CCM Na Bunge La Katiba: Mazingaombwe yanayoelekea ukingoni

CCM Na Bunge La Katiba: Mazingaombwe yanayoelekea ukingoni

- Kaka unanikumbusha sana maneno ya Jana kuna Mbunge mmoja wa bunge la Katiba alisema "kuna watu humu bungeni wandhani wao tu ndio wanajua na kwamba wao tu ndio wamesoma wengine wote hatujui kitu, ukweli ni kwamba Uingereza haina wala haijawahi kuwa na Katiba", I mean the way you writte ni kama vile wengine wote humu JF ni wajinga wajinga flani hivi ni wewe tu ndio mwenye akili humu ndani na waht you say ndio final truth, ukweli ni kwamba una hasira sana na CCM na kwa muda mrefu sana lakini mpaka leo hakuna utabiri wowote uliowahi kuutoa ukawa kweli, umetabiria mabaya CCM kwa muda mrefu sana lakini never happened hata mara moja na here you are as usual na mahasira yako na mautabiri ya waganga wa kienyeji,

- I mean kaka Nassoro Moyo ndiye peke yake aliyebaki kati ya walioanzisha Muungano? Kama alikuwa na tatizo na Muungano kwa nini hakusema Muasisi wake Mwalimu alipokuwa hai? Nassoro Moyo ana nafasi gani ya uzito wa kisiasa Visiwani sasa hivi? He is nobody, sasa kuandika post based on what Nassoro Moyo said baada ya kuukubali Muungano kwa robo tatu ya maisha yake na kujaribu kuubeza now unasema huyo ndio anatakiwa kuwa the final say ya Muungano uwepo au usiwepo? Really?

- Kwenye Criminology nilifundishwa mtu anayejiamini na kujua anachokisema huwa hataji majina ya wengine kwenye hoja zake, sasa wewe tizama watu wote uliowataja na kuwatumia copy ya hii post yako I mean una wasi wasi wa nini kama unajua na kuamini ulichoandika ni sawa sawa, why Mwanakiijiji hivi ni kweli unaamini Mwanakijiji hataki Muungano kama wewe?,

- Eti CCM ilikuwa inawadanganya wananchi kwa miaka 50? na wewe ulikuwa wapi miaka yote hiyo kuwaelimisha wananchi kwamba CCM inawadanganya? I mean wanaodai Serikali tatu wanatumia akili zao ila wale wote wanaodai Serikali mbili wametumwa na CCM? Really kweli an academician unaweza kusimama na kundika low arguments kama hizi?

- Kaka mimi ni muumini wa Serikali Mbili tu, siamini in Serikali tatu kwa sababu kwanza Dunia nzima hakuna Taifa lenye Serikali Tatu, pili Muungano uliua Serikali za Tanganyika na Zanzibar na kuunda Serikali ya Tanzania ndiyo ninayoitaka na kuiamini na ndio ninaisimamia na nitaisimamia mpaka mwisho, sijatumwa na CCM na wala wewe siamini kuwa umetumwa na WApinzani, jamani acheni kujipa madaraka ya kuwakilisha wananchi na huku hamjachaguliwa kuwawakilishia mawazo yao, kila mwananchi wa Tanzania ana haki ya kutoa mawazo yake, wewe mawazo yako ni kuvunja Muungano that is all ungetoa hoja on that line badala ya kujipachika madaraka ambayo ya kuwaongelea wananchi kwa hoja weak kama ulizotoa, kwa kutumia maneno ya Kiongozi ambaye wala hana nafasi yoyote kubwa kwenye siasa za Taifa wapo wanaomzidi wengi sana na bado hawawezi kuongelea wananchi wengine,

- Kaka nasikia kutapika sana ninapoona unakichafua CCM kwa kujifanya na wewe ni CCM na huku unajua wazi kwamba wewe sio CCM ila ni muumini wa kuona CCM inavurugika kitu ambacho hakitakuja kutokea, umetoa utabiri wako wa waganga wa kienyeji kwa muda mrefu sana kuhusu matatizo ndani ya CCM lakini ndio kwanza CCM ipo vizuri na imeshinda Viti 23 vya Udiwani na huku unaowatetea wamepata viti 3 pamoja na helikopta zote walizotumia, kaka si wanasema shetani akiwa mzee anakuwa malaika maana toka uanze na utabiri wako against CCM haujawahi kutoa hata mara moja badilika kaka!!

Le Mutuz

tatizo lako uko kichama sana ila katika katiba hii lazima tumbambanue kwa upana zaidi, hivi unadhan ni sahii kwa zanzibar kua na katiba iliyowapa mamlaka makubwa kiasi hiki?

ishu ni kwamba,zanzibar inajipambanua kama nchi iliyokamilika sasa hivi,tanzania bara (tanganyika iko wapi?)
katiba ya zanzibar inasema tanzania ni muungano wa nchi 2,tanganyika na zanzibar..sasa tanganyika iii wapi?
 
Macho na masikio yetu bado yapo in the magic shop "Dodoma" ambako CCM inaendelea na mazingaombwe yake ya serikali mbili ndani ya muungano wa two "sovereign states" Zanzibar na Tanzania bara?. Kama ambavyo nimekuwa najadili, kikomo cha mazingaombwe hayo hakipo mbali kwani our dear magician is running out tricks. Yapo mengi ambayo yanaendelea kujadiliwa kwa kina kwenye duru za siasa, ambapo kuna uzi kwenye forum ya great thinkers ya mdau mwenzetu Nguruvi3 yenye kichwa kisemacho
Duru za siasa: Bunge la katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka tanganyika
. Kwa jinsi navyoendelea kumsoma Nguruvi3, umuhimu na utofauti wa mjadala wake na huu na mingine mingi ni kwamba mwenzetu anatupeleka nyuma zaidi katika historia na kuchambua mambo yote ya msingi hatua kwa hatua kabla ya kutufikisha hapo tulipo, kwani hivyo ndivyo tutajua twende vipi mbele bila ya kujalisha sana bunge la katiba litakuja na hatima gani juu ya Tanganyika. Tunakushukuru sana mkuu Nguruvi3 kwa mjadala wako, tunasubiri kwa hamu uukamilishe, vinginevyo kufikia hatua ya sasa wengi tunaelewa kwamba mada yako itatuelimisha sana juu ya masuala haya yafuatayo:

1. Jamii zetu zilikuwa ni jamii za namna gani na zenye uhusiano wa namna gani kabla ya muungano.

2. Muungano wa 1964 ulilenga kufanikisha nini kwa washirika (Tanganyika na Zanzibar).

3. Nini ni faida/mafanikio ya muungano, yepi kwa Zanzibar na yepi kwa Tanganyika.

4. Nini ni hasara za muungano kwa pande zote za "nchi washirika" na kwa "muungano" wenyewe.

5. Nini ni kiini cha mgogoro wa muungano kwa miaka 50 (kisiasa na kisheria).

6. Juhudi gani zimefanyika huko nyuma kuokoa muungano na je zimefanikiwa? Kama sio, kwanini?

7. Iwapo tuiamini ccm (rejea kauli ya Nape Nnauye) kwamba miaka 50 baadae, kero za muungano zitapatiwa ufumbuzi na CCM chini ya serikali mbili.

