CCM Na Bunge La Katiba: Mazingaombwe yanayoelekea ukingoni

CCM Na Bunge La Katiba: Mazingaombwe yanayoelekea ukingoni

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Posts
4,850
Reaction score
9,434
SEHEMU YA KWANZA

Hatimaye kiini macho cha muungano kinakaribia kukiumbua chama chetu kikongwe cha CCM. Kwa miaka 50 sasa, ccm iliwafanyia wananchi mchezo wa mazingaombwe and managed to get away with it. Lakini kama ambavyo nimekuwa nikisema over and over again, it reaches a to point when:

Even a magician runs out of tricks

The "trick" nayozungumzia hapa ni suala zima la mfumo wa muungano wa serikali mbili (sera rasmi ya ccm), mfumo ambao umetawaliwa zaidi na kiini macho (illusion) kuliko ukweli au uhalisia wa mambo. Kwa mujibu wa dictionary, an illusion is:

something that deceives by producing a false or misleading impression of reality

Kitendo cha Chama Cha Mapinduzi kudanganya umma kwa miaka karibia 50 kwamba mfumo wa muungano uliopo ni mfumo wa serikali mbili, is deceiving the people kwani for 50 years, the party has been busy producing a false impression before the people that the Government of Tanganyika doesn't exist while in reality, it has been in existence since 1964.

Kada wa CCM na Mwanasiasa Mkongwe kutoka Zanzibar ambae pia historia inamweka kama mmoja wa wajumbe thelathini wa Revolutionary Council (1964), Mzee Hassan Nassor Moyo alinukuliwa na Mwandishi wa Gazeti la ----- toleo la Oktoba 3-9, 2013 akisema maneno yafuatayo:

Tuna serikali ya mapinduzi Zanzibar na serikali ya Tanganyika ambayo ipo katika serikali ya jamhuri ya muungano. Kwahiyo ni serikali tatu tokea huko nyuma. Sasa ukiniambia unataka serikali mbili, nakuachia wewe mwenyewe uendelee na ujinga wako

Huu ndio uhalisia wa mambo, uhalisia ambao viongozi wa CCM wameamua kujitoa mhanga kuugeuza kuwa "kiini macho" (illusion) kwa miaka 50 ya muungano. Tulitarajia viongozi vijana ndani ya ccm kama kina Nape Nnauye ndio wawe mstari wa mbele kukirekebisha chama katika kosa lake hili ambalo kimsingi, huko tuendako ndio litakuwa ni sanda katika jeneza la ccm kama chama tawala nchini Tanzania. Nape Nnauye amefika hapo alipo kutokana na umahiri wake wa kusimamia haki, uwazi, na ukweli lakini kumbe ilikuwa ni danganya toto kwani lilipokuja suala la kusimamia haki ya msingi kabisa ya watanganyika, ikizingatiwa kwamba haki yetu kikatiba imeshaporwa na katiba ya zanzibar (2010), nape na viongozi wenzake ndani ya chama wameshindwa kusimamia haki yetu ya msingi na ya kikatiba. Badala yake, tumemsikia nape na wenzake wakitoa maneno ya kejeli na mara nyingine matusi kwa wananchi (hata wazee wao) wanaotetea haki ya Tanganyika katika muungano wetu.

Kama vile ccm imeshindwa kabisa kusoma alama za nyakati na kuamua kufa na tai yake shingoni, wiki chache kuelekea bunge la Katiba, CCM kupitia Nape ilikuja na tamko la CCM (NEC) ambalo lilisisitiza kwamba chama kinaelekea bungeni kwenda kupigania msimamo na sera yake ya serikali mbili ndani ya muungano. Swali kwamba ccm iliwashirikisha vipi watanzania (let alone wanachama wa ccm) kabla ya kufikia uamuzi mkubwa kama huu, ni swali ambalo limekosa wa kulijibu ipasavyo. Wanaojitahidi kulivaa swali hili huwa wanaishia kuisingizia historia. Wanasahau kwamba historia kamwe haiwezi singiziwa, na hili litazidi kuwa dhahiri huko tuendako.

