CCM nambari wani

CCM nambari wani

natabiri , wewe ni mtoto wa KIONGOZI .

CCM imenifanyia mambo mengi mema katika maisha yangu mpaka hapa nilipofikia naishukuru sana ndio maana popote niendapo lazima nibebe city viwili bible na kadi yangu ya ccm
 
asante sana mkuu kwa jibu kuntu na muruwa sana , hivyo ndivyo wanavyofaidi watoto wa viongozi ambao utafiti unaonyesha kwamba hawazid hata laki 3 ! Bali mamilioni ya wananchi wanateseka sana kama ulivyojionea kwenye uzi huu .
 
CCM walianza na ngonjera ya ‘Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania’. Baada ya kuimba ngonjera hii kwa muda wa miaka 5 na kukosa muitikiaji, wakaamua kubalili mapigo na kuibuka na ngonjera mpya waliyoipa jina la ‘Ari mpya, Nguvu mpya na Kasi mpya’ (ANGUKA). Pamoja na usanii huu wote, maisha ya mtanzania yamezidi kuwa duni mwaka nenda mwaka rudi!

View attachment 175945 View attachment 175951 View attachment 175957

Tangu CCM washike madaraka nchi imekuwa haina mwelekeo. CCM inafanana na mtu mwenye jino moja. Mtu kama huyo hata umlishe namna gani hawezi kunenepa. Lazima atakufa kwa njaa kwa kuwa hana meno ya kutafunia chakula.

View attachment 175940

Nchi hii imejaliwa rasilimali nyingi za asili kama vile ardhi, maziwa , bahari na mito, madini, misitu, wanyama, nk. Lakini kwa kuwa CCM haina meno, imewaalika wenye meno (wawekezaji) waje watafune (wakavune) rasilimali hizo huku wakiiacha nchi ikiwa ikiwa tupu! Migogoro katika maeneo ya uchimbaji madini na maeneo yenye ardhi ya rutuba imekuwa ikitokea kila kukicha. Wananchi wamenyanganywa ardhi yao nzuri wamepewa ‘wawekezaji’. Watanzania wanyonge wamegeuka wakimbizi ndani ya nchi yao. Wananchi wamekata tamaa na utawala wa CCM. Hawana hamu nayo!

View attachment 175946 View attachment 175953

Huduma za jamii kama vile maji, umeme, barabara, elimu na afya imekuwa duni kiasi cha kukatisha tamaa. Wanafunzi kusomea chini ya miti ni suala la kawaida kabisa na wale wachache waliobahatika kupata kupata madarasa duni huketi chini ya sakafu ya vumbi au juu ya matofali! Hali hii mpaka lini hasa? CCM wala hawajali kwa kuwa watoto wao husomeshwa kwenye shule nzuri zenye walimu weledi na vifaa vya kufundishia vinavyotosheleza mahitaji.

View attachment 175947View attachment 175948 View attachment 175950 View attachment 175955 View attachment 175956

Mwalimu Nyerere alipokea uongozi wa nchi kutoka kwa wakoloni wakati nchi ikiwa taabani kiuchumi lakini hatukuwahi kushuhudia ugumu wa maisha kama tunavyoshuhudia hivi sasa. Ni lini hasa CCM na mafisadi wake wataboresha huduma za jamii na kuwafanya wananchi waishi maisha yenye utu?

CCM haina tofauti na mtu mzima aliyekabidhiwa kumlea mtoto mdogo badala yake akanywa maziwa ya mtoto na kumuacha mtoto akifa kwa njaa.

View attachment 175944

Hii maana yake ni kwamba CCM imeamimiwa na wananchi wakaikabidhi rasilimali zote wakitegemea iwaletee maendeleo lakini wanaonufaika na rasilimali hizi ni mafisadi wachache ndani ya chama na seerikali huku wananchi wakiishi maisha duni kupindukia.

CCM ni sawa kabisa na mtu mzima anayemtumia mtoto mdogo kama ngazi kwa manufaa yake binafsi. Mtu wa namna hiyo lazima anakuwa na hililafu kichwani mwake.

