The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,541
Awamu ya 5 au ya 6 is not an issue...Safi, umetengeneza foundation nzuri, Katiba iliyopo inaweka madarakani serikali husika, na Katiba hiyo hiyo inatoa maelezo nini kitatokea endapo Rais aliyepo madarakani ataondoka ofisini either kwa kufariki, kuugua, au vinginevyo.
Moreover, Katiba ikasema, kama Rais aliyepo madarakani hatamaliza muhula wake, ni yule atakayekuwa makamu wa Rais ndie atamalizia muda uliobaki, sasa hapa tunazungumza kisheria, sio habari za Zanzibar au popote pengine.
Ndipo unapoona hoja ya Polepole ilivyo na nguvu, huyu mtu anaonekana ameshachungulia mahala akapata majibu, na wala sio kusema tu CCM walijiwekea utaratibu wa kutoka awamu moja kwenda nyingine bila kuandikwa popote, wanasahau Katiba kama sheria mama inatoa majibu ya hayo yote.
Watake wasitake, Samia kisheria anamalizia muda uliobaki wa awamu ya tano, kama akitaka kugombea tena 2025 ndio ataianza awamu ya sita, hii ni sheria inavyosema sio kelele.
Ishu hapa ni watu hususani watawala kukosa hekima na ustaarabu wa kushindana na kujibizana kwa hoja badala ya kutumia ujambazi ktk kukabiliana na mpinzani wako kihoja...
Andiko la Yericko Nyerere liko very clear. Hamtetei Polepole bali anakemea watawala wanajitetea kwa kuwaumiza wapinzani wao kwa hoja kosoaji wanazozitoa dhidi yao serikali...