Baada ya chama kuingia kwenye bunge la katiba na msimamo wake wa serikali mbili licha ya rais kuhimiza vyama kuacha tabia ya kuweka mbele itikadi za vyama na badala yake maslahi ya taifa, zimeenea taarifa kwamba ccm sasa imekuja na waraka wa rasimu ya katiba mbadala, habari ambazo bado hazijakanushwa na ccm hadi sasa. Cha ajabu ni kwamba ndani ya waraka huo, inadaiwa kwamba chama kinapendekeza uwepo wa baraza la wawakilishi la "Tanzania bara" kwa ajili ya kushughulikia masuala ya bara tu. Hii ni ajabu kwani rasimu ya katiba (2013 na hata mkataba wa muungano (1964) hakuna pahala inataja "Tanzania Bara", hivyo kutuacha na swali la msingi kabisa kwamba je, Zanziba iliungana na Tanzania Bara?

Haya ndio mazingaombwe ya ccm ambayo ni dhahiri yanaelekea ukingoni kwani kuna kila dalili sasa kwamba "our great magician is running out of tricks"; swali linalofuatia ni je,

*How many more tricks could CCM have in the hat?
Mzee Mwanakijiji alijadili vizuri suala hili katika mjadala wetu mwingine.

Kilichodhahiri ni kwamba mashabiki wengi sana tayari wameshatoka kwenye ukumbi huu wa mazingaombwe baada ya kuanza kumshtukia mwanamazingaombwe na hata wale ambao bado wapo ndani ya ukumbi, wengi wao hawapo tena kushangilia yanayojitokeza jukwaani bali wanajadili yalio nje ya jukwaa.

Wanachojadili wengi ni jinsi gani ccm baada ya kutambua kwamba umma utaiumbua 2015, imefikia hatua ya kufanya vituko ndani ya bunge la katiba, kinyume kabisa na matarajio ya wengi ambao walitegemea ccm itaenda kutetea sera yake ya muungano wa serikali mbili kwa hoja. Moja ya vituko hivi ni kile cha ccm aidha kwa kujua au kutokujua, kuunga mkono mfumo wa serikali tatu kwa kupendekeza baraza la wawakilishi la Tanzania Bara pekee, lakini hapo hapo chama kikisema kwamba hakita yumba na msimamo wake wa serikali mbili (mfano rejea kauli ya waziri mkuu pinda hivi karibuni). Katika hili, nadhani mzee hassan nassor moyo alilizungumzia vizuri katika mahojiano yake na gazeti la ----- mwaka jana aliposema hivi:

...anayesema hivyo Tanzania bara imeungana na zanzibar huyo inabidi apelekwe hospitali ya wagonjwa wa akili kabisa kabisa. Maana ni kitu cha wazi kinachoonyesha kwaba nchi mbili ndizo zilizofanya jamhuri ya muungano, sasa wewe leo unatuambia Tanzania Bara imeungana na Zanzibar? Ulipata wapi habari hiyo? Wewe si bora tukupeleke hospitali ya Milembe kwa Tanganyika na Kidongo chekunda unguja? Ndio maana yake. Tujue kwamba ni nchi mbili: Tanganyika na zanzibar ndizo ziliungana

Maneno haya ya mzee Moyo yanazidi kuelezea uhalisia wa mambo, kwani iwapo ni kweli wana ccm kwenye bunge la katiba sasa wamefikia hatua ya kupendekeza uwepo wa baraza la wawakilishi la kushughulikia masuala ya "Tanzania Bara", basi kweli kuna haja ya kuwapima akili kwani kwa maana hii, uelewa wao ni kwamba Zanzibar iliungana na Tanzania Bara na sio Tanganyika.

----- pia linamnukuu Mzee Moyo Katika kongamano la kamati ya maridhiano lililofanyika hoteli ya bwawani mwaka jana (2013, akisema:

...sasa kwa utaratibu au kutoa mfano mzuri ni kwamba wewe umekwenda sokoni, umenunua machungwa matatu, moja ukaliweka kwenye mkoba mmoja na mawili ukayatia kwenye mkoba wa pili, utakuwa na machungwa mangapi?