8. Kwanini zanzibar bila Tanganyika
Hakuna muungano.

9. Kwanini hoja ya Mh. Pinda juu ya Tanganyika kabla na baada ya uhuru ni hoja dhaifu.

10. Nini kitatokea iwapo bunge la Katiba litashindwa kuzindua Tanganyika?

Haya ni baadhi ya mambo ambayo uzi wa Nguruvi3 umeahidi kuyafanyia kazi. Wakati tukimsubiri amalize mada yake, hapa ningependa kujadili machache kuhusiana na mazingaombwe ya ccm yanavyoendelea kule Dodoma, mazingaombwe ambayo hakika tamati yake haipo mbali.

Wiki kadhaa zilizopita, Kupitia katibu wake mwenezi wa chama @nape, CCM ilisisitiza juu ya msimamo wake wa serikali mbili kuelekea bunge la katiba, msimamo ambao Nape alieleza umma kwamba ulipitishwa unanimously na wajumbe wa NEC. Muda sio mrefu tukaja kubaini kwamba nape hakusema ukweli bali ukwelo ni kwamba wajumbe na wabunge wa ccm wamegawanyika sana juu ya Tanganyika, na hii ni kwa ngazi zote za chama. Wengi tulishindwa kuelewa kauli ya nape inasimamia maoni na maslahi ya ccm ipi, ccm ambayo bila ya uangalifu, suala la katiba mpya itaipiga mweleka uchaguzi mkuu wa 2015.

Kufikia hatua hii, yanayoendelea dodoma hasa kuhusiana na kura ya wazi dhidi ya kura ya siri, yanatufanya tuseme kwa kujiamini kabisa kwamba kumbe
siri ni serikali tatu, wazi ni serikali mbili
. Hali hii ni ya hatari sana sio tu kwa stability ya ccm bali muungano wenyewe na taifa kwa ujumla.

Waraka wa ccm juu ya rasimu ya katiba umezidi kudhihirishwa jinsi gani ccm ilivyoamua kuendelea kuwekeza katika mazingaombwe, mazingaombwe ambayo "return on investment" itakuwa ni negative/ a big loss. Ningependa kuzungumzia moja ya mapendekezo (mazingaombwe) ya ccm kwamba
ndani ya muungano wa serikali mbili, pawepo na baraza la wawakilishi la Tanzania Bara ambalo litakuwa na kazi moja tu - kushughulikia masuala ya bara pekee
. Ni vigumu kuelewa kwanini ccm inadhania hili litawezekana. Pengine ccm inadhania kwamba ccm itatawala milele lakini muhimu zaidi, inadhania source of her legitimacy inaendelea kuwa masuala mengine nje ya katiba ya nchi, masuala niliyojadili awali (ujamaa/azimioa la arusha, historia na mafanikio ya Tanu kutetea wanyonge na jina la baba wa taifa kama charismatic leader na mwenye uadilifu na uzalendo kwa taifa lake). Kama nilivyojadili, haya yote yameshakwenda kwa maji na ni kutokana na makosa ya ccm yenyewe, kwahiyo ccm haitaweza tena to command legitimacy ya kutawala kwa vyanzo vingine bila katiba ya nchi, and any attempt to tamper mchakato wa katiba, hasa kuendelea kuizika Tanganyika itakuja andikwa kwenye historia kwamba - ccm ilijimaliza yenyewe na pia iliuvunja muungano.

Again, hoja ya kuwepo kwa baraza
La wawakilishi litakaloshughulikia masuala ya Tanzania bara ni jambp lisilowezekana chini ya mfumo/sera ya serikali mbili. CCM inapendekeza kwamba katika baraza hilo la wawakilishi, wabunge kutoka zanzibar watakuwa wanaambiwa watoke nje pale masuala ya Tanzania yatakapokuwa yanajadiliwa. How pathetic. Ccm inashindwa kuelewa kwamba kitendo cha kuwazuia wabunge wa zanzibar wasishiriki katika mijadala juu ya masuala ya Tanzania bara chini ya serikali mbili kitazua mgogoro mkubwa sana, kinyume na hoja za nape kwa niaba ya ccm kwamba migogoro ya muungano itapatiwa ufumbuzi. Kitendo hiki kitazua mgogoro kwa sababu: chini ya mfumo wa serikali mbili, hakuna kitu kama "mambo ya Tanzania bara pekee" kwani chini ya mfumo huo, kuna mambo ya zanzibar na mambo ya muungano tu! Mazingaommbwe ya ccm yanataka kutuaminisha kwamba chini ya serikali mbili kutakuwepo na bunge la Tanzania bara ambalo litatokana na wananchi wa "Tanzania Bara". Nape na wanamazingaombwe wenzako, naomba niwaulize, je:

*Masuala ya Tanzania Bara yatasimamiwa na nani wakati yatakuwa hayana serikali yake????
*Hamuoni kwamba ndani ya serikali mbili kuna masuala ya zanzibar na ya muungano pekee yake?
*Je nani atawajibika kutekeleza yale yatakayofanyiwa kazi na bunge hilo la wawakilishi la Tanzania bara? Serikali ipi?

Tangia elimu ya awali kabisa tunajifunza kwamba bunge ni moja ya mihimili mitatu ya dola ambayo ni mahakama, serikali na bunge lenyewe. Hili bunge la Tanzania bara litaendeshwa na serikali ipi?

Watanganyika wenzangu, hata kwa kutumia akili ndogo tu tunaona kwamba hatuwezi kuwa na mabunge mawili ndani ya bunge la muungano yani bunge la muungano na bunge la tanzania bara bila ya kuwa pia na baraza la mawaziri la Tanzania bara na pia bila ya kiongozi wa kusimammia baraza hilo, whether tumuite rais, waziri mkuu, gavana au vyoyote itakavyoamuliwa.

Nape na ccm wanatufanya watanzania kwamba ni hamnazo kabisa. Niwaulize swali lingine:

*Chini ya serikali mbili yenye bunge la muungano na baraza la wawakilishi la Tanzania bara, nafasi ya mawaziri wa Tanzania bara, je - nini itakuwa ni nafasi ya mawaziri wasiokuwa wa muungano wakati baraza la mawaziri litakapokuwa linajadili masuala ya muungano?

*Je, iwapo tutakuwa na rais mmoja wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, nani atakuwa ndiye mwenyekiti wa kusimamia mambo ya Tanzanoa bara katika serikali ya muungano?

*iwapo itatokea rais wa jamhuri ya muungano atatokea zanzibar (taifa kamili baada ya katiba ya znz 2010), rais huyu atawezaje kusimamia masuala ya Tanzania bara? Kwa mamlaka gani atakayokuwa nayo?

*Je, iwapo rais wa muungano atatokea Tanzania bara, atakuwa na mamlaka yepi ya kusimamia masuala ya Tanzania Bara wakati atakuwa ameingizwa madarakani na pande zote mbili za muungano?

Katika mapendekezo yake, ccm haijaja na maelezo kwa maswali yote hapo juu.

Wananchi wenzangu, zipo wapi pande mbili za muungano bila ya kuwepo kwa Tanganyika kama mshirika mmoja wapo wa muungano? Katiba ya zanzibar inamtambua Tanganyika namna hiyo.

