CCM Na Bunge La Katiba: Mazingaombwe yanayoelekea ukingoni

CCM Na Bunge La Katiba: Mazingaombwe yanayoelekea ukingoni

"Labda ni vizuri kukumbuka kwamba shabaha ya baadhi yetu ilikuwa ni kuziunganisha nchi za Afrika Mashariki ziwe Nchi Moja. Na wakati Zanzibar na Tanganyika zinaungana, Kenya, Uganda na Tanganyika zilikuwa katika mazungumzo ya kutafuta uwezekano wa kuungana. Kama jambo hilo lingetokea, nina hakika kabisa kwamba mfumo wa nchi mpya ambayo ingezaliwa ungekuwa ni wa Shirikisho: ama Shirikisho la Nchi Tatu zenye Serikali Nne, au Shirikisho la Nchi Nne zenye Serikali Tano. Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali mbili, ya Tanzania na Zanzibar. Wapendao Utanganyika watakuwa wazalendo zaidi, badala ya kuwa wasaliti, wakiazimia Afrika ya Mashariki iliyoungana kuwa Nchi Moja, kuliko Tanzania iliyotengana ikawa nchi mbili" - Julius K. Nyerere's (1995: 16-17) Uongozi Wetu Na Hatima ya Tanzania.
 
Niliuliza mwanzoni:
Sera hii ni ya nani?
Serikali kuwa tatu
Hapa Tanzania kwetu?


...


Ye yote mwenye akili
Asiyekuwa jahili,
Sera hii anajua
Itavunja Tanzania.


Wanajua wanavunja,
Na kusema kwa ujanja
Tanganyika kujitenga
Si kuvunja, ni kujenga.


Ati "ndani ya Muungano",
Tudhanie ni maneno
Ya uwezo wa hirizi
Kukinga maangamizi.


Misingi mkishavunja,
Msidhani kwa ujanja
Nyumba mtashikilia,
Ikose kuwafukia.


Kwanza fikiri gharama
Zitobebwa na kauma:
Hizi serikali mbili
Sasa twaona thakili,
Sembuse zikiwa tatu?
Wataweza watu wetu?


...


Nakiri Wazanzibari
Katiba waliathiri,
Nilidhani kazi yetu
Ni kuwabana wenzetu,
Viongozi wa Zanziba,
Waiheshimu Katiba.


Lakini ni Serikali
Ambayo haikujali,
Na kitendo kama hicho
Ikakifumbia jicho,
Na kuanza kufokea
Wale waloikemea.


Wala kuvunja Katiba
Kuvunja Nchi si tiba.


Hivi wakifanikiwa
Na nchi wakaigawa,
Kumbe hawataandika
Katiba ya Tanganyika?


Wataacha utawala
Uwe shaghalabaghala?
Na kama ikiandikwa,
Katu haitakiukwa?


Endapo itatukia
Nayo ikavunjwa pia,
Tanganyika itengane,
Wapate nchi nyingine?


Wanaovunja sharia
Na Katiba Tanzania
Dawa ni kuwashitaki
Waadhibiwe kwa haki:
Nchi yetu kuigawa
Ni uhaini, si dawa.


...


Tanzania yetu ina
Watu aina aina:
Inao hao Wapemba
Watachomewa majumba,
Sera hii ikipita
Bila ya kupigwa vita.


Lakini ina Wahaya,
Na Wasumbwa na Wakwaya,
Ina Waha na Wamwera,
Na Wakwavi, na Wakara.


Ina Anna ina Juma,
Ina Asha ina Toma,
Kadhaka ina Pateli,
Na wengine mbali mbali.


Uhasama ukipamba
Mkafukuza Wapemba,
Anojua ni Manani
Mbele kuna mwisho gani.


Hivi mnavyofikiri,
Wenzetu Wazanzibari
Walitokea mwezini
Kuja hapo visiwani?


Visiwani humo humo
Wamakonde, Wazaramo,
Wanyamwezi na Wamwera;
Na mbari nyingi za Bara.


Walotoka Arabuni
Waliondoka zamani,
Walobaki ni wenzetu,
Raia wa Nchi yetu.


Mzaramo wa Unguja
Akizuiliwa kuja
Kuishi Darisalama,
Nambieni Msukuma
Mgogo au Mngoni
Aruhusiwe kwa nini.


Na Mchagga watamwacha?
Na Muha na kina Chacha?


Mwajuma wa Zanzibari
Mkimwona ni hatari,
Hivi Juma wa Pangani
Ana uhalali gani?


Na Shabani wa Kigoma?
Na Fatuma wa Musoma?


Na vita vya uhasama
Vitapamba nchi nzima:
Hawa fukuza hawa
Kwa udini na uzawa,
Yalo Yugoslavia
Yatufike Tanzania.


Chuki hizi msidhani
Hazina udini ndani,
Maana behewa hili
Lina watu wa kila hali.


Wamo na maaskofu,
Na mashehe watukufu:
Na wasomi wa sharia,
na wachumi wetu pia,
Kila mtu ana lwake,
Anazo sababu zake.


...


Hizi pilika pilika
Za kutenga Tanganyika
Ni kutafuta nafasi
Za kupata Uraisi


...


Tanganyika mnadhani
Ina mvutano gani
Wenye nguvu kuzidia
Umoja wa Tanzania?


Wa Pwani na wa Unguja
Mkiona si wamoja,
Mtawaona wa Mtwara
Ni wamoja na wa Mara?


Wa Pemba mkiwatenga
Na ndugu zao wa Tanga,
Mtaacha wa Tabora
Wadumu na wa Kagera?


Wafipa wa Sumbawanga,
Na Wasegeju wa Tanga,
Wawatenge Waunguja,
Wao wabaki wamoja?


Hivi Waha wa Kigoma
Na Wakurya wa Musoma
Na Wazaramo wa Pwani
Watabaki majirani?


Msidhani Tanzania
Si sawa na Somalia,
Ati mtaitabanga,
Msihiliki kwa janga.


...


Kikao mchanganyiko
Cha Dodoma huko huko,
Kimesema wazi wazi
Kuwambia Viongozi:


"Serikali kuwa mbili
Si sera ya Serikali,
Bali ni sera ya Chama
Kile kilichowatuma.


Basi kairudisheni
Kwa wenyewe vikaoni,
Wapate kuijadili,
Kibidi waibadili."


Mimi kwa upande wangu
Nawanasihi wenzangu,
Sera wakiibadili,
Tafadhali, tafadhali:
Chama na kilete hoja
Serikali iwe moja

...

Nasi twaiga Warusi
Hata katika maasi,
Tuivunje vunje Dola,
Turudie makabila?

...

