- Kaka unanikumbusha sana maneno ya Jana kuna Mbunge mmoja wa bunge la Katiba alisema "kuna watu humu bungeni wandhani wao tu ndio wanajua na kwamba wao tu ndio wamesoma wengine wote hatujui kitu, ukweli ni kwamba Uingereza haina wala haijawahi kuwa na Katiba", I mean the way you writte ni kama vile wengine wote humu JF ni wajinga wajinga flani hivi ni wewe tu ndio mwenye akili humu ndani na waht you say ndio final truth, ukweli ni kwamba una hasira sana na CCM na kwa muda mrefu sana lakini mpaka leo hakuna utabiri wowote uliowahi kuutoa ukawa kweli, umetabiria mabaya CCM kwa muda mrefu sana lakini never happened hata mara moja na here you are as usual na mahasira yako na mautabiri ya waganga wa kienyeji,
- I mean kaka Nassoro Moyo ndiye peke yake aliyebaki kati ya walioanzisha Muungano? Kama alikuwa na tatizo na Muungano kwa nini hakusema Muasisi wake Mwalimu alipokuwa hai? Nassoro Moyo ana nafasi gani ya uzito wa kisiasa Visiwani sasa hivi? He is nobody, sasa kuandika post based on what Nassoro Moyo said baada ya kuukubali Muungano kwa robo tatu ya maisha yake na kujaribu kuubeza now unasema huyo ndio anatakiwa kuwa the final say ya Muungano uwepo au usiwepo? Really?
- Kwenye Criminology nilifundishwa mtu anayejiamini na kujua anachokisema huwa hataji majina ya wengine kwenye hoja zake, sasa wewe tizama watu wote uliowataja na kuwatumia copy ya hii post yako I mean una wasi wasi wa nini kama unajua na kuamini ulichoandika ni sawa sawa, why Mwanakiijiji hivi ni kweli unaamini Mwanakijiji hataki Muungano kama wewe?,
- Eti CCM ilikuwa inawadanganya wananchi kwa miaka 50? na wewe ulikuwa wapi miaka yote hiyo kuwaelimisha wananchi kwamba CCM inawadanganya? I mean wanaodai Serikali tatu wanatumia akili zao ila wale wote wanaodai Serikali mbili wametumwa na CCM? Really kweli an academician unaweza kusimama na kundika low arguments kama hizi?
- Kaka mimi ni muumini wa Serikali Mbili tu, siamini in Serikali tatu kwa sababu kwanza Dunia nzima hakuna Taifa lenye Serikali Tatu, pili Muungano uliua Serikali za Tanganyika na Zanzibar na kuunda Serikali ya Tanzania ndiyo ninayoitaka na kuiamini na ndio ninaisimamia na nitaisimamia mpaka mwisho, sijatumwa na CCM na wala wewe siamini kuwa umetumwa na WApinzani, jamani acheni kujipa madaraka ya kuwakilisha wananchi na huku hamjachaguliwa kuwawakilishia mawazo yao, kila mwananchi wa Tanzania ana haki ya kutoa mawazo yake, wewe mawazo yako ni kuvunja Muungano that is all ungetoa hoja on that line badala ya kujipachika madaraka ambayo ya kuwaongelea wananchi kwa hoja weak kama ulizotoa, kwa kutumia maneno ya Kiongozi ambaye wala hana nafasi yoyote kubwa kwenye siasa za Taifa wapo wanaomzidi wengi sana na bado hawawezi kuongelea wananchi wengine,
- Kaka nasikia kutapika sana ninapoona unakichafua CCM kwa kujifanya na wewe ni CCM na huku unajua wazi kwamba wewe sio CCM ila ni muumini wa kuona CCM inavurugika kitu ambacho hakitakuja kutokea, umetoa utabiri wako wa waganga wa kienyeji kwa muda mrefu sana kuhusu matatizo ndani ya CCM lakini ndio kwanza CCM ipo vizuri na imeshinda Viti 23 vya Udiwani na huku unaowatetea wamepata viti 3 pamoja na helikopta zote walizotumia, kaka si wanasema shetani akiwa mzee anakuwa malaika maana toka uanze na utabiri wako against CCM haujawahi kutoa hata mara moja badilika kaka!!
Le Mutuz
Karibu katika mjadala. Hoja kuhusu uanachama wangu wa CCM nilishakujibu kwenye mjadala wetu mwingine, ule wako wa juzi uliouanzisha kumshambulia Lowassa.
Hoja yako nyingine inayahoji nilikuwa wapi miako 50 iliyopita, leo ndio naona sera ya ccm ni tatizo ni kwamba - kwanza umri wangu ni mdogo sana kulinganisha na wako, sitashangaa kama umenipita kwa miaka karibia 20 kiumri, hivyo mimi bado ni mchanga katika kuelewa siasa za nchi hii, hasa our political history, na katika uelewa wangu kadri siku zinavyozidi kwenda mbele, mtazamo wangu ndio huu ambao nimekuwa nauwasilisha, yote nikilenga kuachana na unafiki na badala yake kukosoa chama kwa mambo ambayo inayalinda kwa sababu za kijinga. Lakini muhimu pia ni kwamba, awamu za nyuma, hasa ile ya mwalimu, wananchi wengi walikuwa na imani na ccm na serikali yake na kuipa uhalali kwa vyanzo nje ya Katiba ya nchi, na hili nimejadili kwa kirefu awali (azimio la arusha, historia na mafanikio ya TANU kutetea wanyonge ndani na nje ya nchi, na uwepo wa nyerere as a charismatic leader). Haya ndio yaliipa ccm na serikali yake legitimacy, hence the union or zanzibar question na muundo wa muungano kwa ujumla kuweka kukaa under the carpet kwa muda. Leo hizi three sources of legitimacy hazipo tena, na njia pekee ya ccm kupata legitimacy sustainable na sio ya hila hila na ujanja ujana ni kwa kuhakikisha nchi inapata katiba inayotokana na matakwa ya wananchi, na vyama vyote including ccm kuheshimu katiba itakayopatikana kwa vitendo.
