Hili jambo la awamu halipo kikatiba na nilishasema hapa, lipo kimazoea zaidi, muhula wa rais unahesabiwa kwa anaeingia madarakani ( rais wa ngapi). Hata akirawala miezi minne, ilimradi ameshika ueais kikatiba ( iwe kwa kura au kuchukua nafasi iliyoachwa wazi kikatiba).
Na sijawahi kusikia au kuona popote pale kuna jambo limekwama au halijatekelezwa kisa mgongano wa neno mhula.
Kuna vitu inabidi tujadili na vichukue muda wetu lakini sio hili la muhula.
Na hata kama hatupendi au hatukurarajia, kwa katiba hii, huyu ndio rais.
Hapa kama kuna mambo ya kuangaziwa, iwe katiba na hivyo vipengere kwamba ikitokea rais aliyeko madarakani ameacha nafasi kwa sababu yeyote ile, utaratibu ubadilike. Ila kwa hii katiba tuliyonayo, hoja ya mihula haina uzito.