Mbegu mbaya imepandwa,
Lakini hatujashindwa,
Tunaweza kuing'oa,
Na nchi kuikoa.

Akipendezwa Jalia,
Itadumu Tanzania,
Amina! tena Amina!
Amina tena na tena!

Julius K. Nyerere, 16.11.1993 (TPH)


​
 
Mkuu Bobwe, call it what you may, chuki, udikiteta, au jina lolote,
Muungano utadumu!. Wale mnaodhani tofauti, mtaishia kujifia na vijiba vyenu vya roho!.
Pasco

Umebaki mtanganyika peke yako ambae huitaki tanganyika yako,unashangaza walimwengu,zanzibr kwanza.
 
  • Thanks
Reactions: prs
Mabandiko #1 na #2 hapo juu yalilenga kuelezea jinsi gani CCM ina wakati mgumu wa kuendelea na mfumo kiini macho wa muungano. Hii ni kutokana na chama hiki kikongwe kuzidi kupoteza its original sources of legitimacy kama nilivyojadili (azimio la arusha, historia ya TANU ya kupigania wanyonge ndani na nje ya nchi na uwepo wa kiongozi muadilifu, mzalendo na charismatic - Julius Nyerere). Kama tulivyokwisha ona, ni haya mambo matatu ndio yaliyoipa ccm na serikali yake legitimacy ya kutawala nchi, kwani legitimacy ya ccm haikutokana na katiba ya JMT (1977), katiba ambayo ingawa umma haukushirikishwa katika uundaji wake, umma haukujali sana juu ya suala hili kwani kwa mtazamo wa wengi, uongozi chini ya Nyerere ulizaa taifa lenye self determination, vision na liliweka wananchi at the centre (badala ya kuwaacha in the periphery kama ilivyo sasa). Lakini pamoja na mafanikio ya ccm chini ya mwalimu kupata legitimacy ya kutawala kupitia vyanzo tajwa vitatu hapo juu, mgogoro juu uhalali wa utawala wa serikali ya ccm "kikatiba" ukawa ni "a time bomb", hasa kutokana na changamoto za kiuchumi zilizoikumba nchi kuanzia miaka ya mwisho ya sabini, wakati nchi ilipochagua to pursue a "developmental state" approach.

Katika kipindi kilichofuatia, upepo wa mageuzi ya kisiasa na kiuchumi ulianza kuiandama ccm na serikali yake, lakini again, kutokana na ukweli kwamba legitimacy ya serikali ya Nyerere haikutokana na katiba bali masuala niliyojadili hapo juu, CCM iliweza kuendelea to manage mageuzi ya kisiasa in a "top down" fashion bila ya umma kuwa na tatizo kwani imani kwa ccm ilikuwa bado ni kubwa sana kwenye umma. Hata hivyo mageuzi ya kiuchumi yalikuwa ni magumu kuyazuia hasa ikizingatiwa kwamba moja ya masharti ya kuendelea kusaidiwa na wahisani ilikuwa ni kulegeza masharti ya kiuchumi.

Nikirudi kwenye suala la mageuzi ya kisiasa ambayo ccm ilifanikiwa kwa muda mrefu kuyaongoza in a top down fashion tofauti na nchi nyingi za kikomunisti na kjamaa wakati ule (mfano zambia na former soviet satalites), mkakati wa CCM wa kuhakikisha kwamba ratiba ya uchaguzi mkuu haibadiliki (kila baada ya miaka mitano) inaendelea ndani ya mfumo wa vyama vingi ni mkakati ambao ulikisaidia sana ccm, suala ambalo wengi bado wana overlook. Tofauti na Tanzania, nchi nyingine nyingi vyama tawala vilianguka kwa sababu mageuzi ya kisiasa yaliendana na chaguzi kuu ndani ya kipindi kifupi sana. Mkakati mwingine ulioisaidia ccm ni kufanya maamuzi ya kuruhusu vyama vingi licha ya wananchi walio wengi (80pct) kupendekeza mfumo wa chama kimoja uendelee. Lakini kuna suala moja muhimu ambalo makada wengi wa ccm aidha kwa makusudi au bahati mbaya wanalificha pale wanapojenga hoja kwamba ccm ingeweza kuzuia mfumo wa vyama vingi kwani umma ulivikataa. Suala ambalo halisemwi ni kwamba pamoja na tume ya tume ya nyalali kuja na maoni kwamba 80% ya wananchi walipendelea mfumo wa chama kimoja uendelee, takwimu nyingine muhimu katika ripoti ya nyalali haisemwi, nayo ni kwamba karibia 60% ya wananchi walitaka very radical democratic reforms ziwe implemented ndani ya mfumo wa chama kimoja. Ikaja kuwa dhahiri kwamba jambo hili lisingeweza tekelezeka bila kuruhusu vyama vingi kwani soon or later, umma ungeichoka ccm, tena kwa kasi kubwa sana. Matokeo yake ikawa ni kuruhusu mfumo wa vyama vingi but again in a very calculated strategy kama nilivyojadili awali.

Tulipofikia ni hatua muhimu sana kwetu kama taifa kwani katiba ya JMT ya 1977 imejengwa juu ya nguzo kuu mbili:

*Mfumo wa chama kimoja cha siasa.
*Mfumo wa serikali mbili wa muungano.

Bila ya haya mawili kufanyiwa kazi na bunge la katiba, kazi ya tume ya warioba na ya bunge la katiba itakuwa ni karibia na sifuri. Wapo watakaojenga hoja kwamba taifa sasa lipo chini ya multipartism kwahiyo nguzo ya kwanza ya katiba ya 1977 ilishaondolewa kufuatia ujio ya vyama vingi. Lakini upande huu wa hoja unasahau suala moja muhimu, nalo ni kwamba "multipartism and democracy" ni vitu viwili tofauti kwani unaweza kuwa na multipartism lakini usiwe na liberal democracy. Tutajadili hili kwa undani baadae.

Imefikia wakati sasa kwa wale wote wenye mapenzi na Tanganyika yao kuanza kujipanga kimkakati juu ya jinsi gani ya kuidai Tanganyika yao kwa hoja. Kazi hii itafanikiwa tu iwapo tutakuwa na uelewa wa jinsi gani "tuliipoteza Tanganyika", hivyo kuwa na nafasi nzuri ya kujua jinsi gani "tutaipata tanganyika". Katika mjadala wangu unaofuatia, nitajikita katika hili la kuelezea kwa kirefu jinsi gani Tanganyika yetu ilitutoka.





Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu Bobwe, call it what you may, chuki, udikiteta, au jina lolote,
Muungano utadumu!. Wale mnaodhani tofauti, mtaishia kujifia na vijiba vyenu vya roho!.
Pasco

Pasco urusi ilisambaratika tukiona, umeongea maneno yaliyo chini ya kiwango kuwahi kukusoma.

huu ni uchochezi clasified. hamkawii kufa kwa mashinikizo ya damu mambo yakienda tofauti na imla yenu.

eti muungano utadumu!! haya ni maajabu ya chura kupaka poda.
 
Last edited by a moderator:
1. Wametaka zanzibar kuwa na kiti chake katika umoja wa mataifa. Mabadiliko haya yanaashiria wazi kwamba kuna haja ya kuirudisha Tanganyika lakini iwapo msimamo wa makada hawa wa ccm ni kutekeleza haya chini ya sera ya serikali mbili, basi ni dhahiri muungano hautadumu.

2.Wametaka zanzibar iwe na benki yake kuu (BOZ), sarafu, jeshi, usalama wa taifa, polisi, na rais wake kutambulika kama amiri jeshi mkuu; mambo haya sio tu kwamba yanaashiria uwepo wa serikali tatu, bali pia kuvunjika kwa muungano iwapo ccm itataka haya yatekelezwe chini ya serikali mbili.

Mchambuzi umechambua vizuri sana. Kila mara kwenye jamvi hili huwa nasema CCM ya sasa si CCM ya Nyerere, CCM ya sasa ya Zanzibar ni dhaofu sana ikilinagnishwa na ile ya Mzee Karume.

Sio upande wa bara na sio upande wa visiwani, hakuna aliyeweza kusimama kidete kueleza sababu za kweli au sababu za msingi za kuendelea na muungano na kuumimarisha, au kuuvinja. Ukiangalia maneno ya wengi wao unaweza kuona ni porojo za kisiasa ambazo hazioneshi hasa ni nini CCM inataka na nini haitataki na kwanini. Ninachoona sasa ni kuwa CUF na Seif Sharif Hamad wameweza kufanya kazi ya ajenda setting, and now we are thinking in a way that CUF/Maalim Seif wants us to think.

I think it is only Seif Sharif Hamad who is very clear on what he wants, very clear on how he will get what he wants, and very determined to get what he wants. I have not seen or heard from any personality within CCM, with equal honesty and determination, whether for or against Union. Those who talk about Union, whether for or against, do not talk with any enthusiasm, and the matter of union does not seem to be a priority than 2015 is. Matokeo yake ni kuwa tuna hatari ya kupata katiba "mpya" ambayo tutaanza kuiwekea viraka mwaka 2016.

Matatu uliyoyataja ni kweli yameezua legitimacy ya CCM. Ni vizuri wewe unasema wazi ukweli huu kuwa CCM kwa sasa haina legitimacy miongoni mwa watanzania, kote bara na visiwani. Ni chama tofauti kabisa lakini kinaendelea na jina la CCM, kimesahau kinasimamia nini, kisimamie vipi na kwa ajili ya nani. ndio maana hata watu kinaowaongoza wameonesha kuwa na mawazo tofauti kabisa na yale ya Chama.

Kama unakumbuka kila mara nasema kuwa serikali tatu ni kuvunja muungano. So called mapendekezo ya CCM Zanzibar ya kiti UN, BOZ, jeshi na usalama na mengine uliyotaja ni wazi kabisa kuwa ni mwelekeo wa kistaarabu wa kuvunja muungano. .......if that is where CCM is leading us (contrary to what she stands for), there is no need to wait for long to do it, better we do it now. Mkuu Nguruvi3 has been very candid about it he says he does not see any light ahead, so tuvunje jahazi na kila mtu achukue mbazo zake. There is no need for laying down a foundation of breaking the union in the future, and get involved in another political wrangling in the future. If mapendekezo yao is what is in their mind, best way is to break the union now.

Kwa hiyo tunaona wazi kuwa serikali mbili as they are now, hazikubaliki na wabara wameanza kuwa na sauti nyingi za kutokukubali pia. Serikali mbili kwa mtiondo huo wanaousema CCM kwa sasa ni mbaya kuliko ule wa sasa. Serikali 3 mazingaombwe yake hayatakuwa tofauti na yale ya serikali mbili inazopendekeza CCM. Kwa hiyo ili muungano uwe muungano, ni lazima tuwe na serikali moja, au tufuate njia ya mkuu Nguruvi3.


Cc Nguruvi3, Nape Nnauye JokaKuu Jasusi happyfeet, barubaru, Mag3 Candid Scope MTAZAMO Kimbunga Mkandara Pasco,Zinedine, Zakumi, gfsonwin Kobello, Kichuguu JingalaFalsafa ZeMarcopolo Ritz, Mzee Mwanakijiji, zombaMwanaDiwani, EMT, AshaDii, ukwelikitugani, TIMING
 
utamu hapa ni kwamba CDM itapanda chat haraka sana Zenj na wazenj na watanganyika watakuw akitu kimoja dhidi ya CCM .wenyewe watanyong`onyea ktk fao la kujitoa
 
Jamhuri ya kiislam ya watu wa Zanzibar then mafuta tele kama Qatar with American military base... hakuna kuvunja muungano ingawaje for a very selfish reason,ile coast imejaa oil kuliko Saudi Arabia
 
Kabla sijachangia mada ya Mchambuzi, nionglee kidogo kuhusu bandiko #26 la Mkuu Bongolander

1. Amemuongelea Maalim Seif kama mtu anayejua anataka nini na kwanini.
Kwa mtazamo wangu Maalim Seif amewachangaya wznz na sasa hawajui wanataka nini.

i) Ni Katibu mkuu wa CUF yenye sera za serikali 3 anazosimamia.
ii) Akiwa na Uamsho Maalim anataka muungano uvunjwe
iii) Akiwa na wana maridhiano, maalim anataka muungano wa mkataba.

2. Bongolander ameongelea legitimacy ya CCM na umahiri katika kutatua matatizo.
Nakubaliana naye kabisa kuwa CCM ya leo siyo ile waijuayo watu.

i) Zanzibar ilipovunja katiba ya JMT na kuifanya katiba ya SMZ kuwa juu ya JMT, CCM hawakusema lolote. Huu ulikuwa ndio mwanzo wa matatizo ingawa yalikuwepo.

ii)CCM haina uthubutu wa kukabiliana na wanaopinga sera zake. Inakabiliana na akina Mansour Himid na kuwaacha akina Nasor Moyo kwasababu haina uthibiti na udhibiti wa CCM ya 1977

iii) CCM ya akina Nape haijui sera za chama wala ushirikishaji wa wanachama.

