sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,687
- 1,111
CCM ni chama kikongwe kwa vyama vya ukombozi kusini mwa jangwa la sahara na Afrika kwa ujumla. Kilipaswa kuwa mfano bora kwa vyama vingine vya siasa kutokana na kuishi kwingi na kuona mengi.
Ajabu ndicho chama kinacho ogopa siasa kuliko vyama vyote vya siasa nchini,kwa kulitambua hilo kinaiwekea siasa mizengwe kuzuia wengine wasifanye siasa kupitia serikali yake.
CCM imepoteza ideology yake kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi,kimekuwa chama dola chenye kutegemea msaada wa vyombo vya ulinzi na usalama kuibeba,ndo maana leo viongozi wastaafu wa vyombo hivi vya ulinzi na usalama wanendelea kupewa vyeo ili kudhibiti siasa isifanywe na wanasiasa wa vyama vingi.
Kwa kulitambua hilo na udhaifu wa ukongwe wao wanekuwa mabingwa wa kurekebisha sheria ya uchaguzi na vyama vya siasa kila kukicha kwa lengo la kuficha udhaifu wao.
Leo mahafidhina neno maridhiano ya kisiasa kwao ni msamiati mgumu sana,kwa kuwa unajenga msingi mzuri wa madai ya katiba ya wananchi,ambayo kwao ni kaa la moto lenye viashiria vya kuing'oa CCM madarakani.
CCM ya leo imewekeza kwenye rushwa ya madraka kwa kuwahonga vijana madaraka kama sehemu ya mvuto kwa chama chao,na kuacha legitimacy ya kuwa chamqa cha wakulima na wafanyakazi,uhalali ulioachwa na Mwl kama nguzo ya ushawishi wa siasa za uwazi na ukweli.
Lipo la kujifunza na kukataa hii hali ya kuifanya CCM ndiyo mfumo wa utawala uliosimikwa kimabavu dhidi ya ushindani wa hoja,sera na ukubalikaji wake wa aina ya siasa za ushindani nchi.