Inaendelea bandiko linalofuatia...



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Inatoka bandiko #82


Mapendekezo ya ccm yanatutia tu kichefu chefu na kuzidi kutuvuruga hasa tunapochanganya pendekezo hili na lingine kutoka ccm kwamba rais wa znz afanywe kuwa makamu wa rais wa muungano bila ya kujali iwapo rais wa muungano anatokea znz au Tanzania bara. Kimsingi, nape na ccm inapendekeza kwamba chini ya serikali mbili, huku mshirika mmoja wapo (zanzibar) tayari ikiwa na katiba yake, bendera, wimbo wa taifa, rais wake kama amiri jeshi mkuu, ccm bado itatulazimisha kwamba - Rais
Wa znz atakuwa ni makamu wa muungano bila ya kujalisha rais wa muungano atatkea upande upi wa muungano. Kwa maana nyingine, nape na ccm wanajenga mazingira ya Taifa kuwa na raus na makamu wa rais kutokea upande moja wa muungano (zanzibar), lakini pia kwa mapendekezo haya, zanziba itabidi wafute ndoto za kuwa na rais wa muungano! Hii ni kwa sababu, kufuatia mfumo wa vyama vingi, ni wazi kwamba iwapo rais wa muungano na makamo wake wote watatokea znz, ccm haitapata kura za kukipa ushindi Tanzania bara, hii itakuwa ni fursa ya upinzani kushinda urais wa muungano kwani watanzania bara (watanganyika) Watapiga kura za hasira dhidi ya ccm. Je ccm inaliona hili?

As a matter of fact, iwapo itatokea scenario ya rais na makamo wake wote kutokea znz, ni ccm yenyewe ndio itakayoanza minyukano yenye lengo la kuzuia rais wa muungano kutoka znz asipite. Itajengwa hoja nyepesi sana kwamba mzanzibari hawezi kuchagulika kuwa rais wa muungano chini ya mfumo wa sasa ambapo simple majority victory inampa mgombea urais ushindi, hapa nazingatia ukweli kwamba majority ya wapiga kura wapo Tanzania bara (Tanganyika) na hawa kamwe hawatampigia kura mzanzibari kuwa rais wa muungano huku wakijua rais wa znz automatically atakuwa ni makamo wa rais wa muungano. Katika hali hii, ccm imekwama: kwa upande mmoja, ccm itakosa kura za watanganyika nafasi ya urais wa muungano kwa kumsimamisha mzanzibari ambae tayari atakuwa anatokea upande wenye mamlaka kamili. Hili litaitoa ccm madarakani. Kwa upande mwingine, ili kunusurika ndani ya mazingaombwe yake, ccm italazimika kunyima wazanzibari fursa za kuteuliwa kuwa wagombea urais wa muungano, na uamuzi huu utalirudisha taifa kule kule kwenye mgogoro usiokwisha wa muungano.

Atakae vunja muungano ni CCM.

Itaendelea...



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kufuatia hotuba ya Kikwete bungeni juzi, hotuba ile imeweka wazi kwamba the magician has completely run out of tricks.

Baada ya mbinu zote za mazingaombwe kwisha, Chama sasa kimeamua kupingana waziwazi na mapendekezo ya wananchi kupitia rasimu ya katiba, huku pia kikiwatishia wananchi kwamba ufufuo wa Tanganyika utaambatana na vifaru na mizinga barabarani. Wengi wapenda mabadiliko ndani ya chama tulitarajia kwamba mwisho wa chama hiki kisichotaka kubadilika na kusoma alama za nyakati, baada ya kuishiwa mbinu zote za mazingaombwe, kitafanya ilichoamua kufanya.

CCM imekataa kabisa kubadilika na kuamua kutafuta uhalali wa kutawala kwa kupitia katiba itokanayo na wananchi kama source of her legitimacy; chama kinadhania kwamba kitaendelea kuwa "free rider" of sources that gave Nyerere (and somewhat Mwinyi), legitimacy to rule the country, na nilijadili sources hizi ambazo hazikujali kabisa katiba ya nchi bali:

1. Historia ya TANU na CCM ya kabla ya 1992, ya kutetea wanyonge wa ndani na nje ya nchi; Ccm inasahau kwamba this source of legitimacy is gone by the wind, na wakulaumu ni ccm wenyewe kwani leo chama kinatetea wale wenye nguvu wa ndani (matajiri na mafisadi) na wa nje ya nchi (wawekezaji).

2. Azimio la arusha ambalo liliweka utaifa kwanza (kwa dhati, sio porojo za ilani ya uchaguzi), huku wananchi wakiwekwa at the centre/heart ya mikakati yote ya maendeleo kiuchumi na kijamii; chama kinasahau kwamba just as the above source of legitimacy [see item (1)], this source too is gone by the wind na wakulaumu ni ccm yenyewe ambapo 1992, iliua azimioa la arusha na kuleta azimio la znz ambalo kimsingi, sasa linatumika kama kichaka cha ufisadi na kujilimbikizia mali ya umma; hata nyerere aliwahi sikika akishangaa hili kutokea tena bila hata ya kuambiwa;

3. Source ya tatu ya legitimacy wakati ule ilikuwa ni charisma & integrity ya Mwalimu; hapa pia ccm inasahau kwamba leo mwalimu hayupo, na wala hakuna dalili kwamba kuna viongozi ndani ya ccm watakaoweza kuvaa viatu vyake;isitoshe, viongozi wa aina hii leo wanachukuliwa na makada wa ccm kama wasaliti na maadui, hivyo juhudi zao za kutafuta uongozi zitapigwa vita na fitina za kila aina;hawataweza pita michakato ya uongozi ccm;

CCM kimepoteza fursa muhimu sana ambapo kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi, hatimaye serikali yake kwa mara ya kwanza ingepata uhalali wa kuongoza nchi kwa mujibu wa katiba itokanayo na wananchi, kitu ambacho hakijawahi kutokea; changamoto ya ccm ndani ya mfumo wa vyama vingi ilibakia zaidi katika suala la katiba mpya;baada ya chama kuipiga dana dana miaka nenda miaka rudi, Kitendo cha kikwete kuridhia mchakato wa katiba (2010)kilikuwa ni muhimu na cha kishujaa kwani hatimaye ccm ingekuwa na fursa ya kujenga uhalali wa kutawala kwa njia ya katiba kama chanzo cha uhalali utawala wake;