Hapa ndipo narudi kwa Mchambuzi
i) Sera ya CCM katika uchaguzi ilikuwa serikali 2
ii) Aliyekiuka serikali 2 ni CCM nambari one JM Kikwete
iii) Nguvu ya wananchi ilimlazimu atangaze mchakato kwa hoja ya wananchi na siyo CCM
iv) Akina Nape walishirikishwa hoja ikiwa ya wananchi na wala hakuna kikao chochote kilichomuagiza mwenyekiti kuanzisha mchakato.

Ni nguvu ya wananchi na hadi sasa ni nguvu ya wananchi iliyopo mbele.
Hakuna kikao zaidi ya NEC kilichowashirikisha wana CCM kuamua mustakabali wa taifa kwa mtazamo wa ki CCM.

Ni maamuzi ya akina Nape ambayo hayatokani na chama wala kushirikishwa na mwenyekiti bali kudandia train kwa mbele. Ndio maana baadhi ya wabunge na wana CCM hawakubaliani na mawazo ya akina Nape. Wanachokifanya ni kuwatisha na si kuwashawishi kwavile Nape na wenzake wachache hawana mandate ya wana CCM na wala hawakuwa sehemu ya mwanzo wa wazo la mchakato.


iv) Kutokana na kutokuwa na baraka za CCM hata mwenyekiti hakuwahi kuwauliza CCM kama wanataka muungano au la.

v)Tume zaidi ya 5 zimeundwa kushughulikia suala la muungano.
Ni Nyalali, Kisanga, Amina Salum na ya Warioba kwa ujumla.

Zote zimefanya kazi chini ya CCM zikishirikisha makada wa CCM. Tume zote zimekataa serikali 2 na kupendekeza 3 kama njia ya kunusuru muungano ambao ki uhalisia haupo baada ya znz 2010.


vi) Miaka 50 CCM imeshindwa kutatua kero. Nauliza swali hili mara ya 17, ni kwanini tudhani sasa wana Mworabani wa tatizo hilo.

vii) Mwarobani waliokuja nao kwa waraka ni kuwa na serikali 2, ya Muungano na SMZ.
Wanashauri uwepo wa baraza la wawakilishi la Tanganyika.
Na mambo yasiyo ya muungano ambayo hawakuyataja yasisimaiwe na wazanzibar.
Hadi hapo wanakubaliana na mapendekezo ya serikali 3 ya tume ya Warioba.


viii)Tofauti na tume ya Warioba, wao wanataka Rais wa Muungano atakayekuwa na nguvu hadi Zanzibar kwasababu za kisiasa na si kijamii au kiuchumi.

ix) Akina Nape na Andrea Chenge hawaelezi kwanini wamekuja na waraka na si miaka 50 iliypita. Hawaelezi tatizo la serikali 3 ni lipi kama wanachopendekeza ni sawa na wanachosema Tume ya Warioba.
Ile hoja ya gharama imeishia wapi? Je waraka wao utakuwa umepunguza gharama kwa kiasi gani.


x) Waraka wa CCM unasema kutakuwa na Tanzania bara, swali wasilolijibu akina Nape na Chenge ni je iwapi serikali ya Tanzania visiwani?

Endapo tuna SMZ bila tatizo, kwanini litokee tatizo serikali ya Tanganyika ikiwepo? Na kwanini muungano uwepo kwa kuipoteza Tanganyika. Wznz wana kitu gani ambacho Tanganyika inawalazimu kupoteza nchi yao ili kukidhi haja za znz

Na je SMZ imeungana na nani ili kupata Tanzania? na nchi ya Tanzania bara imeanza lini kulingana na historia ya nchi yetu.

3. Kwa vile CCM haikuweza kuwashawashi wananchi kuwa na serikali 1 katika miaka 50, na kwavile CCM haiamini tena uwepo wa serikali 2 kwa waraka wao, kwanini kusiwe na machaguo mawili muhimu yaliyobaki?

1. Uwepo wa serikali 3 ili kunusuru hata hayo mambo 5 yaliyobaki kama muungano
2. Kukubaliana muda umefika, ni wakati wa kuvunja jahazi tugawane mbao kwa amanai na salama.
 
Mkuu Mchambuzi

Be careful na huo msemo wako wa magician, pengine magician hapa ni mnao lilia serikali tatu na wendawazimu kama kina sharif hamad (ambao wameanza kuona kwenye mwanga kunanini kuliko kelele zao za gizani, kama kauli yake iliyoletwa humu ya serikali mbili inaukweli wowote).

CCM aiwezi kukosa tricks kwasababu inataka serikali mbili, what you need to accept first kabla ya kulazimisha agenda zako lazima uelewe CCM ina mizizi ya bara na visiwani. Kwa upande wa bara CCM hana mpinzani mpaka sasa CDM ndio hao kila kukicha kufukuzana hawana stand point inayoeleweka. Upande wa visiwani CCM ni kweli inachangamoto na upinzani wa CUF, lakini wapo.

Mwisho wa siku hata hao CUF kama watakaa chini na kuangalia prospective za baada ya kuachana na bara hawana benefits zozote in the long run everything is short gain kwa hali ya dunia ya sasa ilivyo (kelele zao ni za udini tu), the only way after us ni kutawaliwa kama sio na sultan somebody else. But then where is the land na watapelekana wapi in the future, wasijidanganye uarabuni watabaguliwa tu, si kwa sababu ya rangi bali kuzaliwa. Land is everything katika dunia ya leo na wakitaka kuja huku wanaona sasa wenzao wanavyofanyiwa, that is just a simple rationale.

Rudi kwenye hali halisi ya malalamiko yenu ambayo mtanzania wakaida anaweza ku-sympathize na nyie ni kuhusu gharama za muungano, hilo swala linahitaji more devolution and agreements. Lakini sio tatizo kama wataona wao ardhi yao si ya mmbara, nasisi tukichukua msimamo huo kama viongozi wana akili yoyote lazima wagwaye, kwa sasa upande wa CCM bara kumejaa tricks isipokuwa awazitumii tu. ZnZ lazima waelewe madhumuni yetu ni kuwa sisi ni watu wamoja, lakini vinginevyo there is nothing we cant do without them na CCM bado has so many tricks under their sleeves only that the negotiation is poor.

