CCM na magari ya uchaguzi...


Hiki kiwango cha ushuru ambacho kinatakiwa kulipwa si sahihi kwa magari 200. Estimate ya Hardtop mpya ni kama $48,000 hivi. Weka import duty ya 25%, VAT 18% na Excise duty ya 10% jumla ya kodi kwa gari moja ni $29,880. Kwa gari 200 ni whopping $5,976,000 sawa na Tshs 8 Billion!!!
 
Nadhani hesabu sio sahihi.Toyota L/C mkong moja all duties inclusive ni karibu US$71,000 ama TAS 92,000,000 na ushuru na kodi zingine peke yake ni karibu TAS 30,000,000 kwa gari, kwa hivo magari 200 itakuwa TAS 6,000,000,000 na sio TAS 600,000,000....I hope this is typo error by the editor...or informer of Mzee Slaa...
 

Ndg nimeambiwa bei ya gari moja la mkonga pale Toyota (T) ni Shs 65m kabla ya ushuru na kodi nyingine. Gharama ya hayo magari 200 kwa hiyo bei hapo juu ni sawa na Shs 13 billion. Je, hizi ni sawa na shule ngapi za msingi/sekondari? Je, fedha hiyo yaweza kusomesha wanafunzi wangapi chuo kikuu? Ama yaweza kuhudumia walimu wangapi wa shule za msingi na sekondari?
Tunahitaji neema, mambo si mambo ndani ya nchi hii
 
msamaha ni kwa sisiemu tu...
Wengine lieni hamna chenu
Pole sana nchi inaendeshwa kwa sheria na taratibu na sio kama duka la Muhindi, ikumbukwe kwamba ccm ni chama tu kama vyama vingine hivyo inapaswa kufuata sheria pia. Mkuki kwa nguruwe, itajatokea ccm ikawa kanu. Ni vyema ikajizoeza fair play kwani wakumbuke kuna leo na kesho who knows?
 
Kwani umeambiwa pesa imetoka CCM??? AU Serikalini??? pengine chama kimepata ufadhili. Hii ni changamoto kwa vyama pinzani je wataweza kushindana na hawa??? kama wenzetu wanakosa hata vibendera vya kupeperusha!!!!

Kwa kuwa CCM ni chama cha kisiasa kilichokabidhiwa ridhaa na watu kuongoza serikali, wanaowajibu kueleza umma vyanzo vya mapato hayo. Kwa hili kama wamekomba ndani ya serikali au wamepata kwa wauza unga; walitakiwa kulipia kodi.
Kwa kuwa Roma haikujengwa siku moja, hakika kuna siku wananchi watajitolea kuvifadhili vyama shindani ili kuleta ushindani uliomathubuti ktk kuendesha taifa hili.
 
ni vizuri sana kufikiria mambo ya maendeleo kama ujenzi wa mashule, hospital, maji, umeme wa uhakika, n.k. kama tungekuwa na vision ya taifa na utekelezaji wake usingetegemea chama wala utashi wa raisi. Lakini kwa vile tuna watawala haiwezekani kufika huko kwani wenyewe wanapenda waendelee kututawala kihalari au kifisadi , haijalishi kwamba wanaua au wanawapa wananchi shida na tabu nyingi katika utawala wao, ndo maana utasikia hawalipi kodi, wanafisadi hapa na pale ilimradi azima yao ifanikiwe milele. watawala wa CCM ya sasa ndo hao ninaowaongelea wako radhi tule nyasi ili ndege ya raisi inunuliwe hivyo sitashangaa wakikwepa kodi.

Zaidoi ya hapo sisi je wananchi tunafanya nini pindi tunapopata taarifa kama hizi? tunakaa tukisubiria wapalestistina wapigwe na waisrael ndo tuandamane? hasahasa wanafunzi wa vyuo vikuu mambo ya jamii yetu hayawahusu ila buoooom usiguse. ni lini tutakapoanza kuanzisha mijadala na kuomba kutumia nguvu ya uma kushinda?
 
Kwa hali ilivyo sasa, nina uhakika mkubwa kabisa kwamba CCM haiwezi kufanya upuuzi huo... ila tusubiri tuone
 

Hata mimi nimeshtukia hiyo hesabu. Hata kama ni used cars kodi bado iko chini sana. Kwa hesabu wanazotupa ni kwamba kila gari linalipiwa 3 000 000 (Three million) tu kitu ambacho hakiwezekani kwa viwango vya kodi za TZ.