Hapo juu, hoja yako muhimu in my humble view ni ile kwamba United Kingdom doesn't have a written constitution, na naposema ina umuhimu ni kwa maana moja tu nayo ni kwamba, baadhi ya makada wa ccm wanajaribu kutetea muungano kwa hoja kwamba ni kitu almost like "ordained", na sio kwa mujibu wa matakwa ya binadamu/wananchi, matakwa yaliyokuwa expressed kwa mujibu wa written constitution iliyotokana na wananchi.
Ni hivi:
Ni kweli our former colonial ruler, the british hawana a written constitution. Taifa hili lina certain constitutional conventions ambazo zimeendelezwa historically kwa kipindi kirefu sana. Na hakuna mtawala yoyote wa uingereza ambae atathubutu kuzi breach hizi conventions. Kwa ufupi, hizi conventions derive their binding character kutoka kwenye political practice ya muda mrefu sanan hivyo zimepata historical legitimacy na sio legitimacy based on any legal document. Je, unataka kutuambia kwamba muungano wetu should be treated kwa mtindo huu wa uingereza? By the way, rais wa zanzibar, Dr. Shein ameshasema nakala ya mkataba wa muungano (1964) ipo ikulu ya znz, so hoja ya kufananisha unwritten constitution ya uingereza na suala la muungano goes straight to the trash bin. Nadhani unaelewa kwamba the legal foundation of our union ni mkataba wa muungano (1964.
Nirudi tena kwenye mfano wa Uingereza, taifa ambalo mwalimu alitueleza in the 1960s kwamba tumeiga our unitary union kutoka mfumo wao (bearing in mind kwamba baada ya mfumo wa chamma kimoja kufa, jaji bomano akapewa jukumu la kutafuta ufumbuzi kwani kwa unitary approach, ccm ingeshinda "bara" na cuf zanzibar uchaguzi wa 1995 and pengine chaguzi zilizofuatia). Jaji bomani akaja na wazo la mgombea mwenza kwa kuiga "federal system" ya USA. Mind you, we moved from unitary to federal elements za muungano (na mkataba wa muungano ambao ccm breached it from the get go had proposed a federal structure).
Kinadharia, bunge la uingereza linaweza kutunga sheria ambayo ita breach the constitutional conventions ambazo zipo katika taifa hilo kama nilivyojadili hapo juu. Kwa maana hii, bunge la uingereza isn't only a sovereign entity but also supreme.
Tuzidi kuingia kwenye hoja:
Now while uingereza haina a written constitution, makoloni yake yote yalipewa katiba iliyotoka lancaster hall london, katiba ambazo "zilikuwa enacted na bunge la uingereza"; kwa maana hii, katiba yetu ya kwanza siku ya uhuru ilipata its legal authority na validity kutoka kwa mkoloni. Kilichofuata baadae ni TANU na serikali yake kufanyia marekebisho katiba ile na kuipatia TANGANYIKA katiba yake mpya mwaka 1962. Tukiamua kufuatilia legal gene ya katiba yetu hata ya sasa, ujue tu kwamba haitatuchukua muda mrefu kubaini kwamba imetokana na an ordinary law iliyopitishwa na bunge la uingereza (in writting ingawa taifa husika lina unwritten constitution), tupo pamoja mpaka hapo?
Kwahiyo basi katiba ya sasa ya JMT (ambayo hata hivyo ccm imewaachia zanzibar waifutilie mbali), mizizi ya katiba hii ni written laws passed by bunge la uingereza. Nani alitunga katiba ya 1977? Bunge la katiba la chama kimoja, huku almost 55% ya wajumbe wake wakiwa sio wale kutoka majimboni bali kwenye dawati la rais ikulu. Nani alimpa rais wa jmt mamlaka ya kuteua bunge la katiba 1977? Ni mkataba wa muungano wa 1964, mkataba ambao inasemekana ulipitishwa na wabunge wa BLW na Tanganyika (kutoka vyama viwili vya tanu na asp pekee). Kumbuka, 1964 bado kulikuwa na mfumo wa vyama vingi kama vile vya zuberi mtemvu n.k. Kwahiyo kimsingi legal foundation ya muungano wetu kama anavyojadili shivji ni ule mkataba wa muungano (1964), na kwa vile mkataba huu ukaja chakachuliwa, matokeo yake ni kero za muungano kwa miaka 50 kero ambazo nape anatumabia sasa dawa itapatikana chini ya mfumo ule ule wa serikali mbili ndani ya muungano ambao umevunjwa na katiba ya ya znz (2010). Lakini kwa vile mnatanguliza matumbo kuliko ubongo, badala ya kuwekana vikao kujadili kwanini ccm imeruhusu hili, mnakaa kumjadili warioba.
Tanganyika yetu inarudi na sijui utajificha wapi uso wako utakaojaa aibu. Nasubiri kusikia mchango wako kwa hoja zangu bandiko
#2 ,
#37 na
#38 .
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums