CCM na Serikali jibuni hoja za Humphrey Polepole, msimzime kidola

CCM na Serikali jibuni hoja za Humphrey Polepole, msimzime kidola

Haya ya ilani na mengineyo tusiyaegemee sana kwasababu Katiba yetu inampa Rais husika madaraka makubwa, anaweza akaitupa pembeni ilani ya mwenzake at any time akatengeneza yake japo alikuwa makamu wake wa Rais, naona hapa muhimu iangaliwe zaidi sheria inasema nini.
Exactly kama ambavyo watangulizi wake, tukimnukuu Nappe, walivyoweza kufanya mengi ambayo hayakuwa kwenye ilani mfano :kuhamia Dodoma, ujenzi wa UDOM, bwawa la Nyerere, mchakato wa Katiba mpya etc...
 
CCM NA SERIKALI JIBUNI HOJA ZA POLEPOLE, MSIMZIME KIDOLA.

Na Yericko Nyerere

Kinga uliyonayo ni kwa muda tu, hakuna kinga ya kudumu, Hata Job Ndugai na wenzake kinga walizojiwekea kipindi walipokuwa kwenye dibwi la kuvunja haki za watu na kuvunja Katiba ya Tanzania, ina muda mfupi sana wataanza kutoa nachozi ya samaki soon...
Wacha panda arushe mateke, kiroboto ni mdudu kadogo sana
 
Wapi katika imetamka neno Awamu? Weka icho kipengele
Hakuna scenario yoyote ambayo itamuondoa Rais aliyepo madarakani na kumuweka mwingine kama haipo kikatiba, na hizo sababu zipo iwe, kifo, ugonjwa (kutokutimiza majukumu yake) n.k

Kila awamu inakuwa na Rais ana makamu wake, Samia alikuwa ni makamu wa Rais wa serikali ya awamu ya tano, Magufuli akiwa ndie Rais, hawa walikuwa timu moja ya awamu moja, kwasababu ya kifo Magufuli akampisha Samia anamalizia muda uliobaki.

Katiba imetamka neno term, na hii term ndio alikuwepo Magufuli kama kiongozi na Samia kama msaidizi, huwezi kuifuta hii term kwasababu tu Magufuli alifariki wakati msaidizi wake bado anaiendeleza, ndio maana nae husema "kazi iendelee" kazi ipi hiyo? ya awamu ya tano.

Usiishi kwa kukariri makosa ya mazoea yaliyofanywa na CCM huko Zanzibar, tafuta vitu vingine uone vinasema nini kuhusu hili suala, kwamba CCM wanalitumia neno "awamu" pale wanapobadilisha sura ya aliyepo madarakani, hili ni batili kwasababu halipo kisheria.
 
Hakuna scenario yoyote ambayo itamuondoa Rais aliyepo madarakani na kumuweka mwingine kama haipo kikatiba, na hizo sababu zipo iwe, kifo, ugonjwa (kutokutimiza majukumu yake) n.k..
Acha kuzunguka! Ni kipengele kipi cha katiba kimetamka neno Awamu?

Ilo kosa linapatikana kichwani kwako na kwa Polepole na sio kwenye Katiba?

Nyie ni wapuuzi na washamba tu
 
Karudi kusoma katiba katika hiki kipingele
Article 40 (2) inasema; No person shall be elected more than twice to hold office.

Hapa maana yake ni kwamba; hiki kipindi alichopo Samia kama Rais sasa hivi hakuchaguliwa na wananchi kwa kura (elected), ila akianza chake anaweza kuchaguliwa mara mbili kwa kupigiwa kura na wananchi.

Hapa tena naona kuna maneno mawili yanakuja kwenye kichwa changu.

- Appointed: ambapo hapa ndipo Samia aliposimama kama Rais wa JMT kwa wakati huu.

- Elected: Hapa ni pale atakapopigiwa kura na wananchi kuwa Rais wa JMT.
 
Acha kuzunguka! Ni kipengele kipi cha katiba kimetamka neno Awamu?

Ilo kosa linapatikana kichwani kwako na kwa Polepole na sio kwenye Katiba?

Nyie ni wapuuzi na washamba tu
Kumbe wewe ni mjinga tu ulieamua kuendelea kuishi kwenye tope la fikra huku ukiwatisha watu na polisi wenu, Polepole anapenda sana kuwahangaisha mazuzu wa sampuli yako, endelea kuimba mapambio ya Samia.
 
Acha maneno! Wewe na polepole nileteeni kifungu cha Katiba kinachotamka nano Awamu.

Kuna Milioni mbili hapa kwa kila mmoja wenu
 
Polepole for presidency
[emoji3581][emoji3581][emoji3581]
 
Article 40 (2) inasema; No person shall be elected more than twice to hold office.

Hapa maana yake ni kwamba; hiki kipindi alichopo Samia kama Rais sasa hivi hakuchaguliwa na wananchi kwa kura (elected), ila akianza chake anaweza kuchaguliwa mara mbili kwa kupigiwa kura na wananchi.

Hapa tena naona kuna maneno mawili yanakuja kwenye kichwa changu.

- Appointed: ambapo hapa ndipo Samia aliposimama kama Rais wa JMT kwa wakati huu.

- Elected: Hapa ni pale atakapopigiwa kura na wananchi kuwa Rais wa JMT.
Mataga wakisikia anaweza kuongoza hadi 2035 itakuwa mtafaruku mkubwa sana
Kiturilo Crimea jingalao YEHODAYA
 
Hakuna scenario yoyote ambayo itamuondoa Rais aliyepo madarakani na kumuweka mwingine kama haipo kikatiba, na hizo sababu zipo iwe, kifo, ugonjwa (kutokutimiza majukumu yake) n.k

Kila awamu inakuwa na Rais ana makamu wake, Samia alikuwa ni makamu wa Rais wa serikali ya awamu ya tano, Magufuli akiwa ndie Rais, hawa walikuwa timu moja ya awamu moja, kwasababu ya kifo Magufuli akampisha Samia anamalizia muda uliobaki.

Katiba imetamka neno term, na hii term ndio alikuwepo Magufuli kama kiongozi na Samia kama msaidizi, huwezi kuifuta hii term kwasababu tu Magufuli alifariki wakati msaidizi wake bado anaiendeleza, ndio maana nae husema "kazi iendelee" kazi ipi hiyo? ya awamu ya tano.

Usiishi kwa kukariri makosa ya mazoea yaliyofanywa na CCM huko Zanzibar, tafuta vitu vingine uone vinasema nini kuhusu hili suala, kwamba CCM wanalitumia neno "awamu" pale wanapobadilisha sura ya aliyepo madarakani, hili ni batili kwasababu halipo kisheria.
Mimi naomba nikubaliane na wewe, kwamba hii anamalizia awamu ya 5, halafu 2025 ndio anaanza term ya kwanza ya awamu ya 6, kwahiyo anapiga miaka 14 safi bin muruwa.

Hii inaitwa ukimpiga teke chura ndio kwaanza unamuongezea mwendo.

Maana yake ukikaa nshale, ukisimama nshale, utachaguwa mwenyewe kusuka au kunyowa.
 
Iyo tafsiri ya Awamu umeitoa wapi?

ZANZIBAR kuna Awamu ya 8 saivi Polepole amewai kuwa hadi mwenezi wa CCM ulimsikia wapi akihoji hayo?

Mwambie Polepole kuna matokeo ya kumdharau Amiri Jeshi Mkuu.

Kama anataka kuyapata Safari hii atayapata!
Atayapata ma Nini? Na huo ndio udhaifu wenu vitisho wakati mnapaswa kumjibu tu.
Mlishafirisika hoja muda Sana.
 