View attachment 175937

Vivo hivyo, CCM na mafisadi wake huwatumia walalahoi kama ngazi ya kupandia madarakani na wakishayapata hayo madaraka huuwaacha wananchi solemba. Sote ni mashahidi jinsi ambayo CCM inavyowakumbatia mafisadi na makuwadi wa mabeberu wanaokomba rasilimali za taifa na kuiacha nchi ikiwa kama jangwa.

CCM wameishiwa ubunifu wa kuitoa nchi hapa ilipo na kuipeleka mbele. Hata mcheza shoo anawazidi akili maCCM. Mcheza shoo hutumia mwili wake kama rasilimali ya kujiletea maendeleo kwa kuwaburudisha wateja wake na kuwakonga nyoyo zao.

View attachment 175936

Hata mbuzi anawazidi CCM akili. Wakati wa kiangazi, mbuzi hutumia maarifa yote kuyafikia majani popote yalipo lakini CCM wao wamelala usingizi huku wakitegemea kuombaomba misaada badala ya kutumia rasilimali tulizonazo kuwanufaisha watanzania wote.

View attachment 175935

Kama vile mcheza shoo anayotumia rasilimali aliyonayo (mauno) kujiletea maendeleo, tulitarajia kwamba CCM watumie rasilimali zilizopo nchini kuwaletea wananchi maendeleo endelevu. Nchi hii ina rasilimali lukuki ambazo kama zingetumika vizuri zingeleta manufaa kwa watanzania wote. Kinyume chake rasilimali zote wamekabidhiwa mabeberu (wanaopambwa kwa jina la ‘wawekezaji’) ambao wamemimika kutoka kila pembe ya dunia na kukimbilia kuvuma utajiri uliojaa tele nchini Tanzania.

View attachment 175934

Baada ya CCM kushindwa kuiendeleza nchi, wameamua kuwarubuni wananchi wenye njaa kwa lengo la kuwarejesha madarakani kila uchguzi mkuu uitishwapo. Mgao wa fedha wanazopata kutoka kwa mabepari waliowakabidhi rasilimali zetu, hutumikia kama chambo cha kuwarejesha madarakani kwa kuwapikia chakula, kuwapanga kama ng’ombe kwenye mistari na kuwalisha pilau.

View attachment 175933

Hii ndio kete ya mwisho iliyobaki. Mbinu nyingine zozote ziwazo zimeshindwa kufanya kazi. CCM wamewatia wananchi njaa kwa kutapanya rasilimali zao ili iwe rahisi kuwarubuni kwa kuwalisha chakula, kuwanunulia mbege, mataputapu, t-shirts, kanga, fulana, chumvi, sabuni, nk.

View attachment 175929 View attachment 175930View attachment 175952 View attachment 175978

Na kwa kuwa wananchi hawa wana njaa ya kutisha huamua kugawa kura zao kwa CCM, kisha hukaa na njaa na dhiki zao kwa miaka mingine mitano. Miaka mitano ikiisha CCM huwaendea tena na kuwalisha chakula na kuwapa vizawadi uchwara na hatimaye huwarejesha madarakani tena. Huu ni mzunguko hatari sana ambao kama usipodhibitiwa, wanachi wetu watazidi kutopea kwenye ufukara hadi Yesu atakaporudi. Wakati wa kutafuta kura kwa wananchi, wataingia hadi kwenye mahandaki lakini wakishapata hizo kura hawawakumbuki tena wananchi waliowapa kura.

View attachment 175928 View attachment 175979

Janja ya CCM ni sawa na mfugaji mpumbavu ambaye hamlishi ng’ombe wake lakini kila uchao utamkuta amening’inia kwenye chuchu akimkamua maziwa. Yuko radhi kukamua mpaka damu zitoke kuliko kumlisha na kumnenepesha ng’ombe wake ili apate maziwa mengi zaidi.

View attachment 175926 View attachment 175980

MaCCM hawaboreshi maisha ya wananchi lakini kila mwaka hupandisha kodi za bidhaa na huduma na kuyafanya maisha ya walalahoi yawe magumu zaidi. Kila bajeti isomwapo utasikia bia, soda, mkate, mafuta na bidhaa zingine zikipanda bei wakati uchumi wa watanzania bado upo pale pale!