Wajumbe wa kongamano wakajibu "matatuuuuuu!"

Mzee moyo akauliza:

sasa leo tunaambiwa tuna machungwa mawili kisa tu tumetia kwenye mikoba miwili?

Lakini kama tunakumbuka vyema, vituko vya ccm vilivyoashiria kilometa za mwisho za safari ya mazingaombwe vilianzia pale wazanzibari walipofanya mambo makuu mawili muhimu:

1. Kujipatia Katiba yao (2010)inayoitambua Zanzibar kama "moja ya nchi zinazounda JMT". Hii ni tofauti na Katiba yake ya awali ambayo iliitambua zanzibar kama "sehemu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania".
Tume ya katiba chini ya jaji warioba pia inaakisi hili katika utangulizi wa rasimu iliyopo mbele ya wajumbe wa katiba dodoma leo.

2. Serikali ya CCM ilipopeleka muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba kwa wazanzibari, ndugu zetu wazanzibari kama iliyo jadi yao kuipigania Tanganyika kama njia yao ya kufanikisha zanzibar kutambulika kama dola kamili, waliuchana na kuuchoma moto muswada ule kwani ulizuia suala la muungano kuwa sehemu ya mjadala kama vile muungano ni suala ordained from God na sio suala linalojengwa na kulindwa na watu/wananchi. Isingekuwa busara za waziri sitta ambae ndiye aliyeiwakilisha serikali katika halfa ile, pengine leo tungekuwa tunaongea mengine.

Itaendelea...

Cc Nguruvi3, Nape Nnauye JokaKuu Jasusi happyfeet, Bongolander, Mag3 Candid Scope MTAZAMO Kimbunga Mkandara Pasco, Zinedine, Zakumi, gfsonwin Kobello, zumbekuu, Kichuguu JingalaFalsafa ZeMarcopolo Ritz, Mzee Mwanakijiji, zomba MwanaDiwani, EMT, AshaDii, ukwelikitugani, TIMING, na wengine wote niliowasahau;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
SEHEMU YA PILI

Kufuatia hali hii, CCM ikaanza kujikanyaga kwani mazingaombwe yake yalikuwa safirini kuelekea ukingoni. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wajumbe wa tume ya katiba, baadhi ya viongozi waandamizi wa ccm ambao walipendekeza kwa tume juu ya kuendelea kwa mfumo wa serikali mbili walitoa mapendekezo mengine ambayo kimsingi yalihalalisha kurudishwa kwa Tanganyikan lakini pia maoni ambayo yanapelekea kuuvunja muungano (kinyume na hadidu za rejea kwa tume kulinda na kuboresha muungano). Kwa mfano, makada hawa wa CCM walitaka mfumo wa serikali mbili uendelee huku pia wakitaka mabadiliko yafuatayo (mapendekezo yao mbele ya tume ya jaji warioba:

1. Wametaka zanzibar kuwa na kiti chake katika umoja wa mataifa. Mabadiliko haya yanaashiria wazi kwamba kuna haja ya kuirudisha Tanganyika lakini iwapo msimamo wa makada hawa wa ccm ni kutekeleza haya chini ya sera ya serikali mbili, basi ni dhahiri muungano hautadumu.

2.Wametaka zanzibar iwe na benki yake kuu (BOZ), sarafu, jeshi, usalama wa taifa, polisi, na rais wake kutambulika kama amiri jeshi mkuu; mambo haya sio tu kwamba yanaashiria uwepo wa serikali tatu, bali pia kuvunjika kwa muungano iwapo ccm itataka haya yatekelezwe chini ya serikali mbili.

Tunaelekea kwenye hitimisho la mazingaombwe ya ccm na muungano huku wananchi wengi wakiwa na ufahamu kwamba mjadala juu ya muungano uliingizwa kwenye sheria bila ya matakwa ya watawala wa ccm na kama tulivyoona awali, ni wazanzibari ndio walioshinikiza suala la muungano liingizwe kwenye muswada wa sheria lakini sio kabla ya kuuchoma muswada ulioletwa mbele yao na waziri sitta. Muswada ulikuwa unazuia wananchi wasiujadili muungano katika mchakato wa katiba mpya.