Kikwete angeshauriwa vizuri sana na mapema kabisa - baada ya idara ya usalama, washauri wake wa masuala ya siasa, uchumi na kijamii kumueleza uhalisia wa mambo 2010, hasa baada ya katiba mpya ya znz kupitishwa, wangemueleza mapema kabisa kwamba mzee hali ni ngumu kwani hoja ya serikali tatu haikwepeki tena, kwahiyo ni sawa ccm iendelee na msimamo wake wa serikali mbili lakini chama kiseme kwamba iwapo maoni ya wananchi kupitia mabaraza ya katiba yatasema kitu tofauti, basi ccm itayazingatia maoni hayo kwa kuzingatia mazingira yaliyopo. Kitendo hiki kingeipa ccm mtaji mkubwa sana wa kisiasa na kukiwezesha chama kuaminiwa na umma hata kama kingekuja na msimamo baadae (kwa hoja) kwamba migogoro iliyopo inatatulika chini ya serikali mbili; ni kweli uamuzi huu ungaugawa umma lakini bado ccm ingebakisha a good number of votes for 2015;vinginevyo ccm imepoteza fursa hii, na hili litakigharimu sana chama kwenye uchaguzi mkuu ujao, hasa katika majimbo ya mijini (kura za urais na ubunge); maeneo ya vijijini yataendelea kuipa ccm uhalali wa kutawala kupitia mabakibaki ya three sources of legitimacy nilizojadili hapo juu, lakini kwa mijini, the major source of legitimacy ya uongozi wa ccm na serikali yake itakuwa ni katiba itokanayo na wananchi;

Kwa kweli mikakati ya sasa ya chama sio sustainable for the party na pia sio stable for the country; chama na mikakati yake soon kitajikuta on a collision course na demographic trend za nchi kwani these show kwamba by 2025, karibia majority ya wananchi watakuwa wanaishi mijini - hawa watakuwa wapiga kura kwa kigezo cha katiba kama source of legitimacy kwa serikali na chama husika; kwa mwendo huu, ccm itakuwa inaendesha siasa za "mabakimabaki" ya legitimacy tatu nilizojadili hapo juu i.e vyanzo vya uhalali wa ccm kutawala nchi, na hatimaye chama kupotea katika anga za siasa za Tanzania. There is very little that can be now to reverse the trend ya ccm kufa ingawa itajitahidi sana kufa kiume. Kwa maana nyingine miaka sio mingi, CCM will eventually dissapear in the political grave yard ya Tanzania; the year is 2025 iwapo katiba mpya ya ki-ccm itadumu kwa miaka kadhaa, vinginevyo ccm itaweza pita 2015 lakini haitafika 2025 kwani njia mbadala za kuifufua Tanganyika zitakuwa zimeiva huku ccm ikikosa kuzithibiti:

1. Kura ya maoni kuhoji wananchi iwapo wanautaka muungano.

2. Wananchi kupata fursa ya kuchaga bunge la kweli la katiba kupitia sanduku la kura. Au

3. Mabunge ya JMT na BLW kuifufua Tanganyika kwa njia kama ile iliyotumika Kenya (Bomas Draft).

Kuelekea 2015, ccm itapoteza kura nyingi za mijini kwani umma sehemu hizi utakuwa umeelimika na utapiga kura kwa nia ya kukipa chama cha siasa ridhaa ya kuongoza na kuwa na uhalali kutawala kupitia katiba ya nchi kama source of legitimacy; huko vijijini, ccm itaendelea kupata kura nyingi kwani vijijini, bado wengi watatumia the three sources of legitimacy nilizojadili hapo juu kuichagua ccm; however, this will be short lived kwani as discussed already, given the demographic changes whereby not only Tanzania but africa is urbanizing more and more, itafikiwa siku (2025 to be specific) ambapo majority ya wapiga kura wataacha kukipa ccm uhalali kwa vigezo nje ya katiba (rejea three sources of legitimacy wakati wa nyerere), bali katiba ya nchi iliyotokana na wananchi.

Katika hali hii "HAKITADUMU CHAMA CHA MAPINDUZI";

Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nimesoma huu uzi mwanzo mwisho na niwashukuru wakuu Mchambuzi na Nguruvi3 kwa uchambuzi wenye nguvu ya hoja. Nitaendelea kuusoma na mimi nitachangia machache.
 
Miezi sita iliyopita ndani ya uzi huu, nilijadili kwamba:
Hatimaye kiini macho cha muungano kinakaribia kukiumbua chama chetu kikongwe cha CCM. Kwa miaka 50 sasa, ccm iliwafanyia wananchi mchezo wa mazingaombwe and managed to get away with it. Lakini kama ambavyo nimekuwa nikisema over and over again, it reaches a to point when – ‘EVEN A MAGICIAN RUNS OUT OF TRICK'. Nikaendelea kujadili kwamba – "the trick" nayozungumzia hapa ni suala zima la mfumo wa muungano wa serikali mbili (sera rasmi ya ccm), mfumo ambao umetawaliwa zaidi na kiini macho (illusion) kuliko ukweli au uhalisia wa mambo.

Kina chama, MwanaDiwani na wenzao kadhaa walitubeza na kutukejeli sana sote ambao tulikuwa na mtazamo huu kwani kwa muda wote walikuwa wamefumbwa na ‘kiini macho' husika. Hakika sasa wanaanza kuona tulimaanisha nini tuliposema ‘they have chosen the wrong side of history', kwani ni dhahiri sasa hata kwa mtoto mdogo wa darasa la tatu kuona kwamba – ‘mazingaombwe ya CCM yamefikia ukingoni'.

Baada ya kuwa vichwa ngumu kwa muda mrefu, sasa CCM haina jinsi bali kukubali kwamba agenda ya katiba mpya haikuwa ni agenda ya chama cha mapinduzi bali ya upinzani. Muhimu zaidi ni kwamba, hata kabla ya upinzani kuja na agenda hii, tayari wananchi wengi walikuwa wameanza kuchoshwa na utawala dhalimu wa CCM, hivyo kuhitaji taifa lianze upya kwa kupitia katiba mpya. Pamoja na CCM kuja na jitihada na mbinu nyingi za kuteka agenda ya katiba mpya, miaka mitatu baadae, CCM wamejikuta hawana jinsi zaidi ya kukubali ukweli kwamba mbinu za chama kuchakachua maoni ya wananchi sasa zimegonga mwamba. CCM sasa inaanza kuzinduka na kubaini kwamba - kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba (2011), wamiliki wa mchakato wa katiba (kwa mujibu wa sheria) ni wananchi, na sio chama cha mapinduzi (CCM).

Wananchi walitoa maoni yao kwa tume, tume ikayakabidhi kwa serikali, lakini CCM ikaja na njama za kuleta rasimu yake ya mafichoni huku makada wa chama pia wakiwakashifu na kuwatukana akina wazee Warioba, kama vile wazee hawa hawakuwa wamewasilisha maoni ya wananchi. UKAWA wakachagua upande wa wananchi, upande sahihi wa historia, lakini kama ilivyo jadi yake, CCM ikaendeleza mbinu ovu, vijembe na vitisho, kwa nia ya kuvuruga matakwa ya wananchi na badala yake kupandikiza matakwa ya chama. Lakini kwa vile UKAWA waliamua kusimamia upande wa wananchi, upande sahihi wa historia - ilikuwa ni suala la muda tu kabla ya mazingaombwe ya CCM kufikia ukingoni.

