Ndugu wanabodi,
Leo hii nitazungumza yangu moyoni na kwa Uwazi pasipo kuuma maneno maana naona watu wengi tunapiga kelele pasipo hata kujua tunataka nini isipokuwa ni reaction tu baada ya kuona hali ni tete kama vile mfa maji. Tatizo kubwa la Wadanganyika wengi ni kutojua maana hivyo wanadai katiba mpya pasipo hata kuisoma wala kuijua katiba iliyopo inasema nini na ina makosa gani ambayo ndio sababu haswa ya kutakiwa katiba mpya.
Ni jambo la kushangaza sana tunapoitaka katiba mpya wakati hatujui katiba iliyopo imesema nini pinzani na hali halisi tuitakayo. na ndivyo hivyo hivyo katika swala la Muungano. Watu wengi wanadai serikali 1 (unitary state) au 3 (Federation) lakini hawajui huu muungano wa serikali mbili asili yake nini na kwa minajiri ipi umeundwa isipokuwa tu tumefika mahala tunasema koti likikubana sana unalivua! hii ndio sababu nayoiona mimi na hakuna jingine.
Mchambuzi, Ukimsoma vizuri Nassoro Moyo anaeleza kwa umakini Muungano wetu na jinsi ulivyotungwa kwa kuelezea machungwa matatu ktk vikapu viwili, ni muungano pekee ambao kwa kidhungu unaitwa POLITICAL UNION na imefanyika hivyo kwa sababu maalum. Na kama mliwahi kumsoma mwalimu Nyerere alisema wazi kabisa kwamba Afrika haiwezi kuungana moja kwa moja na kuunda nchi moja ni lazima tuanzae kwa stages akitofautiana na Nkurumah aloitaka Afrika moja. Na ili Muungano huu mdogo uweze kudumu mawazo yote haya tunayoyaziungumzia leo yaliwekwa ubaoni na wakachukua lilokuwa bora zaidi nalo ni serikali 2. na hakika inatimizia miaka 50 pasipo kuvunjika muungano kuvunjika wakati nchi zilizochukua mfumo wa serikali 3 zimevunjika zote.
Inasikitisha sana leo sisi tunafikiria kufanya mabadiliko ya muungano huo kwa sababu tu ya kero za wahaini ambao kisheria walitakiwa kutiwa ndani wasionekane kabisa. Tazameni yanayotokea huko Ukraine ambako wana Muungano wa ushirikiano wa kiuchumi kama ilivyo EU au EAC na sasa Russia inataka kuchukua hatua kutokana na makubaliano yalounda katiba yao ktk kuulinda muungano wao.
Na hata Ukizungumzia Marekani, UK au nchi zote ziloungana,swala la kuvunja muungano uliopo ni UHAINI na kutamka tu kuuvunja muungano huo ni kosa kubwa ambalo pengine kuhumu yake ni kifo. Na muungano hauwezi kuwa altered na unilateral decision of either party, states or the federal political body. Sasa unakuja Tanzania ambapo rais, mawaziri, wabunge na wanasiasa wote wameapa kabla ya kushika madaraka kuwa wataulinda Muungano wetu, leo wamekuwa na kiburi cha ku question hata Muungano wenyewe ili kuandika katiba mpya! Hivi kile kiapo walichochukua kilikuwa Usanii na inakuwaje bado wanapotaka mabaidiliko haya bado wamesima akama wabunge au wanachama wa CCM, CDM au CUF!
Binafsi yangu, naihitaji katiba mpya kwa sababu iliyopo haijitoshelezi. Ni katiba ilopitwa na wakati baada ya Tanzania kuodnoka ktk mfumo wa Kijamaa na kuingia Ubepari. Katiba mpya ilitakiwa toka mwaka 1993 ili kukidhi hali halisi ya dunia ya leo ktk maswala ya mawasiliano, Kiuchumi na Kijamii tofauti kabisa na kuliweka swala la Muungano ndani ya katiba hii.
Na hata hivyo Muungano unaweza tu kubadilishwa kwa kufanya referendum na sio vikao vya wanasiasa na wateule ambao wote sio wawakilishi wa wananchi wote ktk swala hilo. Hivyo kama kweli utaratibu wa kuvunja muungano inabidi ifanyike referendum kwa Wazanzibar na ifanyike pia kwa Tanganyika maana kwanza tunatofautiana sana kifikra. Zanzibar kulingana na CUF wao hawataki kuwa ktk muungano wowote iwe serikali 1, 2 au 3 wanachotaka ni Zanzibar yenye mamlaka kamili na kiti chake UN (Uhaini) na Bara nao kwa sababu tu ya madai ya kero za Wazanzibar wanataka muungano uwepo lakini iwe kwa serikali 3, jambo ambalo hayati mwalimu Nyerere alikwisha lizungumzia sana.
Hivyo basi ni Ujinga mkubwa kuendelea kuzungumzia muungano wakati nchi mbili zote wananchi wake wanataka muungano tofauti. Wazanzibar sio wajinga hawataweza kabisa kukubaliana na serikali 1 ama 3, kwa sababu wanajua wanafaidika na kuwepo kwa serikali 2, isipokuwa kutokana na mfumo wa utawala unaoendeshwa leo haifungamani na hali halisi ya mageuzi ktk mfumo wa kiuchumi tulochukua (ubepari) Wazanzibar wanaona ni kheri wajikate.
Nasi huku bara pia kwa sababu hizo hizo za kikatiba kuendelea kutukuza Ujamaa ktk hali ya Kibepari tunapendekeza serikali 3 ili kuondokana na kadhia ya koti hili linalotubana. Hivyo hapa kinachofanyika ni kukomoana, kama wewe waujua huu basi mimi naujua huu. hii sio busara wala hekima hata kidogo bali ni ujinga unaotokana na kutoelewa maana.
Mwisho nitasema tu ya kwamba katiba mpya haitapatikana nahata kama ikija patikana haitakuwa muarobaini wa matatizo ama kero zetu isipokuwa tutazidi kuwa ktk umaskini. Katiba mpya ingelenga tu mabadiliko ya kiuchumi ambapo wananchi wote tungeweza kuwa na mamlaka ya kuhodhi mali na ardhi (utajirisho), Uraia, serikali kusimamia tu nguzo za kiuchumi badala ya kufanya biashara, mfumo wa ukusanyaji wa kodi, na jinsi gani Zanzibar inaweza kufaidika na mikopo inayotoka nje kwa ajili ya ujenzi wa Tanzania.
Katiba ya nchi haitungwi na wanasiasa wala makundi ya watu wanaodai haki zao bali hutungwa na intellectuals. watu wenye elimu na uelewe, mental capacity ya kuelewa katiba ni msahafu/biblia ya jamii tunayoishi na sii tuitakayo. Katiba inayolinda maslahi ya wananchi wote pasipo ubaguzi na sii mapendekezo ya kila kundi la kijamii.. Na kwa jinsi tulivyoanza na makundi na sii wanataaluma nina hakika mwsho wake utakuwa mbaya sana - Kwa leo inatosha
Mtayakumbuka maneno yangu.