Mtazamo wangu: Awali neno Chawa lilionekana kama "nitakua na Wewe popote ulipo"
Kutokana na kutokuwa na uwezo mzuri wa kufikiri na kuona mbali, watu hawa hawakufikiria kwamba IPO siku watu watauliza kazi na madhara hasa ya Chawa ni yapi!
Ni kama walipoanzisha Make Tanzania Great Again wakiiga kule America ya bwana Trump! Wasijue kwamba watanzania watafupisha na kuiita MATAGA ambayo kimsingi ilileta tafsiri basi na wao kuamua kulikataa jina la MATAGA mpaka likapotea kimya kimya. Ni nadra sana kumkuta kada na kumwita MATAGA akafurahia.
Kwa kuwa wenzetu wamekuwa wavivu wa kufikiri na kuchukua kila alisemalo mkubwa, kumbukeni Kuna wakati Mwenyekiti aliwahutubia UVCCM akawaambia waache uchawa haufai na wao wakauacha! Juzi wakati wa hitimisho la maridhiano Ile kauli ya mwenyekiti "Chawa wangu watakuvaa" ikawatoa Shimoni mithili ya panya na wakaamua kuirasimisha kabisa!
Hii kitu ikitumiwa vizuri na wapinzani wa ccm kupata political milage inawezekana kabisa hasa kwa kutumia maana halisi ya mdudu Chawa Pamoja a sifa na athari zake kwa binadamu!
Ni dhahiri kwamba itafanikisha kuonesha uhalisia wa maisha na muendelezo wa kujengeka kwa matabaka katika Jamii! Kwamba Chawa ndio wanaofaidi matunda ya nchi hii kwa kuinyonya huku watu wasafi wakiendelea kutaabika kwa ugumu wa maisha katika nyanja zote kiuchumi na kijamii!
Rais anabeba identity ya nchi! Hivyo anavyozidi kuwa na Chawa wengi na rate ya nchi kunyonywa inaongezeka. Rejea kula kwa urefu wa kamba, tunaitafsiri kwamba chawa wanyonge kadri wanavyo weza ila wasiumizane Matokeo yake ni nchi kudhoofika kiafya (kiuchumi na kijamii) huku Chawa wakizidi kuneemeka na kunenepa!
Ni jambo la kawaida mmeona sasa serikali (Rais) anakopa kwa Nia njema TU ya kufufua uchumi na kuboresha hali ya maisha ya watanzania kijamii (elimu, afya, maji, umeme) lakini wanaoteuliwa kusimamia fedha hizo ni waliojitanabaisha kuwa ni machawa hivyo huishia kuzitafuna na hatuoni hatua zote juu Yao (fumigation) na hivyo' deni la Taifa linakua na linaakisi kupanda kwa gahrama za maisha (mfumuko wa Bei) na kuumiza wasio machawa.
Ilikua ni Rai ya mheshimwa Mwenyekiti kukataa Katu Katu kuwa na Chawa ambao wanajirasimisha tena kupitia majengo ya umma na kuamua kuwa Rais wa watanzania wote na kuwateua watu kusimamia rasilimali za nchi hii kwa kujali uwezo wao na usafi wao badala ya machawa ambao hata inflation kwao ni karata pia ya kusifia!
Kuhusu Makamanda Hilo Sina wasi wasi nalo sana mana linaakisi hali halisi ya maisha ambayo inahitaji mapambano na mapambano yanahitaji Makamanda ambao wako Tayari kufia vitani Ili nchi ikombolewe. Tatizo linakuja kwenye practicability ya huo ukamanda! Inabaki kwenye keyboard au ni kwenda field au ni kutumia platforms mbali Mbali media na makongamano kuendeleza mapambano?
Kumbuka vita hii sio ya silaha ni vita ya hoja nzito zinazohitaji majibu na utekelezaji kwa wenye mamlaka!
Usisahau Michele kg 1= 3500
Nyama kg 1= 12000
Maharagwe kg 1= 4000
Vocha ya buku = 1200
Vyote hivi havitoki Russia Wala Ukraine
Dominika Njema