Makada wa CCM kama kina Mwigulu Nchemba ndio wanaamka sasa hivi wakati tayari kumeshakucha. Ukweli uliopo ni kwamba njama ovu za CCM kuharibu mchakato wa katiba kwa faida ya chama sasa zimegonga mwamba. Na kwa vile mwakani chama kinarudi kwa wananchi kuomba kura, wananchi wale wale ambao walitoa maoni yao, maoni ambayo CCM ilipanga kuchakachua bila ya mafanikio, wananchi ambao uelewa wao juu ya umuhimu wa katiba ya nchi ni mpana kuliko CCM walivyodhania, sasa, CCM haina jinsi bali kusalimu amri. Pamoja na kusalimu amri, tukae tukifahamu kwamba kinachoendelea sasa ndani ya chama ni mbinu na mikakati ya ccm kuhakikisha kwamba the costs and burden ya kukwama kwa mchakato is equally shared, if not more incurred na UKAWA, hasa kuelekea uchaguzi mkuu ujao. Hivyo UKAWA wanahitaji kuwa na umakini wa hali ya juu katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.
CCM ilidhania kwamba ingefanikiwa kuuteka mchakato wa katiba mpya na kuendelea to command ‘legitimacy' ya kutawala nchi bila ya wananchi kujali umuhimu wa "katiba bora", kama ilivyotokea enzi za utawala wa Mwalimu Nyerere. CCM ilisahau kwamba legitimacy ya serikali ya Nyerere, chanzo chake hakikutokana na katiba ya nchi (Katiba ya mwaka 1965 & 1977). Wananchi wa wakati huo hawakujali sana suala la katiba ya nchi, kwani source of legitimacy ya serikali ya CCM chini ya Mwalimu ilitokana na vitu vikuu vitatu:

1.Itikadi ya ujamaa chini ya azimio la arusha.
2.Historia ya TANU na harakati zake za mapambano dhidi ya ukoloni, unyonyaji, ubeberu ndani na nje ya mipaka ya nchi.
3.Uwepo wa a popular, charismatic leader - Mwalimu Nyerere.

All the three sources of legitimacy hapo juu hazipo tena kwani:

*Tukianza na Azimio la Arusha, ni CCM yenyewe ndio iliyozika, tena kimya kimya azimio la arusha kule zanzibar (1992) bila hata ya kushirikisha umma, wanachama wa CCM, na hata Mwalimu Nyerere katika uamuzi huu muhimu.

*Tukija kwenye suala la historia ya TANU – leo hii CCM sio tena Chama cha kutetea wanyonge na wasionacho (wakulima, wafugaji, wafanyakazi) badala yake, leo hii CCM ni chama kinachojali zaidi mafisadi ambao kinawalinda usiku kucha, ccm ni chama cha wenye nacho (tycoons) and their inner circles;

*Na mwisho, kwenye suala la leadership, hakika CCM imeishiwa na viongozi wazalendo na wanaoweka mbele maslahi ya taifa. Na hata wale ambao umma ulikuwa una matumaini nao japo kidogo, mchakato wa Katiba mpya umesaidia sana wananchi kuona kwamba ndani ya CCM, hakuna kiongozi ambae alitetea maoni, ndoto, na matumaini na matarajio yao (kupitia tume ya katiba).

CCM inahitaji kutambua yafuatayo:


  • CCM sasa itambue kwamba umma wa watanzania umeamka. The only source of legitimacy kwa chama chochote cha siasa nchi kuanzia sasa ni suala la "Katiba ya nchi itokanayo na wananchi."



  • Iwapo mchakato wa katiba mpya utaairishwa, wananchi tayari wanafahamu kwamba haitatokana na mapenzi ya CCM, bali taasisi ambazo ziliamua kukaa upande sahihi wa historia – upande wa wananchi – yani vyama vikuu vya upinzani na tume ya warioba. Hivyo ndivyo historia ya nchi itakavyoandikwa.



  • Uchafuzi wa mchakato wa katiba mpya uliofanywa na CCM ambao umegharimu fedha za walipa kodi ilikuwa ni kinyume cha sheria. Na kwa mantiki hii, wahusika wanastahili kushitakiwa kwa kufuja mali ya umma kukaa na kujadili mambo ambayo ni kinyume cha sheria ya mabadiliko ya katiba (2011).


  • CCM itapoteza majimbo mengi sana ya ubunge, hasa maeneo ambayo tume ya katiba ilipita. Mbali ya ubunge, upo pia uwezekano mkubwa wa CCM kupigwa na mshangao kwenye ngazi ya Urais.
 
Tehe tehe tehe!!!!umesema nani tena???N.A.P.E ??????
Niliwahi kusema mahali. Hoja ya Nyerere dhidi ya G55 ilikuwa kwamba serikali tatu si sera ya CCM na mabadiliko katika sera ya CCM hayawezi kuanzia bungeni. Maana G55 walipeleka hoja yao bungeni - Nyerere akasema hapana. Kwa kuwa wote walikuwa wanachama wa CCM wapeleke hoja hiyo kwenye chama kwanza. Ikikubaliwa sera ya CCM ibadilishwe kisha ndio twende bungeni kama chama.

Safari hii mambo ni tofauti. CCM na unafiki wao wamejikuta pabaya. Hawakuwa na sera ya katiba mpya - wala hakuna kikao chochote halali cha CCM kilichopitisha katiba mpya. Ni utashi wa Kikwete - kwamba nataka katiba mpya na basi iwe hivyo. Katika demokrasia ya kweli walipaswa kumzuia Kikwete na hoja yake ya katiba mpya. Wangemweleza unapotaka kuandika katiba mpya kuna suala la muungano - je uko tayari lijadiliwe kwa uwazi? Sasa wamemwacha na walipofikia ni pagumu kweli. Maana serikali mbili ni kama dini. Ukiulizwa maswali magumu huwezi kujibu. Watanzania wa sasa si wale wa wakati wa Nyerere na kibaya zaidi hakuna Nyerere huko CCM leo - eti wanamtegemea Nape kujenga hoja ya serikali mbili.
 
Mkuu Mchambuzi, kwenye huu mjadala wa muungano, mimi niliisha uweka wazi kabisa msimamo wangu hapa
Kama Kweli Nia ya Dhati ni Kuimarisha Muungano, Then, "Twende Kwenye Serikali Moja!.

Pasco

Pasco,
Kamasijakosea wewe unauzoefu sana na zanzibar na wazanzibar jisi navyokumbuka michango yako humu jf. Mimi nashindwa kuelewa kabisa CCM inashindwaje kuwashawishi wazanzibari kukubali serekali moja kwasababu naamini wazanzibar wakawaida wanafaidika na muungano ila tatizo ni wanasiasa wa zanzibari iwe huru iliwaweze kupiga dili kama viongovi wa Tanzania sasa hivi. Ninavyosema wazanzibar wanafaidika nikwasababu moja zanzibar kimaendeleo ipo mbele kuliko sehemu nyingi huku tanganyika na sizani kama zanzibar inamchango mkubwa kiuchumi ukilinganisha na sehemu zilizopo Tanganyika amazo ziku nyuma kimaendeleo. Pili Wazanzibar kama 2/3 wapo tanganyika au wanafaidika kiuchumi na tanganyika. Sasa inakuwaje CCM inashidwa kupitisha hoja ya serekali moja na kuwatumi hao wazanzibar wanao nufaika na tanganyika kwasababu hata kama ni kupiga kura CCM wangekuwa wanazipata kama wangehakikisha hawa wapemba waliolowea tanganyika wanajua kitakacho wapata muungano ukivunji. Hawa wazanzibar wapo wengi huku tananganyika na wanahela kama kinabaharesa ila CCM inawapa kila kitu lakini bado wanawasaliti CCM. naomba kukosolewa kwasababu siijui Zanzibar vizuri ila huu muungano wa chako chetu changu chakwangu niujinga. Msimano wangu ni serekali moja au kilamtu kivyake na wazanzibar waanze kujiandaa kuhama
 
1.Itikadi ya ujamaa chini ya azimio la arusha.
2.Historia ya TANU na harakati zake za mapambano dhidi ya ukoloni, unyonyaji, ubeberu ndani na nje ya mipaka ya nchi.
3.Uwepo wa a popular, charismatic leader - Mwalimu Nyerere.

