CCM msiompenda Mama Samia, mlitaka nani awe Rais baada ya Hayati Magufuli kufariki?

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,252
Reaction score
8,003
Ninashangaa kuona kuna vikundi vya kijinga ndani ya chama changu cha CCM vinajifanya kua wajuaji sana na kwa wao ndio wanaojua sana nchi kwakua walikua sehemu ya utawala wa awamu ya 5. Vigenge hivi vinajifanya kua active kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali ya awamu ya 6, utafikiri mama hakua sehemu ya utawala wa awamu ya 5.

SWALI LANGU: Kama katiba inasema Rais aliyeko madarakani akifariki basi makamu wa Rais kuapishwa kua Rais kuendeleza gurudumu, hivi baada ya JPM kufariki dunia walitaka nani awe Rais na kwa utaratibu upi? Mnataka kusema kua JPM alikua na makosa kumteua Rais Samia enzi hizo kua Makamu wake mara mbili mfululizo? Hamjui kabisa kua hata Rais Samia ni mteule wa JPM awamu zote mbili mfululizo?

Mnachowewesekea ni nini? Mnataka Mama aendeshe nchi kwa matakwa yenu badala ya katiba na sheria? Kama hamtaki kua waumini wa mifumo yake, kwanini msikae kimya na kama kuna kitu mkamwambie ndani ya vikao vya chama?

Tuache unafki, tumuache Mama aamue kufanya anachoona kinafaa kwa manufaa ya taifa.

#Kazi iendelee!
 
Ninashangaa kuona kuna vikundi vya kijinga ndani ya chama changu cha CCM vinajifanya kua wajuaji sana na kwa wao ndio wanaojua sana nchi kwakua walikua sehemu ya utawala wa awamu ya 5...
Hii ni awamu ya ngapi
 
Kama anakosea asiambiwe yeye mungu
Huu muda kutetea ujinga si mkae naye uko chumbani mwambieni
#kataa Wahuni
 
Nahisi huruma kwa mama maana kuna miradi ela hakuna je mama apate wapi izo ela Basi waseme hadharani wapi wakuzipata ela ili mama hasikope alafu inaamana mama anakosea tu kuliko uongozi uliyopita?
 
Baada Ndugai kuongea upupu wake nimegundua Polepole hayupo pekeake hili ni genge kubwa la kuhakikisha mama 2025 hagombei.. kenge hawa wamwache mama
 
Lakini kwenye hili la deni, Polepole anamsimamo tofauti na Ndugai!
Polepole hapingi kukopa!
Atapingaje wakati Baba yake alikopa zaidi ya Tril. 20 ndani ya miaka 5 tena mikopo ya hovyo ya kibiashara? Huku akiudanganya Umma kuwa tunajenga kwa hela yetu wenyewe, na alikopa kwa siri kubwa?
 
Kwani mkopo sio hela zako mkuu?

Ama mkopo unaulipaje?
 
Mama anajitahidi Sana Sana tena kuliko manyangumi mengi Ndani ya chama ambayo naamini yakipata chance yatatutumbukiza shimoni .miradi Mungu Sana anajitahidi Ila nam dis mambo kadhaa baadhi ni .kuukumbatia mifumo wa awamu ya nne .kuwatoa baadhi ya watumishi , kalemani , kakoko , NK
Kuiinginza Tanesco chaka Kwa kimweka mtu Yule .
 
Ninashangaa kuona kuna vikundi vya kijinga ndani ya chama changu cha CCM vinajifanya kua wajuaji sana na kwa wao ndio wanaojua sana nchi kwakua walikua sehemu ya utawala wa awamu ya 5...
"Mnataka Mama aendeshe nchi kwa matakwa yenu badala ya katiba na sheria?"

Nimecheka Sana; Kwa hiyo anafuata Katiba Na sheria? Kweli Anguko la Ccm limefika.

Huyu Mama yenu mwambieni, amewapa nafasi Chadema ya kuonewa Huruma Na public, hili litamgharimu.
 
Atapingaje wakati Baba yake alikopa zaidi ya Tril. 20 ndani ya miaka 5 tena mikopo ya hovyo ya kibiashara? Huku akiudanganya Umma kuwa tunajenga kwa hela yetu wenyewe, na alikopa kwa siri kubwa?
Hata Ndugai nae alishiriki na kubariki hii mikopo. Tofauti ya Ndugai na Slowslow wamepishana uelewa, mmoja ana cheti cha hospitali njia ya kuelekea by-road Dodoma...
 
Ninashangaa kuona kuna vikundi vya kijinga ndani ya chama changu cha CCM vinajifanya kua wajuaji sana na kwa wao ndio wanaojua sana nchi kwakua walikua sehemu ya utawala wa awamu ya 5...
Naunga mkono hoja.
P
 
Ninashangaa kuona kuna vikundi vya kijinga ndani ya chama changu cha CCM vinajifanya kua wajuaji sana na kwa wao ndio wanaojua sana nchi kwakua walikua sehemu ya utawala wa awamu ya 5. Vigenge hivi vinajifanya kua active kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali ya awamu ya 6, utafikiri mama hakua sehemu ya utawala wa awamu ya 5.

SWALI LANGU: Kama katiba inasema Rais aliyeko madarakani akifariki basi makamu wa Rais kuapishwa kua Rais kuendeleza gurudumu, hivi baada ya JPM kufariki dunia walitaka nani awe Rais na kwa utaratibu upi? Mnataka kusema kua JPM alikua na makosa kumteua Rais Samia enzi hizo kua Makamu wake mara mbili mfululizo? Hamjui kabisa kua hata Rais Samia ni mteule wa JPM awamu zote mbili mfululizo?

Mnachowewesekea ni nini? Mnataka Mama aendeshe nchi kwa matakwa yenu badala ya katiba na sheria? Kama hamtaki kua waumini wa mifumo yake, kwanini msikae kimya na kama kuna kitu mkamwambie ndani ya vikao vya chama?

Tuache unafki, tumuache Mama aamue kufanya anachoona kinafaa kwa manufaa ya taifa.

#Kazi iendelee!
Mmoja atatoboa pipa la mafuta mwingine atachomoa better... Kisha mlipuko utatokea... stay tuned 😉
 
Back
Top Bottom