Kawe Alumni
JF-Expert Member
- Mar 20, 2019
- 8,685
- 12,000
Mwacheni mama apumzike
alijisahau alijua yupo saloon
alijisahau alijua yupo saloon
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Si watume Application , nisawa unataka ushinde bahati nasibu alafu ujashiliki kwenye bahati nasibuWengi wa hao ma air hostess itakuwa ni wasukuma, maana wasukuma wana masura mabaya na hawana mvuto hata kidogo.
Ebu waende moshi wakachukue warembo kule
Hawa waende kule Karatu wakawachukue warembo, wawapige msasa wa lugha ya malkia. Baada ya miezi mitatu watamudu sana hii biashara.Kampuni ya ndege ( ATCL) imemjibu mbunge wa Kigoma kusini mh Husna aliyewanyanyapaa wahudumu wake kuwa hawana mvuto na ni wafupi.
ATCL wamesema wao hawaajiri wahudumu ili wakaonyeshe sura kama kwenye mashindano ya miss Tanzania.
Maendeleo hayana vyama!
Daah kumbe wa Tanzania tunazitumia ndege zetu, nilifiki azina watejaKuna binti wa ATCL flight moja from Mwanza to Dar tulianza safari saa nane usiku kama sikukosei sababu kulikuwa na distruption kwenye flight schedules zao. nikampatia zawadi ya key holder. Ni mrembo sana, ni mrembo mno yule mtoto wa kike.
Toka siku ile nimekuwa nazunguka kwenye hizo ndege sijawahi muona tena. Kama aliacha kazi namtakia kila la kheri huko aliko kama alihamishiwa ofisini kwa bosi siwezi shangaa lakini cha msingi kama yuko hapa JF hata ani PM tu moyo wangu upate faraja japo kidogo naumia mwenzake.
ANAFIKIRI WANAENDA KUJIUZA EEH APAMBANE TI NA HALI YAKEEMbunge wa Kigoma Kusini nchini Tanzania (CCM) Husna Mwilima amesema wahudumu wa ndege wanaoajiriwa na Shirika la Ndege Nchini (ATCL) hawana mvuto kwa wateja.
Mwilima ameyasema hayo leo Alhamisi Novemba 7, 2019 wakati akichangia Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo bungeni jijini Dodoma.
Mwilima amempongeza Rais John Magufuli kwa kutimiza ahadi yake ya kuifufua ATCL na kuwataka mawaziri pia kutimiza ahadi zao.
“Mheshimiwa waziri mimi nataka nitanie kidogo hizi ndege zetu zinafanya vizuri sana lakini mle ndani hebu tuangalie tunaowaajiri. Wale maair hostess (wahudumu) hata ukimuita mle ndani akigeuka abiria anaona kweli tuna maair hostess mle ndani,” amesema na kuongeza:
“Sijui mnatumia vigezo gani? Unakuta air hostess mfupi, hana mvuto wa kuifanya ndege zetu zionekane. Leo mimi hapa nimezeeka na miaka 50 na ukiniweka…”amesema kabla ya kukatishwa na utaratibu uliombwa na Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Musukuma.
Musukuma amesema huo ni ubaguzi na kwamba kuna wengine wanazaa watoto ambao hawana maumbo kama anayoyasema mbunge huyo.
Akiendelea kuchangia Mwilima amesema sifa ya mhudumu wa ndege ni lazima awe mrefu na amenyooka akiwa mwanaume ama mwanamke na kuomba jambo hilo lizingatiwe.
Chanzo: Mwananchi
ATCL YAJIBU, HATUAJIRI WANAWAKE KUONESHA UZURI
Wakati mbunge wa Kigoma Kusini (CCM), Husna Mwilima akisema wahudumu wa ndege za ATCL hawana mvuto kwa wateja, shirika hilo limesema haliwachagui kwa ajili ya kuonyesha sura.3
“Hatuchagui wanawake kwa ajili ya kuwapeleka kuonyesha uzuri kuna vigezo lazima tuwapime uelewa. Lazima kujua wana uwezo upi wa kufuatilia mafunzo watakayopewa ili watoe huduma inayotakiwa kwa wateja wetu na si sura,” alisema Ladislaus Matindi, mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).
Pia soma
Wale madada wa ATCL ndo dada zetu wa Kitanzania halisi. Mwataka waweje?
Heshima kwenu wakuu, Nmeona watu wakiwazihaki na kuwadharau wafanyakazi wa dreamliner mpya wakisema hawavutii. Wanashindwa kujua kwamba hawa ndo dada zetu, shangazi, mama mdogo na wadogo zetu. Mnawacheka mnatakawa waweje? Hii ndo mbegu ya Kitanzania. Tujivunie. Ningeelewa kama watu...www.jamiiforums.com
2020 Kigoma kusini watamchagua " Tumbili" wa Songwe!Baada ya Kauli ya Mbunge Hasna Mwilima kutaka ATCL kuajiri wanawake warembo na vijana watanashati pekee ni dhahiri sasa jimbo la Mbunge huyu limekuwa na makundi mawili.