All the three sources of legitimacy hapo juu hazipo tena kwani:

CCM inahitaji kutambua yafuatayo:


  • CCM sasa itambue kwamba umma wa watanzania umeamka. The only source of legitimacy kwa chama chochote cha siasa nchi kuanzia sasa ni suala la "Katiba ya nchi itokanayo na wananchi."



  • Iwapo mchakato wa katiba mpya utaairishwa, wananchi tayari wanafahamu kwamba haitatokana na mapenzi ya CCM, bali taasisi ambazo ziliamua kukaa upande sahihi wa historia – upande wa wananchi – yani vyama vikuu vya upinzani na tume ya warioba. Hivyo ndivyo historia ya nchi itakavyoandikwa.



  • Uchafuzi wa mchakato wa katiba mpya uliofanywa na CCM ambao umegharimu fedha za walipa kodi ilikuwa ni kinyume cha sheria. Na kwa mantiki hii, wahusika wanastahili kushitakiwa kwa kufuja mali ya umma kukaa na kujadili mambo ambayo ni kinyume cha sheria ya mabadiliko ya katiba (2011).


  • CCM itapoteza majimbo mengi sana ya ubunge, hasa maeneo ambayo tume ya katiba ilipita. Mbali ya ubunge, upo pia uwezekano mkubwa wa CCM kupigwa na mshangao kwenye ngazi ya Urais.

Mchambuzi uko sahihi kabisa kuhusu hili. Nakumbuka kwenye mabadiliko ya mwanzo ya katiba wanazuoni walisema " we have entered in to a market economy and plural politics, the two need a constitution which will support them". Nakumbuka walikuwa ni maprofesa wa chuo kikuu pale mlimani waliokuwa wanasema hivi, na kusisitiza kuwa otherwise mbele ya safari kutakuwa na kizunguzungu. Wanasiasa wetu hasa wa CCM waliwakejeli sana.

Mchakato huu wa katiba kwa sasa umetuonesha wazi kabisa kuwa they were right, they are right and they will be right.
Kwenye bandiko lako umesahau kitu kimoja ambacho kilikuwa kinaifanya CCM iwe na legitimacy...right judgement. Kuna wakati CCM ilikuwa sahihi kwenye kufanya maamuzi na hata kutoa kauli kulingana na hali na maendeleo ya matukio. Lakini sasa naona politics zimedumaza uwezo wa kufikiri wa Chama, na kufanya hata chama kipuuze wataalamu na wale wanaofanya right judgment.

Still, bado sioni 2015 wapinzani wanaweza kupata kura nyingi kwa kuwa CCM mpaka sasa ina uwezo mkubwa wa kuchakachua.
 
Jamhuri ya kiislam ya watu wa Zanzibar then mafuta tele kama Qatar with American military base... hakuna kuvunja muungano ingawaje for a very selfish reason,ile coast imejaa oil kuliko Saudi Arabia


Ndoto za Elinacha
 
mkuu pasco, vipi zanzibar watakubali kupoteza dola yao? Kumbuka wanataka mamlaka kamili, ikipita serikali moja ndoto za wazanzibar kutaka mamlaka kamili zitakuwa zimekufa. Kwao bora serikali 3 au 2. Ila kiukweli serikali 1 ndio suluhisho japo kwa hali halisi ya wazanzibar haiwezekani. Option ya 2 ni serikali 3/shirikisho japo huku sina imani nako.

mMUMECHELEWWAA...... HILI HALIWEZEKANI TENA MAANA ALISHINDWA KAMBARAGE WAKATI ULEE AMBAO NDIO ULIFAA KUFANYA MAAMUZI HAYO (KUIUA SERIKALI YA ZNZ) KUIFANYA ZNZ MKOA. KWA WAKATI HUU CCM ISITHUBUTU TENA ISIFIKIRIE WALA KUTUBUTU KUFANYA UPUMB..AFFUUU HUU. WANANCHI WAMESHAAMKA HIVYO HUWEZI KUWALAZA TENA. MFANO HALISI WA KUFANYA HAYA NI ULEE WA BABU MZEE JULIUS KUMZIMA MZEE ABOUD JUMBE ALIWEZA KUMSHUGHULIKIA LKN KWA WAKATI HUU BABA RIZ HAWEZI NA HATHUBUT KUMGUSA SHEIK KARUME KWA NJIA YOYOTE ILE,
 
Pasco,
Kamasijakosea wewe unauzoefu sana na zanzibar na wazanzibar jisi navyokumbuka michango yako humu jf. Mimi nashindwa kuelewa kabisa CCM inashindwaje kuwashawishi wazanzibari kukubali serekali moja kwasababu naamini wazanzibar wakawaida wanafaidika na muungano ila tatizo ni wanasiasa wa zanzibari iwe huru iliwaweze kupiga dili kama viongovi wa Tanzania sasa hivi. Ninavyosema wazanzibar wanafaidika nikwasababu moja zanzibar kimaendeleo ipo mbele kuliko sehemu nyingi huku tanganyika na sizani kama zanzibar inamchango mkubwa kiuchumi ukilinganisha na sehemu zilizopo Tanganyika amazo ziku nyuma kimaendeleo. Pili Wazanzibar kama 2/3 wapo tanganyika au wanafaidika kiuchumi na tanganyika. Sasa inakuwaje CCM inashidwa kupitisha hoja ya serekali moja na kuwatumi hao wazanzibar wanao nufaika na tanganyika kwasababu hata kama ni kupiga kura CCM wangekuwa wanazipata kama wangehakikisha hawa wapemba waliolowea tanganyika wanajua kitakacho wapata muungano ukivunji. Hawa wazanzibar wapo wengi huku tananganyika na wanahela kama kinabaharesa ila CCM inawapa kila kitu lakini bado wanawasaliti CCM. naomba kukosolewa kwasababu siijui Zanzibar vizuri ila huu muungano wa chako chetu changu chakwangu niujinga. Msimano wangu ni serekali moja au kilamtu kivyake na wazanzibar waanze kujiandaa kuhama

Cc Pasco, Nguruvi3, JokaKuu, Mag3



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi, kwenye huu mjadala wa muungano, mimi niliisha uweka wazi kabisa msimamo wangu hapa
Kama Kweli Nia ya Dhati ni Kuimarisha Muungano, Then, "Twende Kwenye Serikali Moja!.

Pasco

Naunga mkono hoja yako ya serikali moja, ila kuna viongozi wanaojielewa kutupeleka kwenye serikali 1? Je, tuna viongozi wenye uwezo wa kuuwa serikali 3tulizonazo sasa wakati wao wenyewe ni "wasakatonge".