Watu ambao kwa sasa hawana tricks ni wa serikali tatu na kuuvunja muungano, kwanza kosa lao kubwa ni kutotaka kutambua kama ZnZ ni nchi na muungano wetu ni wa unitary, kutotaka kujifunza miungano hii inafananaje ndio maana wanashindwa kueshimu katiba ya ZnZ na madai yao ya devolution haki ambzo ni za msingi kabisa kwa upande wao chini ya serikali mbili. Vilevile na sisi inabidi tuweke demands zetu, ni hapo tu ndio kwenye tatizo lakini si muungano. Serikali mbili ndio solution pekee, tatu ni bora kutokuwa na muungano kila mtu aende zake.
 
mkuu, zanzibar kwan ni mkoa?
Serikali moja, inaigeza Zamzibar mkoa wenye wilaya mbili Pemba na Ugunja, lakini ili kupunguza kelele, badala ya kuigeuza mkoa, inapewa hadhi ya jimbo, hivyo rais wa Zanzibar anakuwa ni Gavana General!.
Pasco
 
Serikali moja, inaigeza Zamzibar mkoa wenye wilaya mbili Pemba na Ugunja, lakini ili kupunguza kelele, badala ya kuigeuza mkoa, inapewa hadhi ya jimbo, hivyo rais wa Zanzibar anakuwa ni Gavana General!.
Pasco

haaha ahaha ahahah....mkuu pasco, naona unataka kumwagiwa tindikali ww, rais awe gavana?

na sera ya majimbo cc hawaezikubali ipite
 
haaha ahaha ahahah....mkuu pasco, naona unataka kumwagiwa tindikali ww, rais awe gavana?

na sera ya majimbo cc hawaezikubali ipite
Mkuu Wakikichi, si ni afadhali gavana, tungemgeuza RC ingekuwaje?!.

Pasco
 
hiyo katiba inayojadiliwa huko ni ya serikali moja, mbili ama tatu, je ni rasimu ya katiba ya muungano? ama ya serikali ya tanganyika, naona watu wanajilia kodi zetu tu, wengine ata hatuelewi kabisa katiba ya nini.
 
Vyanzo vyangu vya uhakika vinanieleza kwamba kauli ya Nape Nnauye hivi karibuni kwamba NEC imeazimia kwamba CCM inaenda na msimamo mmoja kwenye bunge la katiba kupigania sera ya ccm ya serikali mbili ni taarifa zisizo sahihi. Kwa mujibu wa chanzo changu, kikao kile kilimalizika huku wajumbe wakiwa wamegawanyika kuhusiana na msimamo wa chama juu ya mfumo wa muungano. Inasemekana kwamba wapo waliojenga hoja kwamba sera ya ccm haitakelezeki hivyo kuna haja ya serikali tatu na hoja hii kupokewa kwa nguvu sana ndani ya kikao, lakini pia wapo wachache walioendelea na msimamo wa serikali mbili ingawa makada hawa hawakuweza kufafanua wala kutetea kwanini serikali mbili ndio mfumo unaofaa. Iwapo walishindwa kusimamia hoja yao ndani ya chama, ni vigumu kuelewa wataisimamia vipi kwenye bunge la katiba. Ndio maana nimekuwa nikijadili sana kwamba kuna uwezekano wa makada wa ccm kumtumia mwalimu vibaya katika hoja zao pamoja na kuwatishia watanzania juu ya athari za serikali tatu kwa mujibu wa hoja zao za kutunga.

Kimsingi, sasa ni wazi kwamba ccm imebadilisha msimamo wake juu ya mfumo wa muungano, lakini inajisikia aibu kuja hadharani kuweka hilo wazi. Matokeo yake ni nape kuja hadharani kusema kwamba chama chake bado kinaamini katika muunda wa serikali mbili huku akielezea jinsi gani anaamini kero za muungano zitapata ufumbuzi. Nguruvi3 amejadili vyema jinsi gani such a belief na ndoto za alinacha kwani iwapo kero hizi zimeshindwa kupata ufumbuzi kwa miaka 50, tena chini ya ccm ya wakati ule ambayo ili command legitimacy kubwa sana mbele ya umma, tena kwa hiyai ya wananchi, iweje leo ccm ya kina nape ambayo kila kada ni msemaji wa chama, ccm iwe na uwezo wa kutatua kero za muungano? Tutazijadili kero hizi punde ili kupima hoja ya nape lakini kwa sasa ebu tuchambue zaidi ukinyonga wa ccm katika suala hili la mfumo wa muungano, hoja ya msingi ikiwa ni kwamba tamati ya mazingaombwe ya mfumo wa serikali mbili imeanza kuwa dhahiri kama mabandiko yangu ya awali yalivyoweka wazi.

Swali linalofuatia ni je, kwanini ccm imebadili msimamo wake wa awali?
Jibu ni kwamba, kama nilivyojadili awali, legitimacy ya CCM kutawala nchi haijawahi kuwa ni Katiba ya nchi as source of legitimacy bali mambo mengine (azimio la arusha na ujamaa, historia ya TANU kutetea haki za wanyonge ndani na nje ya nchi, na charisma ya baba wa taifa, Mwalimu Nyerere). Kama nilivyofafanua awali, all the three sources of legitimacy have now been eroded, mostly kwa sababu ya internal factors - ccm yenyewe kuliko external factors. Sasa CCM wamezinduka usingizini na kubaini kwamba bila ya uangalifu, msimamo wao sio tu utavunja muungano bali pia utakipotezea ushindi chama 2015.

CCM sasa imegundua kwamba msimamo wake kisera regardless how much msimamo huu unapakwa "make up" na kufanyiwa "face lift", ukweli kwamba serikali mbili hazitekelezeki ni ukweli usiokwepeka, and again kuendelea kulazimisha "face lift" kisera huku msimamo ukiwa ni serikali mbili mwisho wake ni kuvunja muungano.

Kinachojadiliwa kwamba ni nyaraka ya ccm ambayo imebeba mawazo mbadala ya rasimu ya pili ya katiba, inasemekana content yake kubwa ni matokeo ya waraka kutoka idara ya siasa na uhusiano wa kimataifa ya CCM ambayo ipo chini ya Dr. Migiro. Katika waraka huu ambao aliuwasilisha kwenye NEC iliyomaliza kikao chake hivi karibuni, kikao ambacho Nape Nnauye anatueleza kwamba chama kiliondoka na msimamo mmoja wa kusimamia serikali mbili, inasemekana kwamba mapendekezo ya migiro katika kikao kile cha NEC yalithibitisha kwamba kuendelea na mfumo wa serikali mbili ni kuchongea jeneza muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar. Jina la Tanganyika inasemekana linatajwa wazi wazi ndani ya vikao vya chama na wajumbe lakini wasemaji wa chama wakija hadharani, inatajwa "Tanzania Bara".