1. Kundi la kwanza la wanawake warembo na wenye urefu kiasi flani
2. Kundi la pili la wale wasio na mvuto na wafupi.
Uchaguzi wa mwaka 2020 utaonesha ni akina nani wapo wengi jimboni mwake.je watakuwa warembo ambao wataona amewatetea vyema kabisa katika kipindi hiki.
Ama watakuwa wasio na mvuto ambao hawataona sababu ya kumpigia kura kwa vile ameshawatenga na kuwaona hawastahili kupata kazi?mgawanyiko huu utaleta taswira ya siasa na harakati za Ubunge kwa Mbunge Hansa Mwilima.
Wanatakiwa wawe namvuto ili wateja wakiume waweze kuomba namba za simu, alaf itasaidia wateja wakiume kupenda kutumia ndege zetu wakijua watakitana na madem wazuriKuna mashindano ya umiss kwenye hizo ndege,sijaelewa logic ya urembo kwenye ndege,kwamba wanajiuza kwenye hizo ndege, au wasafiri wanaburudika wanavyowaona,kwamba si wasafi wananuka,sjajua urembo kwenye vyombo vya usafiri kuna umuhimu gani,kwamba usafiri wa ndege ni sehemu ya maonyesho ya Sanaa ya burudani kama ilivyo casino,sijapata logic ya urembo kwenye usafiri wa umma
Ubaguzi unaouona ni huu tu! Ule wa wapinzani wanaofanyiwa kwenye misafara ya Rais kwako ni sawa tu, yule mwananchi aliyeshushuliwa alipotoa ombi la maji! Kisa eti Mbunge wake ni wa Chadema?Wewe nawe bwege tu
1. Tunatafuta mshindi wa urembo safarini?
2. Kunabiashara ya ukahaba ndani ndege?
3. Je hiyo sio fani wanasomea na kufaulu?
4. Watanzania wafupi hawana haki kupata ajira hizo?
5. Watanzania wenye sura mbaya kwa kauli yake Mbunge mpumbavu hawana sifa kuajiliwa iwapo wamefaulu Masomo yao?
6. Je katiba inasemaje ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kuhusu usawa?
7. Kanuni za ccm zinsema vipi kuhusu binadamu na usawa?
Mbwa kama nyinyi enzi za Nyerere ilikuwa nikufukuza kazi na kuwafunga.
Tukianza kubaguwana kwa
-ufupi kawawa na mwinyi hata Mkapa wasingekuwa Marais
-Tukianza kubaguwana kwa sura Remi ongala asingepata wafuasi pande zote za taifa la tanzania
Tunakuwa wapumbavu na wajinga watokufikiri vema ili kutenda mema kwa taifa letu.
Tuache upumbavu
Kwani wabunge wote wa ccm ndio akili zao hizo huaYaani nilishasema wanaume tu ndo wanapendana lakini wanawake tunaoneana wivu wa kijinga sana.
Hii kauli ya Mbunge tena mwanamke kuhusu wafanyakazi wa ndege ATCL kuwa hawana mvuto na wafupi, huu ni wivu wa kuzodoa, kuwakejeli, kuwadhalilisha watoto wa kike wa mwanamke mwenzio au wanawake wenzio.
Wewe Hasna Mwilima, je wewe ni mrembo? Urembo wa mwanamke mwenzie unataka uufanyie nini?
Au unataka hao wanawake waachishwe kazi wakafanye kazi gani? Mpaka hapo umeisha poteza sifa za kuwa Mbunge, umewadhalalisha sana wanawake wa Tanzania.
Natamani niwafahamu watoto wako wa kike, nione urembo walio nao, wanawake tuna mambo ya ajabu sana, ambayo hata shetani ameshindwa kutudefine.
Nilitegemea kauli kama hii ingetolewa na Mbunge viti maalumu, kumbe tena Mbunge mwenye jimbo aliyepigiwa kura na kila aina ya mwanamke, wafupi, warefu, rangi tofauti tofauti, leo unawadhalalisha kiasi hiki.
Ufupi wa mwanamke si ulemavu wa kushindwa kufanya kazi, au hizo ndege ni madanguro? Inabidi tufahamishwe kazi ya ziada wafanyao hao wanawake.
Haya mabunge ya ccm ni gonjwa hatari kwa ustawi wa Taifa, pole kwa wapigakura waliowachaguaNi mbunge wa CCM huyo, kuna mbunge mwingine mwanamke wa CCM alilitaka bunge kuchunguza wabunge wanaume wenye magovi wasiingie bungeni