Rai yangu ni kwamba tunahitaji mjadala mpana wa kitaifa utaotawaliwa na fikra za kizalendo na si fikra za ki_UKAWA/kiCCM kama ilivyo sasa. Popote penye wasakatonge weusi bila taasisi makini na zenye mamlaka kamili tusitegemee jipya.

Mungu ibariki Afrika
 
Tatizo kubwa ninaloliona la kupata viongozi wa wabovu wenye maamuzi haya mobuvu ni sisi wenyewew watz haswa tunaojifanya wasomi na kuishi mijini. Tunapuuza kupiga kura na kuhimiza wengine kupiga kura ili kuchagua viongozi sahihi kwa kijafanya tuko bize na tunaishia kuponda na kukashifu na mihadala kibao, sijui na utafiti kuhusu tulipokwama kama taifa. Jaribuni kuangalia wapiga kura wengi ni watu wa vijijini, wamama wa nyumba na wajisiriamali wadogowadogo ambao wengi wanaribuniwa kirahisi na viongozi wabovu kwa rushwa, vitisho nk. Tujiulize ni wasomi wangapi ama matajiri wangapi wanakwenda kupiga kura? Wanaona hawana muda wa kwenda kusimama kwenye maeneo yenye kero za kuchanyikana na jamii eti hawana shida. Matokeo yake viongozi wabovu wakikamata madaraka ni kodi zisizo na tija na hata zikilipwa zinaibiwa, kufujwa nk. Tubadilike jamani kama tunataka nchi yetu iendeshwe tunavyotaka. Tupige kura tuone mtu akichakachua hapo ndio tutaheshimiana, vinginevyo viongozi wabovu wataendelea kubaki madarakani na sisi tutabaki kulalamika tukitegemea maisha bora toka kwa viongozi wabovu wanaoshinda kwa rushwa na wizi wa kura.
 
mMUMECHELEWWAA...... HILI HALIWEZEKANI TENA MAANA ALISHINDWA KAMBARAGE WAKATI ULEE AMBAO NDIO ULIFAA KUFANYA MAAMUZI HAYO (KUIUA SERIKALI YA ZNZ) KUIFANYA ZNZ MKOA. KWA WAKATI HUU CCM ISITHUBUTU TENA ISIFIKIRIE WALA KUTUBUTU KUFANYA UPUMB..AFFUUU HUU. WANANCHI WAMESHAAMKA HIVYO HUWEZI KUWALAZA TENA. MFANO HALISI WA KUFANYA HAYA NI ULEE WA BABU MZEE JULIUS KUMZIMA MZEE ABOUD JUMBE ALIWEZA KUMSHUGHULIKIA LKN KWA WAKATI HUU BABA RIZ HAWEZI NA HATHUBUT KUMGUSA SHEIK KARUME KWA NJIA YOYOTE ILE,
Naunga mkono hoja...hakuna haja ya kulazimisha muungano acha Zanzibar iwe na mamlaka yake 100% kama nchi
 
Hakika mazingaombwe ya CCM yanafikia ukingoni kwa kadri siku zinavyosonga Mbele kuelekea kura ya maoni. Wananchi wengi wanaendelea kujiuliza:

• Iwapo katiba inayopendekezwa inapingwa na tume ya mabadiliko ya katiba ambayo iliundwa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa Mujibu wa Sheria ya mabadiliko ya katiba, uhalali wa katiba hii unatokana na nini?

•iwapo katiba inayopendekezwa imepitishwa kwa kura za hila na kila aina ya uharamu, uhalali wa katiba hii unatokana na nini?

• suala la gharama za serikali Tatu - inakuwaje katiba ya Chenge inapendekeza kofia Saba za urais, na wabunge 400, Wakati CCM Ndio ilikuwa Mstari wa Mbele Kupinga serikali Tatu Kwamba zitakuwa ni mzigo kwa wananchi? Kipi nafuu kwa walipa kodi, kofia Saba za urais au chache zaidi Kama zilivyo kwenye rasimu ya tume ya jaji warioba? Kipi nafuu zaidi Kati ya idadi ya wabunge na mawaziri ndani ya rasimu ya tume na idadi hiyo kwa Mujibu wa rasimu ya Chenge?

Na maswali mengine kem kem.

Kwanza kuna suala la takwimu. CCM ilikuwa Mstari wa Mbele kupotosha juu ya takwimu za wananchi waliotoa maoni Yao Mbele ya tume ya jaji warioba, takwimu ambazo ushahidi wake upo ingawa serikali imeifunga tovuti ya tume kuzuia wananchi wasiongee takwimu hizo. Kwa CCM, takwimu za tume ni haramu, lakini kwa CCM hiyo hiyo, takwimu za wafugaji, wachuuzi, wafuga nyuki walioitwa na Sitta Dodoma ambapo Sitta Kinyume na Sheria, akajigeuza kuwa tume ya mabadiliko ya Katika na Kuanza kuchukua maoni nje ya utaratibu, kwa CCM, takwimu hizi ni halali. Kwa CCM, takwimu za kura za Facebook, gmail, Instagram, fax, wagonjwa mahututi vitandani kupitisha katiba iliyopendekezwa, kura hizi ni halali. Kwa CCM, wapiga kura kwenda kulala usiku wakiwa wajumbe wa upande mmoja wa muungano, na kesho yake Kuamka na kuwa wajumbe wa upande mwingine wa muungano, takwimu ya kura hizi ni halali. Kwa CCM, takwimu ambazo hadi Leo zinaendelea kuwekwa sawa kima hesabu licha ya bunge la katiba kumalizika, kwa lengo la kuhalalisha upitishaji wa katiba haramu, takwimu hizi ni halali kwa CCM.

Kwa CCM, muungano wa vyama vya siasa kutetea katiba ya wananchi yani UKAWA, muungano huu ni haramu, lakini muungano wa CCM kupitisha katiba ya haramu, UDP, UPDP, TLP, muungano huo ni halali kwa Mwamvuli wa TCD.

Zanzibar ilifanya mabadiliko yake makubwa kikatiba mwaka 2010 na kuna dalili zote kuwa hatua hii Ndio ilifanya serikali ya CCM kutangaza mchakato wa katiba mpya kuepuka Aibu ambayo ingetokana na mgongano wa kikatiba baina ya katiba ya JMT 1977 na katiba ya Zanzibar 2010. Katiba ya Chenge na Sitta inalazimisha kufutwa kwa mambo mengi ndani ya katiba ya Zanzibar 2010, suala ambalo ni miujiza tu Ndio itakayofanikisha Hilo. Hii ni kwa sababu:

Wazanzibari waliporidhia kutambuliwa Kama nchi ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka 2010, hawakuwa na Malengo ya kuja kufuta uamuzi huo miaka minne baadae 2014. Hata hivyo, kwa Mujibu wa katiba ya Zanzibar 2010, ili Jambo lolote kubadilishwa, ni lazima kwanza kura ya maoni ipigwe na kupitisha uamuzi huo kwa Robo Tatu ya kura. Kwa upande wa rasimu ya Chenge, katiba hii itapita iwapo itapita kwa 50.01% ya kura kutoka pande Mbili za muungano. Huu ni mgongano mkubwa sana na utapelekea machafuko muda sio mrefu.

