiwa sofa...Kwamba Hayati Magufuli anamwagiwa sifa huko mitandaoni. Mie nilikuwa sijui ndo nimesikia toka kwako!
Mkuu,Miafrika pasipo kuipelekesha kama punda kwa mijeledi na fimbo akili hazikai sawa, tunahitaji kama JPM anyooshe hizi ngedere kwa miaka kama 40 hivi.
wewe Inakuuma nini kusifiwa Magufuli basi kufa basi na wewe usifiweBado hujajibu hoja... Kukumbuka yaliyopita hakuwezi kuwa Sawa na Harakati za kuonesha huyu ndiye anafaa.
Tuliosoma falsafa na historia tumekutana na hoja kwamba mtu hafariki mpaka siku mtu wa mwisho anapoacha kumuwaza.
Yani ukimfikiria, ukimkumbuka, ukimtaja, anaendelea kuishi katika mawazo yako.
Labda wanataka Magufuli aendelee kuishi katika mawazo ya watu.
"No one is finally dead until the ripples they cause in the world die away, until the clock wound up winds down, until the wine she made has finished its ferment, until the crop they planted is harvested. The span of someone’s life is only the core of their actual existence."
Terry Pratchett, Reaper Man (Discworld, #11; Death, #2)
Hapana,Falsafa za kishirikina hizi
🤔JPM alikuwa rais bora ndio maana bado anatajwa na wengi, au nasema uongo ndugu yangu.?
📝🤝🔭🙏Watakuja watu mwaka 2064 hapa kutafuta habari za Magufuli na kuangalia watu walifanya maongezi gani miaka michache baada ya kifo chake.
Kwa niaba yao, nawaomba mziandike, mziandike sana, tena mziandike kwa usahihi.
Zenye makosa zirekebishwe, lakini msikose kuandika. Ikibidi hata makala ndefu za kisomi na vitabu.
Mimi nasikitika habari za mwaka 1984 hatujaziandika vizuri, nikisimulia maisha yalivyokuwa wadogo zangu wengine wanaona kama sinema vile.
Hiyo ilikuwa miaka 40 tu iliyopita.
👍👏🤝🙏📝🔊🆒Kama anafaa au hafai, ni lazima watu wakumbuke.
Ili, kama anafaa, kwa kadiri anavyofaa, mazuri yake yadumishwe, na kama hafai, kwa kadiri asivyofaa, mabaya yake yaepukwe.
Pinga hoja, usipinge mtu kuzungumziwa. Kama wanachakachua historia, weka sawa. Lakini usiseme kwa nini mnamuongelea Magufuli mtu kashafariki. Mtu akifariki si mwisho wa kuongelewa. Kuna wengine wanaona ndiyo mwanzo wa kuongelewa, kwa sababu kumuongelea mtu maisha yake kabla hajayamaliza anaweza kubadilika, akifariki ndiyo hawezi kubadilika.
Kwa nini unaona watu kukumbusha historia ni jambo baya as long as kinachokumbushwa ni kweli?
Rais Mwinyi ametuachia somo kwamba maisha ya mtu ni hadithi, ishi ili hadithi yako iwe nzuri watu wakihadithia ulivyoishi, usiache aibu.
Sasa watu wakisimulia hadithi za mtu tatizo liko wapi?
Umeshindwa kufikiri kidhahania kwamba hayo mazuri ya huyo mtu yanaweza kuwapa darasa wengine la kuyafuata, au kama mabaya, yanaweza kutoa darasa la kuyaepuka?
Unataka mtu akifa asizungumziwe tena?
Rais aliyeongoza mamilioni ya watu akifa asizungumziwe tena?
Unaelewa kuna simulizi wa Wafalme waliokufa maelfu ya miaka, wa Kirumi, Kiyunani, Mafarao wa Misri, mpaka leo watu wanazisimulia kujifunza kutokana na maisha yao?
Watu wanaandika habari za Caesar, Augustus, Nero, Caligula, Alexander the Great, Darius, Rameses, Ptolemy, Genghis Khan, Napoleon, Washington, Hitler, Martin Luther King Jr., Kennedy.
Mpaka leo.
Wewe unashangaa habari za Magufuli kafariki juzi hapo? Hata watu hawajamuandikia biographies za maana za kuchambua maisha yake.
If anything Tanzania hatujamuongelea vya kutosha Magufuli. Hatujamuongelea kwa kina kuchambua mazuri na mabaya yake, tuepuke mabaya yake yasijirudie na mazuri yake tuyaenzi na kuyaendeleza.