Hangaya anataka aonekane kwamba kipindi alichopo ni kipindi cha kwanza cha awamu ya sita, ili apate justification ya kugombea kipindi cha pili, wakati basically kipindi tulichopo ni kipindi cha pili cha awamu ya tano, na kwa kuwa walijinadi wote na Magu ukomo wake ni 2025, ambapo mchakato mpya wa kuwapata wagombea kwenye vyama kwa ajili awamu ya sita ya urais utafanyika.......tuwe waungwana tuache janja janja...
 
CCM NA SERIKALI JIBUNI HOJA ZA POLEPOLE, MSIMZIME KIDOLA.

Na Yericko Nyerere

Kinga uliyonayo ni kwa muda tu, hakuna kinga ya kudumu, Hata Job Ndugai na wenzake kinga walizojiwekea kipindi walipokuwa kwenye dibwi la kuvunja haki za watu na kuvunja Katiba ya Tanzania, ina muda mfupi sana wataanza kutoa nachozi ya samaki soon. Hivi ndivyo wahenga husema, Kinga ya kirais aliyokuwa nayo Humphrey Polepole katika ule utawala dharimu imeisha, ni kinga hiyohiyo ndio alikuwa nayo Paul Makonda, Sabaya, Chalamila, Mnyeti, Odunga na wahuni wengine wengi.

Tulishaisikia na kuona milio ya maumivu ya Sabaya, huku Paul Makonda akianza kuwambwa kisawasawa na kuandaliwa makazi mapya Segerea. Naam miliyo ya maumivu ya Polepole tumeanza kuisikia vizuri sana, Bahati mbaya kwetu sisi milio hiyo sio migeni, Tulishalia sana, Tulishazika ndugu zetu wengu, Tulishafungwa jela sana na tulishafanyiwa madhila mengi, Polepole akiwa ni moja ya magenge makuu ya uhalifu huo nchini. Lakini tulishavuka viwango hivyo vya mateso, na Sasa tuna wajibu wa kumtetea yoyote anayeonewa.

Serikali inawajibu wa kujibu hoja za Polepole badala ya kutumia vyombo vyake vya dola kumnyamazisha, Hoja za Polepole ni nzito na zina maslahi kwa umma wa Watanzania, zijibiwe kwa hoja na sio vinginevyo. Uhuru wa Polepole usipokwe kwa njia zilezile tulizopitishwa sisi. Yale madhila yaishie kwetu, tuzuie yasiendelee kwa wengine. Polepole ajibibiwe.

Hoja ya Polepole kwamba hii ni Awamu ya Tano itakayokamilika 2025 na sio ya Sita ni hoja ya muhimu sana kwa umma, Kwasababu kwa muda mrefu serikali hii iliyojichagua kinguvu 2020 kukamilisha awamu ya tano ya miaka 10, imekuwa ikijitambulisha kwamba ni serikali ya awamu ya sita. Jambo ambalo kimantiki si kweli. Ni wajibu wa serikali itoke imjibu Polepole, badala yake inamjibu kwa kutumia machineries zilezile ilizotumia kwetu.

CCM na Serikali yake kwa miaka mingi ikishindwa kujibu hoja kinzani, imekuwa ikiagiza Vyombo vya "dola" kama Polisi, TRA, TCRA, Uhamiaji, TAKUKURU, MAHAKAMA nk, kuzima hoja za wapinzani, na kwa miaka mitano iliyopita vimetumika kwakiwango cha kutisha kuumiza Watanzania wengi sana hususani Wanachadema wengi hadi leo wako waliokufa (Alfonce Mawazo), wako walipotea (Ben Saanane na Azory), wako vilema (Lissu), wako walioko jela (Mbowe), na wako waliofilisiwa (Mbowe na wengine), wako wanaohangaika mahakamani kila siku (Wanachadema kila kona ya Tanzania. Msingi wa haya yote ni ccm na serikali yao kushindwa kujibu hoja zao.