Katiba ya Zanzibar mwaka 2010 imempa rais wa Zanzibar mamlaka ya kuigawa nchi ya Zanzibar kwa mipaka ya mikoa, Wilaya na wadi. Zanzibar haikufanya maamuzi haya ili miaka minne baadae waje kuyafuta. Lakini katiba ya Chenge na Sitta inataka Zanzibar wayafute haya ili kurudisha mamlaka ya kuigawa Zanzibar kimamlaka yawe chini ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Hayo Ndio CCM inataka yafanyike, suala ambalo ni miujiza tu Ndio itafanikisha.

Mwaka 2010, kikatiba Zanzibar waliidhinisha kuipatia Mahakama ya Zanzibar hadhi ya kufanya maamuzi yasiyopingika na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, Kama vile masuala yaliyoamuliwa na Mahakama ya kadhi. Katiba ya Sitta na Chenge inataka Zanzibar wageuze hili. Hii ni miujiza.

Kwa katiba ya Chenge, Mahakama ya Zanzibar italazimika kurudi Kule Kule nyuma badala ya kubakia na mamlaka ya kusikiliza na kuamua masuala yanayohusu katiba ya Zanzibar ambayo kwa Mujibu wa mabadiliko ya kumi, yalikuwa hayafikishwi kwenye Mahakama ya Rufaa ya Tanzania. Kwa Mujibu wa katiba ya Zanzibar, maamuzi yanatolewa na Majaji watatu, halafu Majaji watano, basi, hakuna kitachopelekwa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania. CCM inataka badilisha haya kupitia rasimu ya Chenge. Hii ni miujiza.

Mkataba wa muungano wa 1964 ulibainisha Kwamba rais wa Zanzibar awe ni makamu wa kwanza wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, lakini Rasimu ya Chenge na Sitta imefuta Hilo.

Mazingaombwe ya CCM yanaelekea tamati, na Anguko Hilo litaanzia Zanzibar. Tukumbuke Kwamba muungano uliopo ni baina ya TANU na ASP ambao baadae ukaja halalishwa kwa lazima sababu tu nchi ilikuwa ni ya chama kimoja. Lakini kwa vile huu ulikuwa ni uchakachuaji kwani mkataba wa muungano hautaji vyama vya siasa, ikachukua miaka 12 Kabla ya jamhuri mpya ya muungano wa Tanzania Kupata katiba yake ya kwanza Kama jamhuri mpya. Hata hivyo, katiba hiyo upatikanaji wake ulikuwa ni sawa tu na ule wa katiba ya Tanganyika (1962) kwani haikutokana na wananchi Bali Kamati ya chama cha TANU. Tume ya jaji warioba ikawapatia wananchi fursa ya Mara ya kwanza kuandika katiba Yao, lakini fursa hiyo imeporwa na CCM ambapo katiba inayopendekezwa ni Ile Ile ya mwaka 1977 ambayo moyo wake ni Mfumo wa serikali Mbili, na Mfumo wa chama kimoja cha siasa.

Tanzania bado inaendeshwa na Mfumo wa chama kimoja, Mfumo wa vyama Vingi unaendelea kuwa ni nadharia tu. Ushahidi wa hili ni jinsi mchakato wa katiba mpya ulivyotekwa na kuvurugwa na CCM.

Awali tulisema Kwamba "even a magician runs out of tricks." Haya yanajidhihirisha sasa, macho na masikio yetu yapo kwenye siasa za Zanzibar. Mengi yatajitokeza hivi karibuni. Lakini muhimu ni Kwamba, Historia itakuja andika Kwamba muungano uliletwa na TANU na ASP na Ukavunjwa na CCM.

Cc Buchanan, Mtanganyika, chama, MwanaDiwani, Kobello, Mag3, Bongolander, ZeMarcopolo, Pasco, zomba, Nguruvi3, King Suleiman, Barubaru, Mkandara.





Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi kwa maoni yangu suala la katiba tayari tumechemnsha. Sidhani kama kuna njia nyingine yoyote mbeleni ambaye inaweza kubadilisha makosa ya sasa. Makosa yamefanywa na wakubwa kwa makusudi. I am very skeptikal kuwa kura za maoni zitapigwa na kuikataa.

Inawezekana kabisa kuwa watu wanaweza kupiga kura ya kukataa, lakini given ujuzi wa uchakachuaji uliopo sidhani kama litakuwa tatizo kwenye uchakachuaji. Besides that, mwamko wa watu si mkubwa kivile kwenye kutaka katiba mbaya.

Anything can happen, lakini kwa Zanzibar naona tayari kuna ugumu kwenye kuikubali katiba. Huko ndio suala la legitimacy lita-translate kwenye upigaji kura, but still there are ways of bypassing them.

The best we can do now ni kuwaelimisha watu kuwa katiba ni mbaya hainajazingatia maslahi mkaubwa muhimu ya Tanganyika, imepakwa sukari ya mambo mengine mazuri mazuri ambayo NGO zilikuwa zinayataka, lakini yale makuu yenye maslahi ya mtanganyika yamewekwa pembeni. If we do that kuna uwezekano wa kuizuia.

But again, kama yote yatashindikana, naona in 10 years from now we will be back to the same exercise again. Siku hizi watu wanaendelea kuamka.
 
Hakika mazingaombwe ya CCM yanafikia ukingoni kwa kadri siku zinavyosonga Mbele kuelekea kura ya maoni. Wananchi wengi wanaendelea kujiuliza:

• Iwapo katiba inayopendekezwa inapingwa na tume ya mabadiliko ya katiba ambayo iliundwa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa Mujibu wa Sheria ya mabadiliko ya katiba, uhalali wa katiba hii unatokana na nini?

•iwapo katiba inayopendekezwa imepitishwa kwa kura za hila na kila aina ya uharamu, uhalali wa katiba hii unatokana na nini?

• suala la gharama za serikali Tatu - inakuwaje katiba ya Chenge inapendekeza kofia Saba za urais, na wabunge 400, Wakati CCM Ndio ilikuwa Mstari wa Mbele Kupinga serikali Tatu Kwamba zitakuwa ni mzigo kwa wananchi? Kipi nafuu kwa walipa kodi, kofia Saba za urais au chache zaidi Kama zilivyo kwenye rasimu ya tume ya jaji warioba? Kipi nafuu zaidi Kati ya idadi ya wabunge na mawaziri ndani ya rasimu ya tume na idadi hiyo kwa Mujibu wa rasimu ya Chenge?

Na maswali mengine kem kem.
Kwa ujumla, hoja yako inatatanisha kwa sababu unatetea tume ya mabadiliko ya katiba. Hicho ni chombo cha rais (executive) na bunge ni chombo kinachowakilisha wananchi (ingawa nakubaliana na wewe kuwa composition yake could've been better).

Uzuri ni kuwa kuna referendum. Katiba inapata uhalali wake kutoka kwa WANANCHI. Siyo tume .... na sijaona ukiwatetea wananchi kwa kusisitiza subira.

Kuhusu marais saba ..... you know what you are doin' na bora niache kwa sababu nadhani upo kazini na inabidi niheshimu kazi.
 
Back
Top Bottom