Achana na data za kupika tafadhali. Tumia akili. Watu 61m, inawezekana vipi watu wazima wakawa wengi kuliko watoto? Idadi yetu watanzania iko kwa mfumo wa Msonge, watoto wako chini watu wazima wako juu. Sasa unaposema hivi unamaanisha watoto nchi hii ni wachache kuliko watu wazima!
Uchaguzi wa 2020 wanasema wapiga waliandikishwa 29m+, tukasema ni uongo wa wazi, haiwezekani watu wazima kuwa sawa na watoto. Na kama kweli waliandikishwa watu 29m+, maana yake ni kila watu wawili hapa nchini, mtu mmoja alijiandikisha kupiga kura. Je ni kweli kwenye familia yako kama mko 6, watatu walijiandikisha kupiga kura? Huu sio kwamba ni uongo tu, bali ni ujinga wa kitoto.