Hatuna shida na Polepole kusulubiwa kwa mechanism zilezile zilizotusurubu sisi, Msulubuni Polepole kama Polepole kwa makosa mengine hata yake ya kijinga ya Vieitii, sio kwa hizi hoja zake, hoja zake jibuni kwa hoja, Hoja zake ni hoja zetu pia, Hoja zake zina maslahi kwa umma. Tunakemea na kuzitaka mamlaka zirudi kwenye mstari, Leo Polepole analilia uhuru wa kutoa maoni ambao yeye akiwa madarakani aliupora kwa wengine, Noo tunaka Polepole awe huru tena huru kabisa.

Ni Polepole huyu huyu na CCM yao walichota pesa ya Umma na wakaongoza genge la kupora uhuru wa Watu kuwa wanachama wa chama chochote wakipendacho, wakawatishia na kuwapatia pesa na ahadi lukiki za kimadaraka ili wahame vyama vyao walivyovipenda, ni Polepole huyu huyu alikuwa na lugha chafu sana kwa wanaccm wenzake waliokuwa na maoni tofauti ndani ya Chama kumbuka matusi yake ya nguoni kwa Paul Makonda alipoanza kuonyesha nia ya kugombea ubunge Kigamboni.

Hayo yote hayawezi kuwa sababu tuache kusikiliza na kujadili hoja zake, Tumpuuze Polepole, lakini tuzichukue hoja zake tuzichambue, tuzitake mamlaka ya dola na chama chake wazijibu hoja zake. Tutakuwa wajinga kama hatutaitaka serikali ijibu hoja za Polepole na badala yake tukaacha Polepole asulubiwa kama tulivyofanyiwa sisi, Kitendo cha kuitaka serikali ijibu na ikijibu, tutatukuwa tumefanikiwa kufunga njia ya mateso kwa Watanzania wengine kesho.

Tunaposimama kudai Katiba mpya tuna maana pana zaidi na moja ya mambo muhimu ni kama haya katiba itazuia vyombo vya dola kutumika kisiasa, Leo Mwenyekiti wetu amebambikiwa kesi ya Ugaidi kisa anadai katiba mpya, Hilo haliwezi kuwa mwisho wa madai ya umma kuhusu katiba mpya. Mwachieni Mbowe, jibuni hoja zake.

View attachment 2041229
View attachment 2041233
🤔🤔🤔 Lkn mkuu yericko tang lini hawa jamaa wakajibu hoja kwa hoja? Hata kipind slow slow akila cake ya Taifa ndo ilikua mbaya zaid toa hoja inapingwa kwa kuteswa au kutekwa, over!!
 
Safi, umetengeneza foundation nzuri, Katiba iliyopo inaweka madarakani serikali husika, na Katiba hiyo hiyo inatoa maelezo nini kitatokea endapo Rais aliyepo madarakani ataondoka ofisini either kwa kufariki, kuugua, au vinginevyo.

Moreover, Katiba ikasema, kama Rais aliyepo madarakani hatamaliza muhula wake, ni yule atakayekuwa makamu wa Rais ndie atamalizia muda uliobaki, sasa hapa tunazungumza kisheria, sio habari za Zanzibar au popote pengine.

Ndipo unapoona hoja ya Polepole ilivyo na nguvu, huyu mtu anaonekana ameshachungulia mahala akapata majibu, na wala sio kusema tu CCM walijiwekea utaratibu wa kutoka awamu moja kwenda nyingine bila kuandikwa popote, wanasahau Katiba kama sheria mama inatoa majibu ya hayo yote.

Watake wasitake, Samia kisheria anamalizia muda uliobaki wa awamu ya tano, kama akitaka kugombea tena 2025 ndio ataianza awamu ya sita, hii ni sheria inavyosema sio kelele.
nimekuelewa sana ila naomba ufafanuzi, iwapo Samia atagombea je mchakato wa kupitisha jina la mgombea(akiwemo Samia)utapitia mchujo wa kumpambanisha na wana ccm wengine na akipita inamaana awamu yake ndiyoinaanza hapo that means anapiga miaka 10 +na hii ya Magufuli anatawala 15yrs? kwa kupitia hoja yako
 
Back
Top Bottom