Kwa kuruhusu mchakato wa katiba mpya kufuatia shinikizo la upinzani, CCM ilidhania kwamba serikali yake itauteka mchakato wa katiba mpya na bado itaendelea kuwa na legitimacy ya kutawala nchi bila ya wananchi kujali kuipa umuhimu katiba, kama ilivyotokea wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere. Ni muhimu kwa CCM kuelewa kwamba legitimacy ya serikali ya Nyerere, chanzo chake hakikutokana na katiba ya nchi (ile ya 1965 na ile ya 1977). Wananchi wa wakati ule hawakujali suala la katiba, hivyo source ya legitimacy ya serikali ya CCM chini ya Mwalimu ilitokana na vitu vikuu vitatu:

1. Itikadi ya ujamaa chini ya azimio la arusha.
2.Historia ya TANU na harakati zake za mapambano dhidi ya ukoloni, unyonyaji, ubeberu ndani na nje ya mipaka ya nchi.
3.Uwepo wa a popular, charismatic leader - Mwalimu Nyerere.

All the three sources of legitimacy hapo juu hazipo tena kwani:

*CCM yenyewe ilizika kimya kimya azimio la arusha kule zanzibar (1992) bila ya kushirikisha umma (let alone wanachama wa CCM) katika uamuzi huu muhimu.

*CCM sio chama cha kutetea tena wanyonge (wakulima na wafanyakazi) bali sasa ni chama cha tycoons and their inner circles;

*CCM imeishiwa na viongozi wazalendo na wanaoweka mbele maslahi ya taifa.

Haya yote yanadhihirisha suala moja kubwa na la msingi, nalo ni kwamba, iwapo CCM ya leo ingeendelea kuwa na uhalali wa kutawala kwa source of legitimacy other than Katiba kama wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere (rejea hoja yangu hapo juu), basi ccm ingefanikiwa kuendelea na mazingaombwe yake ya serikali mbili ndani ya muungano. Lakini kwa uhalisia wa mambo, ni muhimu CCM ikazinduka na kuacha kujidanganya kwani the only source of legitimacy kwa chama chochote cha siasa kuanzia sasa itakuwa ni "katiba ya nchi ambayo imetokana na wananchi." CCM ikiteleza tu kidogo kwa kudhania kwamba still it will command the legitimacy regardless of the outcome ya katiba mpya, hasa suala la Tanganyika, Katiba Mpya Inaweza Kuiangusha CCM 2015.

Njia pekee ya ccm kuendelea kuwepo katika siasa za ushindani kwa muda mrefu hata kama itatolewa ikulu ni kwa kuheshomu umuhimu wa katiba, kuheshimu matakwa ya umma kuhusiana na nini kiwepo kwenye katiba, lakini muhimu zaidi, iwapo sasa watajitokeza viongozi wakuu wa ccm ambao watakuja na maamuzi na maelekezo kwa wafuasi wao ndani ya bunge la katiba kuhakikisha kwamba katiba ijayo itokane na wananchi huku ccm ikiweka maslahi ya taifa na matakwa ya umma juu ya yale ya chama. Vinginevyo, kuna umuhimu kwa, viongozi wa CCM kukumbuka maneno ya Mwalimu kama alivyonukuliwa na gazeti la Observer la uingereza Aprili 20, 1968:

. Iwapo umma wa zanzibar bila ya ushawishi kutoka nje na kwa sababu zao wenyewe wataona kuwa muungano una hasara kwa uhai wao, sitowapiga mabomu kuwalazimisha. Muungano utakuwa hauna tena sababu ya kuendelea kuwepo iwapo washirika wake wataamua kuukana.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Wakati mwingine nafikiri pengine viongozi wengi na wana CCM wengi waliofanya kazi na Mwalimu Nyerere hawakuwahi kumwelewa kwanini muundo huu sasa aliona ndio utakaozaa Tanzania imara ili wasimamie hoja hizo sasa.