Msimamo huu wa migiro unatufanya tujiulize maswali kadhaa:
1. Was it a coincidence kwa Rais kumteua kuwa waziri wa sheria ba katiba?
2. Je, sasa tunapata idea juu ya kwanini Kikwete aliwaonya wana ccm kujiandaa kisaikolojia na ujio wa serikali tatu?
3. The fact kwamba haya yanaendelea huku kiongozi mkuu wa shughuli za serikali ambae pia ni mwenyekiti wa wabunge wa CCM Mizengo Pinda anasema haitambui Tanganyika, je maana yake ni kwamba ccm ipo tayari to settle na serikali tatu ilimradi ile ya tatu isiitwe Tanganyika?

Hapo juu niliahidi kurejea kujadili kero za muungano, kero ambazo Nape Nnauye katueleza kwamba ni changamoto ambazo zitafanyiwa kazi. Katika hili, Nguruvi3 ameuliza maa 17, mara 20, je ccm ina mwarubaini wakati huu baada ya kukosa tiba ya ugonjwa husika kwa miaka 50? Is there a medical break through that ccm is about to reveal? Its obvious kwamba jibu ni hapana, unless tushauriane kuwa wavumilivu kusubiri press conference ya Nape kwamba sasa chanjo ya kero za muungano imepatikana.

Naungana na Nguruvi3 na wengine kwamba kero za muungano haziwezi kupatiwa ufumbuzi chini ya serikali mbili. Tuangalie mambo ambayo nape anayaita changamoto za muungano na ana amini yatapatiwa ufumbuzi chini ya serikali mbili.

*kwanza ni suala la rais wa znz kuondolewa kuwa makamo wa rais wa JMT. Kama tunakumbuka vyema, miaka ya sitini, mwalimu alielezea umma kwamba mfumo wetu tumeiga ule wa unitary system wa UK. Mfumo huu ulifanikiwa kwasababu ya mfumo wa chama kimoja, ndio maana baada ya ujio wa vyama vingi, kuendelea na muungano wa "unitary" kungepelekea hali ya znz kuwa na ais wa chama kimoja na bara kuwa na rais wa chama kingine. Ndio maana akateuliwa jaji bomani kuja na solution ambae baadae akaja na wazo la mgombea mwenza kwa kuiga "federal structure" ya USA. Tukumbuke kwamba mkataba wa muungano (1964) ulilenga shirikisho (federalism) na kama ungefuatwa tangia mwanzo, kero za muungano zingekuwa chache sana, bearing in mind kwamba in any union, there's no absolute stability, but relative stability; ukweli huu upo USA, Australia, UK, Switzerland etc.

*pili (kero nyingine) ni ukweli kwamba chini ya serikali mbili, tutalazimika kuwa na mambo mengi ya muungano, suala ambalo litazidi kuimeza zanzibar. Tukumbuke kwamba for 50 years, the "union question" has always been the "zanzibar question". Katika hili, jaji warioba pia amelijadili kwa sura ya "koti la muungano" ambalo limevaliwa na Tanganyika.

*tatu, lenye uhusiano na hilo hapo juu la pili ni kwamba, chini ya serikali mbili, ni vigumu kutenganisha mamlaka ya serikali ya JMT kwa masuala ya muungano na mamlaka ya serikali hiyo hiyo kwa masuala yasio ya muungano. Jaji warioba alifafanua sana tatizo hili wakati wa halfa ya kuwasilisha rasimu ya pili ya katiba, na pia Nguruvi3 na wadau wengine humu wamelifafanua vizuri suala hili. Kimsingi, mfumo wa serikali mbili unaopigiwa debe na ccm unafukia madudu mengi sana yanayohusiana na mgawanyiko wa mapato na matumizi juu ya uendeshaji wa serikali ya muungano, na hii ni moja ya kero kubwa sana ambazo sasa watanganyika wameamua kuivalia njuga. Serikali mbili haiwezi kutatua kero hii bali serikali tatu kama nilivyowahi jadili kwa kina elsewhere, vinginevyo ikishindikana, kama asemavyo Nguruvi3, na pia job ndugai kaanza kutumia maneno haya haya, tupasue jahazi na kila mtu abebe mbao zake. CCM inajaribu to repair meli inayovuja, tena ikiwa katikati ya bahari. Its nonsense, its a non starter.

*tatizo lingine ambalo haliwezi kupatiwa ufumbuzi na serikali mbili ni the obvious one - katiba ya znz (2010) pamoja na yaliyomo mle, mambo ambayo znz haiwezi kurudi tena nyuma juu yake. CCM inajaribu kupigania katiba ya sasa ya JMT inayotambulisha Tanzania kama nchi moja wakati zanzibar kimsingi kama anavyosema Nguruvi3, imeshauvunja muungano uliopo. Katiba ya znz inaitambua znz kama moja ya nchi mbili zinazounda JMT.

Itaendelea.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Inaendelea toka #37


Katika harakati zake za kuendelea na mazingaombwe, makada wengi wa ccm wakiongozwa na nape waliishambulia sana tume ya warioba kwamba imekuja na mapendekezo yatayovunja muungano. Lakini makada hao hawajadili ukweli kwamba uongozi wa ccm umeshindwa kuizuia znz na katiba yake iliyovunja muungano unaotajwa ndani ya katiba ya JMT (1977). Pengine nirudie hili tena kwa makada wa ccm (nape, mkono, bulembo, kisumo etc) wanaopotoshwa ukweli na kukimbia chanzo cha tatizo ambalo ni ccm yenyewe:

Ni hivi- Hatua ya znz kubadili katiba yake 2010 sio tu imechukua madaraka ya muungano bali pia imeifanya katiba ya JMT kuwa irrelevant kwa mfano kwa kuelekeza sheria za muungano zilizopitishwa na bunge dodoma ziende kuamuliwa kwenye BLW unguja. Mbali ya hili, znz tayari ina bendera yake, wimbo wa taifa, na majeshi yake (kinyume na katiba ya jmt inayokataza uundwaji wa majeshi nje ya serikali ya jmt). Pia, kuna suala la mamlaka ya mahakama ya rufaa ya JMT ambayo kwa mujibu wa katiba ya jmt (1977), mahakama hii ina mamlaka ya kuamua rufaa zote ndani ya JMT. Lakini katiba ya znz (2010) katika ibara yake ya (99) inazuia mzanzibari yoyote kupelekea kwenye mahakama ya rufaa ya jmt, suala lolote linalohusu tafsiri ya katiba ya znz. Haya ni baadhi ya mambo ambayo yalichangia sana tume ya warioba kuja na pendekezo la serikali tatu ikizingatiwa kwamba ilikabidhowa hadidu za rejea zikitaka tume kulinda na kuboresha muungano. Now, given hatua ya znz kikatiba hapo juu, serikali mbili au moja zinatekelezeka kivipi???