View attachment 175924 View attachment 175925

Silaha ya mwisho kabisa waliyosalia nayo ni kuwabeba wananchi kwenye malori ya mchanga kuwapeleka kwenye mikutano yao ya siasa pamoja na kuwalipa posho uchwara ili kuwajazia mikutano yao ambayo siku za nyuma ilikuwa ikikosa wasikilizaji/wahudhuriaji. CCM wametufikisha hapa tulipo baada ya kuwafukarisha wananchi ili iwe rahisi kuwatawala.

View attachment 175923 View attachment 175958

Posho zenyewe wanzopewa ili kuhudhuria mikutano ya CCM huwa ni kidogo sana kiasi cha kupelekea wahudhuriaji kupigana ngumi na mateke wakigombea hayo makombo kidogo wanayoambulia kutoka kwa mafisadi. Hii ndio CCM zaidi ya mnavyoifahamu. CCM oyeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!

View attachment 175977 View attachment 175981

:israel:
Kaka nimekukubali, heshima kwako. Maccm Mungu ayalaaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Mungu ni mwema, ccm 2015 hawatoki hata kwa maroli wala kwa pilau wala kwa viposho vyao mshezi,utawaona mwakani wako radhi kujibweteka mavumbini kuonyesha unafiki wao.
 
ccm ndio mama yenu,ccm isipokuwepo maisha ya watanzania yatakuwa magumu sana,ccm imewapa elimu leo mnakuja kuitukana humu jf.ccm imekuwa tunu kwa watanzania
 
CCM imenifanyia mambo mengi mema katika maisha yangu mpaka hapa nilipofikia naishukuru sana ndio maana popote niendapo lazima nibebe city viwili bible na kadi yangu ya ccm

CCM 'imekufanyaje' mkuu? Imekufanya vizuri au vibaya?
 
ccm ndio mama yenu,ccm isipokuwepo maisha ya watanzania yatakuwa magumu sana,ccm imewapa elimu leo mnakuja kuitukana humu jf.ccm imekuwa tunu kwa watanzania

Mkuu, CCM imewapa elimu watanzania kwa kutumia KODI zao na RASIMALI ZA TAIFA (madini, misitu, maliasili, ardhi, samaki, nyuki, etc). Kwani CCM wanaokota hela au wanazipata kama KODI kutoka kwa wananchi?
 
Uwepo wa cCM madarakani mwaka 2015 ni ndoto.

Nimebahatika kuweza kuonana na wananchi wa kata ya KIBUTUKA katika wilaya ya LIWALE mkoani LINDI; Juu ya MABADILIKO wamenihakikishia kuwa CHADEMA itapata ushindi wa kishindo mwaka 2015.

Nilipowauliza kitu gani cha msingi kimewapelekea kuwa na matumaini hayo? Walijibu kama ifuatavyo; HUKU KUSINI CHAMA CHA CHADEMA HAKINA NGUVU KUBWA NA HATA UWEZEKANO WA KUCHUKUA UBUNGE NI VIGUMU LABDA KWA JIMBO LA MASASI. SASA, HATA KAMA CUF NDIO YENYE NGUVU SANA HUKU KUSINI LAKINI UWEZEKANO NA MATUMAINI YA KUSHINDA URAISI NI NDOTO. KWAHIYO WANANCHI TUNAJIPANGA KUHAKIKISHA KUWA TUTAFANYA UCHAGUZI KWA KUPIGIA KURA CUF KWA MBUNGE NA DIWANI, LAKINI KWAKUWA HATUNA MATUMAINI YA URAISI HATUWEZI KUPIGIA KURA CUF ILA TUTATIA NGUVUKWA CHADEMA ILI CCM KUIONDOA KABISA KATIKA ULIMWENGU WA SIASA. Nilifurahia sana msimamo wao huo. Mungi ibariki CHADEMA.
 