Kwanini CCM wanashindwa kutetea hoja ya serikali mbili hadi watumie viini macho kama anavyoita Mchambuzi katika issues ambazo zinahitaji kujenga hoja tu? Mbona Mwalimu aliweza kuvunja hoja za lile kundi la G55 kwa hoja na kundi kusambaratika bila vitisho wala ujanja ujanja? Lile kundi lilikuwa imara na waliamua kweli kujitosa lakini wakashindwa kupangua hoja makini za Mwalimu na kundi kufa kimya kimya.

CCM waache hizi mbinu zinazoleta dalili za kama wanataka kulazimisha mambo maana wataaibika, Wasisusiane chama bali wajenge hoja ili sisi wananchi tupime pengine wakaungwa mkono na kuheshimika tofauti na huu ujanja ujanja katika zama hizi za utandawazi.

Lakini pia msimamo wa CCM juu ya serikali mbili si dhambi wala uhaini ni kama Chadema wanavyoamini ktk serikali tatu lakini wananchi wasilazimishwe kile hivi vyama vinavyoamini bali wote wajenge hoja mwisho wananchi waamue maana kama ushindani utakuwa ule wa misimamo ya vyama hivi viwili vikubwa tu vipi sisi tunaoamini ktk serikali moja na hakuna taasisi kubwa inayotusemea?
 
yana mwisho .. na tunaomba "kura ya siri-upitishaji katiba " ipite ccm wakose kifaakazi cha kupitisha hoja zisizo na tija kwa taifa.. hasa hii ya ya muundo wa muungano...

binafsi naamini kama wasipo lainika kwenye hii issue wanauvunja muungano kirahisi sana.. bora wakubali serikali tatu udumu hata miaka michache..

muda utaongea tuna Mch. mtikilia na Wazenj hakiharibiki kitu sie wapenda tanganyika
mungu saidia
 
Tatizo la CCM ni kuwa hawajajua Adui yao halisi ni nani ,sasa wanajikuta wakihangaika bila kujua nini target yao , hawajui vita yao mwisho wake ni kitu gani , hawajui watumie mbinu gani kwani hawamjui Adui yao, hawawezi kuandaa silaha za kupambana kwani hawajui ni vita ya misitu ni ama ni ya anga , sasa waandae makombora ya kuvunja madaraja ama mizinga ya kutungua ndege?

Mpaka watakapoweza kuomba insight Adui yao halisi , vita itakuwa imeshafikia ukomo na wao kushindwa , maana Adui yao ni sehemu ya jeshi Lao na amevaa malazi kama yao ........
 
Wakati mwingine nafikiri pengine viongozi wengi na wana CCM wengi waliofanya kazi na Mwalimu Nyerere hakuwahi kumwelewa kwanini muundo huu sasa aliona ndio utakaozaa Tanzania imara ili wasimamie hoja hizo sasa.

Kwanini CCM wanashindwa kutetea hoja ya serikali mbili hadi watumie viini macho kama anavyoita Mchambuzi katika issues ambazo zinahitaji kujenga hoja tu? Mbona Mwalimu aliweza kuvunja hoja za lile kundi la G55 kwa hoja na kundi kusambaratika bila vitisho wala ujanja ujanja? Lile kundi lilikuwa imara na waliamua kweli kujitosa lakini wakashindwa kupangua hoja makini za Mwalimu na kundi kufa kimya kimya.

CCM waache hizi mbinu zinazoleta dalili za kama wanataka kulazimisha mambo maana wataaibika, Wasisusiane chama bali wajenge hoja ili sisi wananchi tupime pengine wakaungwa mkono na kuheshimika tofauti na huu ujanja ujanja katika zama hizi za utandawazi.

Lakini pia msimamo wa CCM juu ya serikali mbili si dhambi wala uhaini ni kama Chadema wanavyoamini ktk serikali tatu lakini wananchi wasilazimishwe kile hivi vyama vinavyoamini bali wote wajenge hoja mwisho wananchi waamue maana kama ushindani utakuwa ule wa misimamo ya vyama hivi viwili vikubwa tu vipi sisi tunaoamini ktk serikali moja na hakuna taasisi kubwa inayotusemea?