Kwa kuhitimisha - hatimaye ccm imekubali kimsingi kwamba serikali tatu ndio suluhisho pekee lililobakia la kulinda muungano, sio moja wala mbili. Kazi yetu iliyobakia watanganyika ni kuondokana na hiki kiwavi "Tanzanoa Bara" na kuirudisha "Tanganyika Yetu". Kama nilivyo ahidi jana, nitajadili jinsi gani tulipoteza tanganyika ili tuwe katika nafasi nzuri ya kubadilishana mawazo juu ya jinsi gani tutampata tena tanganyika.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Ccm hawawezi kuisimamia misingi ya nchi kwa sababu misingi ya chama wameiua.
 
SEHEMU YA KWANZA

Hatimaye kiini macho cha muungano kinakaribia kukiumbua chama chetu kikongwe cha CCM. Kwa miaka 50 sasa, ccm iliwafanyia wananchi mchezo wa mazingaombwe and managed to get away with it. Lakini kama ambavyo nimekuwa nikisema over and over again, it reaches a to point when:



The "trick" nayozungumzia hapa ni suala zima la mfumo wa muungano wa serikali mbili (sera rasmi ya ccm), mfumo ambao umetawaliwa zaidi na kiini macho (illusion) kuliko ukweli au uhalisia wa mambo. Kwa mujibu wa dictionary, an illusion is:



Kitendo cha Chama Cha Mapinduzi kudanganya umma kwa miaka karibia 50 kwamba mfumo wa muungano uliopo ni mfumo wa serikali mbili, is deceiving the people kwani for 50 years, the party has been busy producing a false impression before the people that the Government of Tanganyika doesn't exist while in reality, it has been in existence since 1964.

Kada wa CCM na Mwanasiasa Mkongwe kutoka Zanzibar ambae pia historia inamweka kama mmoja wa wajumbe thelathini wa Revolutionary Council (1964), Mzee Hassan Nassor Moyo alinukuliwa na Mwandishi wa Gazeti la ----- toleo la Oktoba 3-9, 2013 akisema maneno yafuatayo:



Huu ndio uhalisia wa mambo, uhalisia ambao viongozi wa CCM wameamua kujitoa mhanga kuugeuza kuwa "kiini macho" (illusion) kwa miaka 50 ya muungano. Tulitarajia viongozi vijana ndani ya ccm kama kina Nape Nnauye ndio wawe mstari wa mbele kukirekebisha chama katika kosa lake hili ambalo kimsingi, huko tuendako ndio litakuwa ni sanda katika jeneza la ccm kama chama tawala nchini Tanzania. Nape Nnauye amefika hapo alipo kutokana na umahiri wake wa kusimamia haki, uwazi, na ukweli lakini kumbe ilikuwa ni danganya toto kwani lilipokuja suala la kusimamia haki ya msingi kabisa ya watanganyika, ikizingatiwa kwamba haki yetu kikatiba imeshaporwa na katiba ya zanzibar (2010), nape na viongozi wenzake ndani ya chama wameshindwa kusimamia haki yetu ya msingi na ya kikatiba. Badala yake, tumemsikia nape na wenzake wakitoa maneno ya kejeli na mara nyingine matusi kwa wananchi (hata wazee wao) wanaotetea haki ya Tanganyika katika muungano wetu.

Kama vile ccm imeshindwa kabisa kusoma alama za nyakati na kuamua kufa na tai yake shingoni, wiki chache kuelekea bunge la Katiba, CCM kupitia Nape ilikuja na tamko la CCM (NEC) ambalo lilisisitiza kwamba chama kinaelekea bungeni kwenda kupigania msimamo na sera yake ya serikali mbili ndani ya muungano. Swali kwamba ccm iliwashirikisha vipi watanzania (let alone wanachama wa ccm) kabla ya kufikia uamuzi mkubwa kama huu, ni swali ambalo limekosa wa kulijibu ipasavyo. Wanaojitahidi kulivaa swali hili huwa wanaishia kuisingizia historia. Wanasahau kwamba historia kamwe haiwezi singiziwa, na hili litazidi kuwa dhahiri huko tuendako.

Baada ya chama kuingia kwenye bunge la katiba na msimamo wake wa serikali mbili licha ya rais kuhimiza vyama kuacha tabia ya kuweka mbele itikadi za vyama na badala yake maslahi ya taifa, zimeenea taarifa kwamba ccm sasa imekuja na waraka wa rasimu ya katiba mbadala, habari ambazo bado hazijakanushwa na ccm hadi sasa. Cha ajabu ni kwamba ndani ya waraka huo, inadaiwa kwamba chama kinapendekeza uwepo wa baraza la wawakilishi la "Tanzania bara" kwa ajili ya kushughulikia masuala ya bara tu. Hii ni ajabu kwani rasimu ya katiba (2013 na hata mkataba wa muungano (1964) hakuna pahala inataja "Tanzania Bara", hivyo kutuacha na swali la msingi kabisa kwamba je, Zanziba iliungana na Tanzania Bara?

Haya ndio mazingaombwe ya ccm ambayo ni dhahiri yanaelekea ukingoni kwani kuna kila dalili sasa kwamba "our great magician is running out of tricks"; swali linalofuatia ni je,

*How many more tricks could CCM have in the hat?
Mzee Mwanakijiji alijadili vizuri suala hili katika mjadala wetu mwingine.

Kilichodhahiri ni kwamba mashabiki wengi sana tayari wameshatoka kwenye ukumbi huu wa mazingaombwe baada ya kuanza kumshtukia mwanamazingaombwe na hata wale ambao bado wapo ndani ya ukumbi, wengi wao hawapo tena kushangilia yanayojitokeza jukwaani bali wanajadili yalio nje ya jukwaa.

Wanachojadili wengi ni jinsi gani ccm baada ya kutambua kwamba umma utaiumbua 2015, imefikia hatua ya kufanya vituko ndani ya bunge la katiba, kinyume kabisa na matarajio ya wengi ambao walitegemea ccm itaenda kutetea sera yake ya muungano wa serikali mbili kwa hoja. Moja ya vituko hivi ni kile cha ccm aidha kwa kujua au kutokujua, kuunga mkono mfumo wa serikali tatu kwa kupendekeza baraza la wawakilishi la Tanzania Bara pekee, lakini hapo hapo chama kikisema kwamba hakita yumba na msimamo wake wa serikali mbili (mfano rejea kauli ya waziri mkuu pinda hivi karibuni). Katika hili, nadhani mzee hassan nassor moyo alilizungumzia vizuri katika mahojiano yake na gazeti la ----- mwaka jana aliposema hivi:



Maneno haya ya mzee Moyo yanazidi kuelezea uhalisia wa mambo, kwani iwapo ni kweli wana ccm kwenye bunge la katiba sasa wamefikia hatua ya kupendekeza uwepo wa baraza la wawakilishi la kushughulikia masuala ya "Tanzania Bara", basi kweli kuna haja ya kuwapima akili kwani kwa maana hii, uelewa wao ni kwamba Zanzibar iliungana na Tanzania Bara na sio Tanganyika.