May be wamedanganya ili aseme halafu baadaye walipe 600 million. Si unajuwa washatuona waTZ wote mazezeta tu. Anything is possble.
 
Siku zote huyu bwana anaposema huwa mnarudi kusema kuwa ni PR na kukanusha lakini mwisho wa siku huthibitika kuwa ni kweli.
Hii ni tahadhali kwamba magari hayo yasitoke bila kulipiwa ushuru. Full stop.
 
ni vema kusema kabla hayajatoka ili kuhakikisha kuwa kodi inalipwa. Slaa amefanya kinachoitwa whistle blowing. Sasa taifa zima litazingatia kuona kuwa kodi halali inalipwa ili magari haya yaingie na vinginevyo yasiingie
 
Siku zote huyu bwana anaposema huwa mnarudi kusema kuwa ni PR na kukanusha lakini mwisho wa siku huthibitika kuwa ni kweli.
Hii ni tahadhali kwamba magari hayo yasitoke bila kulipiwa ushuru. Full stop.

mimi napenda viongozi kama Slaa, siyo kiongozi anayesubiri kitu kifanyike ndiyo aje,NO kabla akijafanyika unazuia! safi sana Slaa.
 
What do you want to tell us Mr. Invisible?

kama CCM wangelipa hizo pesa zingeweza kusaidia wananchi kibao wanaotegemewa kuadhirika kwa njaa kwa sababu ya kulikupata mavuno ya kutosha msimu huu.......................!!!!!!

Kwani tatizo lako liko wapi??? Huna uchungu na hizo 600 million/Billion???
 

Kwa maelezo yako kuna mambo 2
Ama unamtumikia kafiri mradi wako ambao ni mkono uende kinywani ama uelewa wako ni mdogo huoni kwa kuwa umevaa miwani ya chuma na akili unayo ila mawazo mgando .Slaa anataka umaarufu ili awe nani ?
Kama kuna magari kweli bandarini basi kuna ukweli wa zengwe la kodi . Wanao toa habari wanajua nini kinacho endelea . Bora kusema magari yako hapo kuliko kusema baadaye ambako hata traces za ushahidi zitakuwa nimesha fichwa .

Ionee Tanzania huruma usibishe kila kitu hata kama ni kwa njia hii ndiyo unapata mkate wako .
 


Unafikiri mpaka sasa hawapandikiza watu wao humu??? Subiri 2010 ndiyo wataongezeka na wao wenyewe watakuja na majina bandia kama sisi kuconfuse situation.
 
Fortunately, Slaa yuko juu ya petty politics za hawa kina Albano. Alipotaja orodha ya mafisadi tuliona walivyohaha kila mmoja kwa wakati wake akijaribu kumtisha kuwa anakwenda mahakamani na hakuna aliyethubutu.

Hata alipoibua EPA bungeni alibezwa sana na Spika wa bunge lakini leo wengi tunaheshimu kazi yake.
 

Umenena. Na badala yake baadhi yao ndiyo wamefikishwa mahakamani, hasa Mgonja ambaye alitishia sana kushitaki.

Kuhusu haya magari: Aliyeyaleta ni Subhash Patel -- fisadi aliyetajwa na Slaa na swahiba mkubwa wa JK. Viongozi wengi katika CCM hawajui hili. CCM watakatiwa magari machache na mengine yatauzwa na Subhash bila ya ushuru. Huo ndiyo ulikuwa mpango ambao Slaa kauvuruga.
 
Kusubiri yatolewe kwanza bila kulipiwa na taifa kuibiwa ndio unadhani ni uzalendo? Slaa kafanya ambacho wengi hatufanyi. Unaona uhalifu unataka kutendeka unakaa kimya kusubiri ushahidi. Then?
 
Good Slaa for the whistle blown; but wajumbe hamna mwenye data kw undani; hii ni habari mhimu sana; badala ya CCM kushughulikia kushuka kwa uchumi; njaa; mabadiliko; viwanda vya ndani; madini; ufisadi kama watawala ndio kwanza wananunua magari ya kuzungukia akina mabwana wao; this country bwana is very poor; an i dont know why it is poor -JK
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…