Niliwahi kusema mahali. Hoja ya Nyerere dhidi ya G55 ilikuwa kwamba serikali tatu si sera ya CCM na mabadiliko katika sera ya CCM hayawezi kuanzia bungeni. Maana G55 walipeleka hoja yao bungeni - Nyerere akasema hapana. Kwa kuwa wote walikuwa wanachama wa CCM wapeleke hoja hiyo kwenye chama kwanza. Ikikubaliwa sera ya CCM ibadilishwe kisha ndio twende bungeni kama chama.

Safari hii mambo ni tofauti. CCM na unafiki wao wamejikuta pabaya. Hawakuwa na sera ya katiba mpya - wala hakuna kikao chochote halali cha CCM kilichopitisha katiba mpya. Ni utashi wa Kikwete - kwamba nataka katiba mpya na basi iwe hivyo. Katika demokrasia ya kweli walipaswa kumzuia Kikwete na hoja yake ya katiba mpya. Wangemweleza unapotaka kuandika katiba mpya kuna suala la muungano - je uko tayari lijadiliwe kwa uwazi? Sasa wamemwacha na walipofikia ni pagumu kweli. Maana serikali mbili ni kama dini. Ukiulizwa maswali magumu huwezi kujibu. Watanzania wa sasa si wale wa wakati wa Nyerere na kibaya zaidi hakuna Nyerere huko CCM leo - eti wanamtegemea Nape kujenga hoja ya serikali mbili.
 
naam nnasubiri sijalala, vp mjadala huu utazidi kutufumbua macho
 
Kilichokosekana kwenye Muungano wetu huu wa serikali mbili ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyeapa kuilinda na kuitetea KATIBA ya Jamhuri na akafanya hivyo kweli.

Kingine kilichotufikisha hapa ni BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo kwa mujibu wa KATIBA hii ya sasa lingemuwajibisha Rais wa Jamhuri ambaye waziwazi kabisa ameshindwa kuilinda na kuitetea Katiba hii hata baada ya kiapo kizito hadharani, pale uwanja wa Taifa.

Huu haukuwa Muungano wa kiini macho Mchambuzi. Miungano yote DUNIANI inalindwa na KATIBA. Ndio maana wanaochaguliwa au kuteuliwa kwenye nafasi zote kubwa na nzito za KISIASA wanalazimika KUAPA kwa DINI zao kuilinda na kuitetea KATIBA inayoziweka nafasi au vyeo vyao hivo.

Mwaka 1995 Mwalimu aliliongelea sana hili la kuilinda KATIBA pale Kilimanjaro Hotel ya enzi hizo. Hatukumsikiliza. Linatusambaratisha sasa kama NCHI na TAIFA.
 
Last edited by a moderator:
Wakati mwingine nafikiri pengine viongozi wengi na wana CCM wengi waliofanya kazi na Mwalimu Nyerere hakuwahi kumwelewa kwanini muundo huu sasa aliona ndio utakaozaa Tanzania imara ili wasimamie hoja hizo sasa.

Kwanini CCM wanashindwa kutetea hoja ya serikali mbili hadi watumie viini macho kama anavyoita Mchambuzi katika issues ambazo zinahitaji kujenga hoja tu? Mbona Mwalimu aliweza kuvunja hoja za lile kundi la G55 kwa hoja na kundi kusambaratika bila vitisho wala ujanja ujanja? Lile kundi lilikuwa imara na waliamua kweli kujitosa lakini wakashindwa kupangua hoja makini za Mwalimu na kundi kufa kimya kimya.

CCM waache hizi mbinu zinazoleta dalili za kama wanataka kulazimisha mambo maana wataaibika, Wasisusiane chama bali wajenge hoja ili sisi wananchi tupime pengine wakaungwa mkono na kuheshimika tofauti na huu ujanja ujanja katika zama hizi za utandawazi.

