CCM na Serikali jibuni hoja za Humphrey Polepole, msimzime kidola

CCM na Serikali jibuni hoja za Humphrey Polepole, msimzime kidola

Haya ya ilani na mengineyo tusiyaegemee sana kwasababu Katiba yetu inampa Rais husika madaraka makubwa, anaweza akaitupa pembeni ilani ya mwenzake at any time akatengeneza yake japo alikuwa makamu wake wa Rais, naona hapa muhimu iangaliwe zaidi sheria inasema nini.
Ni kweli ndani ya chama ilani inaweza tupiliwa mbali kama ilivyotupiliwa mbali utaratibu wa kugombea nafasi ya urais Kutoka kwa wanachama wa ccm na hakuna mbobezi aliyejitokeza kupinga mahakamani
 
Kwa nini asiruhusiwe kugombea vipindi viwili wakati bado hajaanza kutumikia hata kipindi cha kwanza cha awamu yake ?!
Utata wa hili unaletwa na fact kuwa huu urais wake utakuwa ni miaka 4 na miezi kama 8 hivi, so ni almost miaka 5, lakini mfano JPM angefariki mwaka march 2025, ina maana urais wa aliyerithi ungekuwa wa miezi 7 kabla ya uchaguzi mkuu, so angeweza kugombea kwa vipindi viwili hapo. So hapa shida inaletwa na katiba. Yaani katiba haikugusia urefu wa kipindi cha mrithi urais na kitahesabiwa vipi.

When winning two elections does not equate to two terms in office​

Following the untimely death of former President Michael Sata while in office, President Lungu assumed office to complete his term – after winning a presidential by-election – from the 25 of January 2015 to the 13 of September 2016. In 2016, President Lungu was then re-elected to serve a full term of 5 years in office. From this context, one would naturally deduce that Lungu has twice been elected to the office of president.

In addition to this, Article 106(3) of the 2016 constitution of Zambia asserts that “A person who has twice held office as President is not eligible for election as president”. This can be interpreted to mean a person who holds the office of president in Zambia for two terms is no longer eligible for re-election for a third term. Again, this seems to rule Lungu out.

However, this all depends on exactly how one defines a “presidential term”.
 
CCM NA SERIKALI JIBUNI HOJA ZA POLEPOLE, MSIMZIME KIDOLA.

Na Yericko Nyerere

Kinga uliyonayo ni kwa muda tu, hakuna kinga ya kudumu, Hata Job Ndugai na wenzake kinga walizojiwekea kipindi walipokuwa kwenye dibwi la kuvunja haki za watu na kuvunja Katiba ya Tanzania, ina muda mfupi sana wataanza kutoa nachozi ya samaki soon. Hivi ndivyo wahenga husema, Kinga ya kirais aliyokuwa nayo Humphrey Polepole katika ule utawala dharimu imeisha, ni kinga hiyohiyo ndio alikuwa nayo Paul Makonda, Sabaya, Chalamila, Mnyeti, Odunga na wahuni wengine wengi.

Tulishaisikia na kuona milio ya maumivu ya Sabaya, huku Paul Makonda akianza kuwambwa kisawasawa na kuandaliwa makazi mapya Segerea. Naam miliyo ya maumivu ya Polepole tumeanza kuisikia vizuri sana, Bahati mbaya kwetu sisi milio hiyo sio migeni, Tulishalia sana, Tulishazika ndugu zetu wengu, Tulishafungwa jela sana na tulishafanyiwa madhila mengi, Polepole akiwa ni moja ya magenge makuu ya uhalifu huo nchini. Lakini tulishavuka viwango hivyo vya mateso, na Sasa tuna wajibu wa kumtetea yoyote anayeonewa.

Serikali inawajibu wa kujibu hoja za Polepole badala ya kutumia vyombo vyake vya dola kumnyamazisha, Hoja za Polepole ni nzito na zina maslahi kwa umma wa Watanzania, zijibiwe kwa hoja na sio vinginevyo. Uhuru wa Polepole usipokwe kwa njia zilezile tulizopitishwa sisi. Yale madhila yaishie kwetu, tuzuie yasiendelee kwa wengine. Polepole ajibibiwe.

Hoja ya Polepole kwamba hii ni Awamu ya Tano itakayokamilika 2025 na sio ya Sita ni hoja ya muhimu sana kwa umma, Kwasababu kwa muda mrefu serikali hii iliyojichagua kinguvu 2020 kukamilisha awamu ya tano ya miaka 10, imekuwa ikijitambulisha kwamba ni serikali ya awamu ya sita. Jambo ambalo kimantiki si kweli. Ni wajibu wa serikali itoke imjibu Polepole, badala yake inamjibu kwa kutumia machineries zilezile ilizotumia kwetu.

