KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, jana alifichua ufisadi mkubwa uliofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kuingiza magari 200 aina ya Land Cruiser ‘mkonga' bila ya kulipia sh milioni 600 za ushuru wa forodha kwa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).
Hiki kiwango cha ushuru ambacho kinatakiwa kulipwa si sahihi kwa magari 200. Estimate ya Hardtop mpya ni kama $48,000 hivi. Weka import duty ya 25%, VAT 18% na Excise duty ya 10% jumla ya kodi kwa gari moja ni $29,880. Kwa gari 200 ni whopping $5,976,000 sawa na Tshs 8 Billion!!!