Lakini pia msimamo wa CCM juu ya serikali mbili si dhambi wala uhaini ni kama Chadema wanavyoamini ktk serikali tatu lakini wananchi wasilazimishwe kile hivi vyama vinavyoamini bali wote wajenge hoja mwisho wananchi waamue maana kama ushindani utakuwa ule wa misimamo ya vyama hivi viwili vikubwa tu vipi sisi tunaoamini ktk serikali moja na hakuna taasisi kubwa inayotusemea?
Mwalimu alitumia hoja tu kweli kusambaratisha hoja za kundi la G55? Hapana ni nguvu zake ndani ya chama wakati huo, ambako aliomba hoja hiyo ianzie, ndiyo iliyosambaratisha. Unakumbuka ni kutokana na hoja hizo Mh. Malecela alitishiwa na kuelezwa alishindwa kumshauri vyema Rais, matokeo yake ni kitabu maarufu alichokitunga Mwl.
 
Niliwahi kusema mahali. Hoja ya Nyerere dhidi ya G55 ilikuwa kwamba serikali tatu si sera ya CCM na mabadiliko katika sera ya CCM hayawezi kuanzia bungeni. Maana G55 walipeleka hoja yao bungeni - Nyerere akasema hapana. Kwa kuwa wote walikuwa wanachama wa CCM wapeleke hoja hiyo kwenye chama kwanza. Ikikubaliwa sera ya CCM ibadilishwe kisha ndio twende bungeni kama chama.

Safari hii mambo ni tofauti. CCM na unafiki wao wamejikuta pabaya. Hawakuwa na sera ya katiba mpya - wala hakuna kikao chochote halali cha CCM kilichopitisha katiba mpya. Ni utashi wa Kikwete - kwamba nataka katiba mpya na basi iwe hivyo. Katika demokrasia ya kweli walipaswa kumzuia Kikwete na hoja yake ya katiba mpya. Wangemweleza unapotaka kuandika katiba mpya kuna suala la muungano - je uko tayari lijadiliwe kwa uwazi? Sasa wamemwacha na walipofikia ni pagumu kweli. Maana serikali mbili ni kama dini. Ukiulizwa maswali magumu huwezi kujibu. Watanzania wa sasa si wale wa wakati wa Nyerere na kibaya zaidi hakuna Nyerere huko CCM leo - eti wanamtegemea Nape kujenga hoja ya serikali mbili.
Pengine ilikuwa ni njia ya kutatua uvunjivu wa Katiba uliotokana na mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar, zaidi ya utashi wa mtu? Lakini kama unavyosema hail kuwa na mwafaka ndani ya chama kabla!
 
Kwa nini Jakaya alishindwa kumdhibiti Amani Karume kama Mwalimu alivyofanya kwa Aboud Jumbe? Ni Jakaya huyuhuyu na wanamtandao wake ndio waliosaidia Amani Karume kuwa Rais kule Zanzibar!
 
Mkuu Mchambuzi, kwenye huu mjadala wa muungano, mimi niliisha uweka wazi kabisa msimamo wangu hapa
[h=3]Kama Kweli Nia ya Dhati ni Kuimarisha Muungano, Then, "Twende Kwenye Serikali Moja!.[/h]Pasco

mkuu pasco, vipi zanzibar watakubali kupoteza dola yao? Kumbuka wanataka mamlaka kamili, ikipita serikali moja ndoto za wazanzibar kutaka mamlaka kamili zitakuwa zimekufa. Kwao bora serikali 3 au 2. Ila kiukweli serikali 1 ndio suluhisho japo kwa hali halisi ya wazanzibar haiwezekani. Option ya 2 ni serikali 3/shirikisho japo huku sina imani nako.
 
Tunapozungumzia serikali moja, tunazungumzia nchi moja, hivyo hapo kutakuwa hakuna tena, mtu anayeitwa Mzanzibari, hapo wote ni Watanzania, tukifika huko, ni wengi wape!, hata kama Wanzibari wote hawataki serikali moja, wabara wote tukitaka serikali moja, na kama tuko wengi, then ni serikali moja Wazanzibari watake wasitake!.
Pasco.
 