CCM na Serikali yake kwa miaka mingi ikishindwa kujibu hoja kinzani, imekuwa ikiagiza Vyombo vya "dola" kama Polisi, TRA, TCRA, Uhamiaji, TAKUKURU, MAHAKAMA nk, kuzima hoja za wapinzani, na kwa miaka mitano iliyopita vimetumika kwakiwango cha kutisha kuumiza Watanzania wengi sana hususani Wanachadema wengi hadi leo wako waliokufa (Alfonce Mawazo), wako walipotea (Ben Saanane na Azory), wako vilema (Lissu), wako walioko jela (Mbowe), na wako waliofilisiwa (Mbowe na wengine), wako wanaohangaika mahakamani kila siku (Wanachadema kila kona ya Tanzania. Msingi wa haya yote ni ccm na serikali yao kushindwa kujibu hoja zao.

Hatuna shida na Polepole kusulubiwa kwa mechanism zilezile zilizotusurubu sisi, Msulubuni Polepole kama Polepole kwa makosa mengine hata yake ya kijinga ya Vieitii, sio kwa hizi hoja zake, hoja zake jibuni kwa hoja, Hoja zake ni hoja zetu pia, Hoja zake zina maslahi kwa umma. Tunakemea na kuzitaka mamlaka zirudi kwenye mstari, Leo Polepole analilia uhuru wa kutoa maoni ambao yeye akiwa madarakani aliupora kwa wengine, Noo tunaka Polepole awe huru tena huru kabisa.

Ni Polepole huyu huyu na CCM yao walichota pesa ya Umma na wakaongoza genge la kupora uhuru wa Watu kuwa wanachama wa chama chochote wakipendacho, wakawatishia na kuwapatia pesa na ahadi lukiki za kimadaraka ili wahame vyama vyao walivyovipenda, ni Polepole huyu huyu alikuwa na lugha chafu sana kwa wanaccm wenzake waliokuwa na maoni tofauti ndani ya Chama kumbuka matusi yake ya nguoni kwa Paul Makonda alipoanza kuonyesha nia ya kugombea ubunge Kigamboni.

Hayo yote hayawezi kuwa sababu tuache kusikiliza na kujadili hoja zake, Tumpuuze Polepole, lakini tuzichukue hoja zake tuzichambue, tuzitake mamlaka ya dola na chama chake wazijibu hoja zake. Tutakuwa wajinga kama hatutaitaka serikali ijibu hoja za Polepole na badala yake tukaacha Polepole asulubiwa kama tulivyofanyiwa sisi, Kitendo cha kuitaka serikali ijibu na ikijibu, tutatukuwa tumefanikiwa kufunga njia ya mateso kwa Watanzania wengine kesho.

Tunaposimama kudai Katiba mpya tuna maana pana zaidi na moja ya mambo muhimu ni kama haya katiba itazuia vyombo vya dola kutumika kisiasa, Leo Mwenyekiti wetu amebambikiwa kesi ya Ugaidi kisa anadai katiba mpya, Hilo haliwezi kuwa mwisho wa madai ya umma kuhusu katiba mpya. Mwachieni Mbowe, jibuni hoja zake.

View attachment 2041229
View attachment 2041233
Duh !!
 
Mimi naomba nikubaliane na wewe, kwamba hii anamalizia awamu ya 5, halafu 2025 ndio anaanza term ya kwanza ya awamu ya 6, kwahiyo anapiga miaka 14 safi bin muruwa.

Hii inaitwa ukimpiga teke chura ndio kwaanza unamuongezea mwendo.

Maana yake ukikaa nshale, ukisimama nshale, utachaguwa mwenyewe kusuka au kunyowa.
Tukikubaliana hivyo ni sawa kabisa . Ila ndani ya chama itabidi mchakato wa kutafuta mgombea Urais ufanyike . Kama ataamua na yeye kuchukua fomu sawa. Kila mwanachama atakuwa na haki sawa kuomba dhamana hiyo.
 
Tukikubaliana hivyo ni sawa kabisa . Ila ndani ya chama itabidi mchakato wa kutafuta mgombea Urais ufanyike . Kama ataamua na yeye kuchukua fomu sawa. Kila mwanachama atakuwa na haki sawa kuomba dhamana hiyo.
Tangu lini mwenyekiti wa ccm anapambanishwa na mtu?

Kwa taarifa yako CCM baada ya Mungu ni mwenyekiti.

Unajuwa ni kwa nini Membe amefutwa uanachama?
 
Kweli akili za celebrity forum haziwezi kufit sehemu zote.

Ni vizuri mkawa mnasubiria hoja mserereko mlizozoea kabla ya kuandika mada zilizowapita uwezo kiakili.
Mama ni rais anayemalizia serikali ya awamu ya 5.
ili asiitwe rais wa awamu ya 6.
akishamaliza hii 5.
atagombea Tena 5.alafu mitano Tena.
Ina maana ataongoza miaka 15.
ili aongoze miaka 10.
tunatakiwa tukubali hii ni awamu ya 6.
 
Kinga ya kirais aliyokuwa nayo Humphrey Polepole katika ule utawala dharimu imeisha, ni kinga hiyohiyo ndio alikuwa nayo Paul Makonda, Sabaya, Chalamila, Mnyeti, Odunga na wahuni wengine wengi.
Nimepitia kauli za kihuni wakati Magufuli akitukana watu. Nimeelewa sasa hawa wahuni ni legacy ya HAYAWANI.
 
Back
Top Bottom