----- pia linamnukuu Mzee Moyo Katika kongamano la kamati ya maridhiano lililofanyika hoteli ya bwawani mwaka jana (2013, akisema:



Wajumbe wa kongamano wakajibu "matatuuuuuu!"

Mzee moyo akauliza:



Lakini kama tunakumbuka vyema, vituko vya ccm vilivyoashiria kilometa za mwisho za safari ya mazingaombwe vilianzia pale wazanzibari walipofanya mambo makuu mawili muhimu:

1. Kujipatia Katiba yao (2010)inayoitambua Zanzibar kama "moja ya nchi zinazounda JMT". Hii ni tofauti na Katiba yake ya awali ambayo iliitambua zanzibar kama "sehemu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania".
Tume ya katiba chini ya jaji warioba pia inaakisi hili katika utangulizi wa rasimu iliyopo mbele ya wajumbe wa katiba dodoma leo.

2. Serikali ya CCM ilipopeleka muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba kwa wazanzibari, ndugu zetu wazanzibari kama iliyo jadi yao kuipigania Tanganyika kama njia yao ya kufanikisha zanzibar kutambulika kama dola kamili, waliuchana na kuuchoma moto muswada ule kwani ulizuia suala la muungano kuwa sehemu ya mjadala kama vile muungano ni suala ordained from God na sio suala linalojengwa na kulindwa na watu/wananchi. Isingekuwa busara za waziri sitta ambae ndiye aliyeiwakilisha serikali katika halfa ile, pengine leo tungekuwa tunaongea mengine.

Itaendelea...



Cc Nguruvi3, Nape Nnauye JokaKuu Jasusi happyfeet, Bongolander, Mag3 Candid Scope MTAZAMO Kimbunga Mkandara Pasco, Zinedine, Zakumi, gfsonwin Kobello, zumbekuu, Kichuguu JingalaFalsafa ZeMarcopolo Ritz, Mzee Mwanakijiji, zomba MwanaDiwani, EMT, AshaDii, ukwelikitugani, TIMING, na wengine wote niliowasahau;



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

- Kaka unanikumbusha sana maneno ya Jana kuna Mbunge mmoja wa bunge la Katiba alisema "kuna watu humu bungeni wandhani wao tu ndio wanajua na kwamba wao tu ndio wamesoma wengine wote hatujui kitu, ukweli ni kwamba Uingereza haina wala haijawahi kuwa na Katiba", I mean the way you writte ni kama vile wengine wote humu JF ni wajinga wajinga flani hivi ni wewe tu ndio mwenye akili humu ndani na waht you say ndio final truth, ukweli ni kwamba una hasira sana na CCM na kwa muda mrefu sana lakini mpaka leo hakuna utabiri wowote uliowahi kuutoa ukawa kweli, umetabiria mabaya CCM kwa muda mrefu sana lakini never happened hata mara moja na here you are as usual na mahasira yako na mautabiri ya waganga wa kienyeji,

- I mean kaka Nassoro Moyo ndiye peke yake aliyebaki kati ya walioanzisha Muungano? Kama alikuwa na tatizo na Muungano kwa nini hakusema Muasisi wake Mwalimu alipokuwa hai? Nassoro Moyo ana nafasi gani ya uzito wa kisiasa Visiwani sasa hivi? He is nobody, sasa kuandika post based on what Nassoro Moyo said baada ya kuukubali Muungano kwa robo tatu ya maisha yake na kujaribu kuubeza now unasema huyo ndio anatakiwa kuwa the final say ya Muungano uwepo au usiwepo? Really?

- Kwenye Criminology nilifundishwa mtu anayejiamini na kujua anachokisema huwa hataji majina ya wengine kwenye hoja zake, sasa wewe tizama watu wote uliowataja na kuwatumia copy ya hii post yako I mean una wasi wasi wa nini kama unajua na kuamini ulichoandika ni sawa sawa, why Mwanakiijiji hivi ni kweli unaamini Mwanakijiji hataki Muungano kama wewe?,

- Eti CCM ilikuwa inawadanganya wananchi kwa miaka 50? na wewe ulikuwa wapi miaka yote hiyo kuwaelimisha wananchi kwamba CCM inawadanganya? I mean wanaodai Serikali tatu wanatumia akili zao ila wale wote wanaodai Serikali mbili wametumwa na CCM? Really kweli an academician unaweza kusimama na kundika low arguments kama hizi?

- Kaka mimi ni muumini wa Serikali Mbili tu, siamini in Serikali tatu kwa sababu kwanza Dunia nzima hakuna Taifa lenye Serikali Tatu, pili Muungano uliua Serikali za Tanganyika na Zanzibar na kuunda Serikali ya Tanzania ndiyo ninayoitaka na kuiamini na ndio ninaisimamia na nitaisimamia mpaka mwisho, sijatumwa na CCM na wala wewe siamini kuwa umetumwa na WApinzani, jamani acheni kujipa madaraka ya kuwakilisha wananchi na huku hamjachaguliwa kuwawakilishia mawazo yao, kila mwananchi wa Tanzania ana haki ya kutoa mawazo yake, wewe mawazo yako ni kuvunja Muungano that is all ungetoa hoja on that line badala ya kujipachika madaraka ambayo ya kuwaongelea wananchi kwa hoja weak kama ulizotoa, kwa kutumia maneno ya Kiongozi ambaye wala hana nafasi yoyote kubwa kwenye siasa za Taifa wapo wanaomzidi wengi sana na bado hawawezi kuongelea wananchi wengine,

- Kaka nasikia kutapika sana ninapoona unakichafua CCM kwa kujifanya na wewe ni CCM na huku unajua wazi kwamba wewe sio CCM ila ni muumini wa kuona CCM inavurugika kitu ambacho hakitakuja kutokea, umetoa utabiri wako wa waganga wa kienyeji kwa muda mrefu sana kuhusu matatizo ndani ya CCM lakini ndio kwanza CCM ipo vizuri na imeshinda Viti 23 vya Udiwani na huku unaowatetea wamepata viti 3 pamoja na helikopta zote walizotumia, kaka si wanasema shetani akiwa mzee anakuwa malaika maana toka uanze na utabiri wako against CCM haujawahi kutoa hata mara moja badilika kaka!!

Le Mutuz
 
Back
Top Bottom