Kaka umefanya analysis iliyoshiba na somo kwa vilaza kama kina Nape et al. Nimekuwa najiuliza sana hofi hii ya CCM mpaka wanajitoa ufahamu wa uhalisia wa mambo ya msingi yatakayojenga na kuimarisha muungano uliopo. Nimependa sana Uchambuz wako na umeweka bayana mambo mengi ambapo kila mwenye akili timamu atautafakari na kuona uhalisia wa mambo katika mchakato huu kuelekea katiba mpya.

CCM wamekuwa kama dragon fly kwa sasa hawana mwelekeo unaoeleweka kwani wanashindwa kutoa elimu na hoja zenye mashiko while wakipinga bila kutoa logical solution ambay inacome up na solution ya matatizo yalokuwepo ktk muungano na mfumo wa serikali. Ninachoweza kusema ni kwamba, CCM imekosa viongozi imara na hawana heshima yoyote kwa jamii kwa kuwa wana rangi nyingi za kuimitate mambo angali hawana uwezo.

Hamna msemaji, kila mmoja ni msemaji, hamna nidham kila mmoja anaibuka kila kona akisema la kwake kuhusu chama kitu ambacho hakikuwepo kabisa kipindi cha nyumba wakati wa uhai wa mwalimu Nyerere. Ni nani anayeweza kusimama kama nyerere na akatoa somo na kujenga nidham kama nyerere kwa ccm kwa sasa? hakuna hakuna.Mwenyekite mwenyewe ni porojo tu, Mwenezi mipasho huku makatibu wakiwa kama wamepigwa ganzi. Kila mwenye nguvu yake ya kifedha anaendesha chama awezavyo. Ni lazma wajitazame upya na wakubaliane na mabadiliko la sivyo hiki sio chama zaidi ya genge linalojilindia maslahi yake yenyewe kwa kuwa kwa kuua na kukatili raiya ili mambo yake yaende ndo jadi.

Mungu anawaumbua na tunamshukuru sana M/Kiti wa mda kwa kuanza kuonesha matumaini na tungependa Sita Samwel awe ndo Mshindi ili asimamie viwango na Tanzanyika yetu iwe Huru. Mungu Ibariki Tanganyika, Mungu Ibariki Zanziba na Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
 
Tunapozungumzia serikali moja, tunazungumzia nchi moja, hivyo hapo kutakuwa hakuna tena, mtu anayeitwa Mzanzibari, hapo wote ni Watanzania, tukifika huko, ni wengi wape!, hata kama Wanzibari wote hawataki serikali moja, wabara wote tukitaka serikali moja, na kama tuko wengi, then ni serikali moja Wazanzibari watake wasitake!.
Pasco.

Eti 'wazanzibar watake wasitake' ni chuki au udikteta?hivi hujui kuwa hizi ni nchi 2 huru?muungano ni jambo la hiari na kama munalazima na muungano basi nchi zipo nyingi za kuungana sio lazima iwe zanzibar,zanzibar kwanza.
 
Mkuu Bobwe, call it what you may, chuki, udikiteta, au jina lolote,
Muungano utadumu!. Wale mnaodhani tofauti, mtaishia kujifia na vijiba vyenu vya roho!.
Pasco
 
Kwa nchi masikini hii tunahitaji serikali moja. Ila kwasababu hakuna anayetaka kutatua tatizo serikali tatu ni njia ya kwenda solo gov.

Malalamiko ya Wazanzibar yananifanye nikumbuke ukoloni. Kama wazanzibar wanajiona hawako huru, wanaminywa, na wapo kwenye muungano kikoloni inabidi wapewe uhuru wao.

Muungano wa nchi mbili huwa unadumu kama pande zote mbili zinaridhiana na kukubali kuungana yaani watu, mali, ajira, ndoa, nk na kuwa nchi moja na serikali moja. Nchi nyingi zilizoungana ama kwa hiari ama kwa nguvu zilijitajihidi sana kumaliza utengano na kutengeneza serikali moja, amiri jeshi mmoja, dola moja ndio zilizodumu kwenye muungano.

Muungano wa kutengeneza madaraka hautamaliza kasheshe. Kinacholiliwa sasa ni muundo wa kugawana keki kwa kupeana madaraka na kumaliza kodi zetu kwa vyeo vya ajabu ajabu.
 
Back
Top Bottom