CCM MP has said that ATCL air hostesses are not attractive

CCM MP has said that ATCL air hostesses are not attractive

Ameongea ukweli tupu hiii ni biashara tuwe wawazi kweli hawana mvuto that's is true.
 
Aulizwe kama mamake mzazi aliyejipatia kazi ya kumlea kama hupo "Attractive" Yaani mtu mzima na akili zake anategemea kuamsha fikra za mahaba na airhostess? Hivi amekosa pesa za kwenda bata oysterbay ale anasa na mabinti wanao fanya hiyo kazi ya uzinzi? Wahudumu ndani ya ndege wapo hapo kupakua matapishi yako ukipata air-sickness, kukuokoa ndege ikianguka ama ikipata hitilafu.. Hawapo hapo kukupea
 
Mbunge wa Kigoma Kusini nchini Tanzania (CCM) Husna Mwilima amesema wahudumu wa ndege wanaoajiriwa na Shirika la Ndege Nchini (ATCL) hawana mvuto kwa wateja.

Mwilima ameyasema hayo leo Alhamisi Novemba 7, 2019 wakati akichangia Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo bungeni jijini Dodoma.

Mwilima amempongeza Rais John Magufuli kwa kutimiza ahadi yake ya kuifufua ATCL na kuwataka mawaziri pia kutimiza ahadi zao.

“Mheshimiwa Waziri mimi nataka nitanie kidogo hizi ndege zetu zinafanya vizuri sana lakini mle ndani hebu tuangalie tunaowaajiri. Wale maair hostess (wahudumu) hata ukimuita mle ndani akigeuka abiria anaona kweli tuna maair hostess mle ndani,” amesema na kuongeza:

“Sijui mnatumia vigezo gani? Unakuta air hostess mfupi, hana mvuto wa kuifanya ndege zetu zionekane. Leo mimi hapa nimezeeka na miaka 50 na ukiniweka…”amesema kabla ya kukatishwa na utaratibu uliombwa na Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Musukuma.

Musukuma amesema huo ni ubaguzi na kwamba kuna wengine wanazaa watoto ambao hawana maumbo kama anayoyasema mbunge huyo.
 
Hivi huwa tunapanda Ndege ili tufike tunapoenda au ili tuwe tunawaangalia na kuwachunguza hao akina dada / mama wahudumu wa ndani ya ndege zetu.

Yaani Mbunge mzima ametafuta kero zote za kimsingi ambazo zina tija kwa wananchi na akaiona hii ya wahudumu wa kike ndani ya ndege?

Kinachonisikitisha zaidi aliyekuja na hoja hii isiyo na mashiko ni Mbunge kutoka chama tawala cha CCM. Na kwakuwa nae ni mwanamama tukichunguza kiundani na kwanini ameamua kuwawakia hawa wahudumu wa kike wa ATCL kuna uwezekano tukaja Kugundua kuwa huenda ana Ugomvi nao wa Kugombea Mwanaume / Mabwana.

Mara nyingi ukiona wanawake hawapendani na wanachukiana jua hapo tatizo kuu ni abwana na hakuna kingine.
 
Napita tu hapa sina komenti.Tunamfundisha Mungu katika uumbaji wake kweli? Wakiajiriwa warembo watadai ni nyumba ndogo zao. Wenye sura kama zangu oooohh hawavutii. Sasa mfanyiwe nini ili mridhike nyie BINADAMU?

Serikali/Shirika haiajiri/haliajiri kwa ubaguzi,bali kinachoangaliwa ni kazi tu. Tunachotaka kazi ifanyike,mengine hayo ya sura na maumbile ni macho ya mtazamaji. Mbele ya Mungu hakuna aliye nzuri au mbaya,ndio maana kila nafsi itaonja mauti au BINADAMU yeyote ameumbwa kwa mavumbi na mavumbini atarudi.

ATCL CHAPENI KAZI,MSISIKILIZE YETU MSIJE KATA TAMAA BURE,HUWA HATUKOSI LA KUSEMA.

TUSIPOTOSHANE, hahahahaha!!

Tusipotoshane
 
Mh. Mbunge yuko sawa kabisa.

Ila wanafiki wa JF wote leo watajifanya kama kilichosemwa ni uongo.
Excellent.

Wanafki watataja Muumbaji sijui what, huu ni ulimwengu wa ushindani, kila kitu kina standards zake.Ndio maana si kila mtu anastahili kuajiriwa hata kama ni msomi.

Air hostess mwingine (juzi tu nilipanda) namwambia nipe WINE tena usiku ananiangalia kwa huruma utadhani zake.

Weka watu wanao meet global standards..angalia Ethiopian Airline, Rwanda , Uganda air etc utaelewa.Nachojua hapa kwetu mule tumeweka binamu zetu kwa kujuana hio ndio inasumbua hata ukitaka kupunguza ajira kisu kinagonga mfupa.
 
Tumetoka kwenye Undugulization saizi tunaelekea kwenye Mvuto.. Vip kuhusu sisi wenye sura za kazi..
 
Back
Top Bottom