CCM MP has said that ATCL air hostesses are not attractive

CCM MP has said that ATCL air hostesses are not attractive

Anayesema biashara ni sura za watu basi hata viwandani tuajiri warembo, na wengine waende kulima mashambani maana wataharibu biashara

Mahospitalini tuondowe madakitari na wahudumu wote wanaosemekana na sura mbovu au wafupi waende kulima mashambani

Maofisini tuondowe wote wanaosemekana na sura mbovu au wafupi waende kulima mashambani

Diplomats wetu wote wenye sura mbovu na waliowafupi warudishwe nyumbani waje kulima...maana wanaliwakilisha taifa nje ya nchi hawana mvuto watatufukuzia wafanyabishara nk

Hii ni hoja yakijinga nakipumbavu kabisa
Ubaguzi wa sura
Ubaguzi wa rangi
Ubaguzi wa maumbile nk

Hayati Baba wa taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere alipinga vikali ubaguzi. Sasa tunarudi kulekule.
Mteja haendi kiwandani na haonani na watu wa kiwandani, ila anakutana na watu wa sales/mauzo ambao huwa warembo na watanashati.
 
Kweli Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake.

Taswira ambayo huyo mama anataka ijengeke ni kwamba mwanamke ni chombo cha starehe au kuburudisha kitu ambacho sio sahihi.

Hivi ufupi inakuaje ni kigezo cha kumfanya mtu hafai?hao wahudumu majukumu yao ni zaidi ya urembo maana hata ndege ikipata dharura ni haohao ndio wanahusika na usalama wa abiria,matumizi ya vifaa vya usalama na kuhudumia wagonjwa.

Sasa katika hali kama hizo urembo wake pekee unatusaidia nini?ni lazima vigezo muhimu vizingatiwe.
Ni mchangiaji mmoja amesema eti wanatakiwa wawe warefu ili waweze kuonekana wakiwa wamsimama eti mfupi aweza kukingwa na viti
 
Mteja haendi kiwandani na haonani na watu wa kiwandani, ila anakutana na watu wa sales/mauzo ambao huwa warembo na watanashati.

Umesoma mpaka mwisho?

Jibu kila kipengele ndipo utaipata hoja yangu

1. Viwandani

2. Mahospitalini

3. Maofisini.....watendaji, procurement, sales nk

4. Diplomats (mabalozi, waziri, wawakilishi kimataifa etc)

Then tutaendelea
 
Habarini wanaJF wote,

Ninapenda kuchukuwa fursa hii kulaani kauli iliyotolewa bungeni na Mbunge wa Kigoma Kusini Hasna Mwilima, kauli yake isiyo na staha juu ya dada zetu wanaohudumu katika Shirika la Ndege la Tanzania.

Kauli au hoja yake imeleta madhara makubwa kwa wahudumu hawa pamoja na familia zao.

SABABU ZA KULAANI KAULI YAKE

1. Amewasababishia wahudumu hawa kutokujiamini katika kutimiza majukumu yao, hilo nimelishuhudia jana na leo, wanapotoa matangazo wanakwama kabla hawajamaliza.

2. Wamejaa huzuni usoni japo wanatabasamu kwa kulazimisha.

3. Hawakujipangia kazi wenyewe bali waliomba ajira na wakakidhi kutokana na mahitaji ya mwajiri.

4. Sura, urefu au ufupi ni matokeo ya uumbaji hakuna mwenye uwezo kujifanya atakavyo au jamii.

JE, HOJA ZAKE ZINA MASHIKO?

1. Huenda ni kweli aliyoyasema lakini hoja yake ANGEIVALISHA NGUO isiwaumize au kuwadhalilisha wanawake wenzake.

2. Angeshauri hata kwa maandishi, naamini pia hoja ingefanyiwa kazi.

Nashauri ufike wakati tuheshimiane na kuuheshimu utu wa kila mtu na tukosoane kwa staha.

Mwanamke ni mama
Mwanamke ni dada
Mwanamke ni mpenzi na mke
Tuwaheshimu na waheshimiane.

Hali hii ina madhara. Ninasikitika sana kamera zinawaandama vimwana hawa hadi wanatembea kwa hofu sana...
UKWELI usiovalishwa nguo ni shambulio

Nimetoa la moyoni.
 
Msimlaumu sana huyu mama nadhani yeye amejaribu kuwalinganisha kati ya wale wahudumu wa mshirika mengine mfano Ethiopian ,Rwndan n.k so akaja kutazama na hawa wa kwetu labda akaja kuona kuna utofauti bt cha msingi ni kuangalia kama kuna ukweli basi maboresho yafanyike maana Ile biashara ya ndege warembo wale bright. ni muhimu sana
 
Umesoma mpaka mwisho?

Jibu kila kipengele ndipo utaipata hoja yangu

1. Viwandani

2. Mahospitalini

3. Maofisini.....watendaji, procurement, sales nk

4. Diplomats (mabalozi, waziri, wawakilishi kimataifa etc)

Then tutaendelea
Huko mahospitalini unaenda kwa shida na sio kwa raha, na ndio maana japo sindano inauma bado unaifuata, lakini kwa mtu anaetumia pesa yake na ana luxury ya kuchagua lazima atachagua airline yenye mvuto.
 
Katika kila kipengele ulicho kitaja angalia ni watu gan wana contact na wateja hua wana appearance gan, hata hospitalin mapokezi pale hua kuna wadada mashallah unapona kabla hujatibiwa wakuu
 
Unaelewa kama nibiashara hospitali na watu wanatengeza fedha?
 
Huko mahospitalini unaenda kwa shida na sio kwa raha, na ndio maana japo sindano inauma bado unaifuata, lakini kwa mtu anaetumia pesa yake na ana luxury ya kuchagua lazima atachagua airline yenye mvuto.
Agiza soda mkuu, hawa wanao mkosoa huyo mbunge huenda wana undugu na hao wadada
 
Katika kila kipengele ulicho kitaja angalia ni watu gan wana contact na wateja hua wana appearance gan, hata hospitalin mapokezi pale hua kuna wadada mashallah unapona kabla hujatibiwa wakuu

Wewe naweza kukuita mjinga sababu huelewewi unatetea nini

1. Kwahiyo mhudumu mfupi au mwenye sura isiyo ya mamiss asihudumie wagongwa hatakama the best professional?

2. Dakitari mfupi au ambaye sio mwenye sura za mamiss asipewe Ajira sababu hana mvuto hatakama ni excellent professional

Wewe nimpumbavu
 
Adjustments.JPG
Adjustments.JPG
Adjustments.JPG
Adjustments.JPG

someni vigezo vya kuwa air hostess! Tusibishane kwa emotions bali facts
 
Kwa wadada tu:-

Imagine wewe ni
1. Mfupi.
2. Huna kazi nzuri kivile (so financially hauko poa). 3. Sio mrembo na huna tabia za kujipodoa sana.
4. Huna shepu saaana. Yan wa kawaida tu.

Halafu huyu mama ndo anakuwa MKWEO. Na uliolewa kwa sababu imejulikana mwishon kwmb mwanae kakupiga mimba na tyr unakaribia kujifungua. Na mama alikuw hajui.
 
Haya ndo matatizo ya kauli "mwanamke akiwezeshwa anaweza". Mwanamke mwenye akili ni yule anayepambana kama wanaume wanavyopambana na ukimkuta mwanamke aliyetoboa kwa kupambana na sio kuwezeshwa au kupewa nafasi za upendeleo anakuwa na akili kichwani. Mianamike ya dizaini ya Hasina Mwilima yanatia kinyaa hata tukikutana nayo katika ofisi za umma
 
Huyu mama hata kwenye chama chetu pendwa (ch-p-t-. Fill the missing words)hafai kumtumia halafu anawasema wale warembo[emoji57].
 
Back
Top Bottom