CCM hata wasimamishe mgombea mbuzi nitawapa kura yangu. Sijaona mbadala
 
CCM walianza na ngonjera ya ‘Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania’. Baada ya kuimba ngonjera hii kwa muda wa miaka 5 na kukosa muitikiaji, wakaamua kubalili mapigo na kuibuka na ngonjera mpya waliyoipa jina la ‘Ari mpya, Nguvu mpya na Kasi mpya’ (ANGUKA). Pamoja na usanii huu wote, maisha ya mtanzania yamezidi kuwa duni mwaka nenda mwaka rudi!

View attachment 175945 View attachment 175951 View attachment 175957

Tangu CCM washike madaraka nchi imekuwa haina mwelekeo. CCM inafanana na mtu mwenye jino moja. Mtu kama huyo hata umlishe namna gani hawezi kunenepa. Lazima atakufa kwa njaa kwa kuwa hana meno ya kutafunia chakula.

View attachment 175940

Nchi hii imejaliwa rasilimali nyingi za asili kama vile ardhi, maziwa , bahari na mito, madini, misitu, wanyama, nk. Lakini kwa kuwa CCM haina meno, imewaalika wenye meno (wawekezaji) waje watafune (wakavune) rasilimali hizo huku wakiiacha nchi ikiwa ikiwa tupu! Migogoro katika maeneo ya uchimbaji madini na maeneo yenye ardhi ya rutuba imekuwa ikitokea kila kukicha. Wananchi wamenyanganywa ardhi yao nzuri wamepewa ‘wawekezaji’. Watanzania wanyonge wamegeuka wakimbizi ndani ya nchi yao. Wananchi wamekata tamaa na utawala wa CCM. Hawana hamu nayo!

View attachment 175946 View attachment 175953

Huduma za jamii kama vile maji, umeme, barabara, elimu na afya imekuwa duni kiasi cha kukatisha tamaa. Wanafunzi kusomea chini ya miti ni suala la kawaida kabisa na wale wachache waliobahatika kupata kupata madarasa duni huketi chini ya sakafu ya vumbi au juu ya matofali! Hali hii mpaka lini hasa? CCM wala hawajali kwa kuwa watoto wao husomeshwa kwenye shule nzuri zenye walimu weledi na vifaa vya kufundishia vinavyotosheleza mahitaji.

View attachment 175947View attachment 175948 View attachment 175950 View attachment 175955 View attachment 175956

Mwalimu Nyerere alipokea uongozi wa nchi kutoka kwa wakoloni wakati nchi ikiwa taabani kiuchumi lakini hatukuwahi kushuhudia ugumu wa maisha kama tunavyoshuhudia hivi sasa. Ni lini hasa CCM na mafisadi wake wataboresha huduma za jamii na kuwafanya wananchi waishi maisha yenye utu?

CCM haina tofauti na mtu mzima aliyekabidhiwa kumlea mtoto mdogo badala yake akanywa maziwa ya mtoto na kumuacha mtoto akifa kwa njaa.

View attachment 175944

Hii maana yake ni kwamba CCM imeamimiwa na wananchi wakaikabidhi rasilimali zote wakitegemea iwaletee maendeleo lakini wanaonufaika na rasilimali hizi ni mafisadi wachache ndani ya chama na seerikali huku wananchi wakiishi maisha duni kupindukia.

CCM ni sawa kabisa na mtu mzima anayemtumia mtoto mdogo kama ngazi kwa manufaa yake binafsi. Mtu wa namna hiyo lazima anakuwa na hililafu kichwani mwake.

View attachment 175937

Vivo hivyo, CCM na mafisadi wake huwatumia walalahoi kama ngazi ya kupandia madarakani na wakishayapata hayo madaraka huuwaacha wananchi solemba. Sote ni mashahidi jinsi ambayo CCM inavyowakumbatia mafisadi na makuwadi wa mabeberu wanaokomba rasilimali za taifa na kuiacha nchi ikiwa kama jangwa.

CCM wameishiwa ubunifu wa kuitoa nchi hapa ilipo na kuipeleka mbele. Hata mcheza shoo anawazidi akili maCCM. Mcheza shoo hutumia mwili wake kama rasilimali ya kujiletea maendeleo kwa kuwaburudisha wateja wake na kuwakonga nyoyo zao.

View attachment 175936

Hata mbuzi anawazidi CCM akili. Wakati wa kiangazi, mbuzi hutumia maarifa yote kuyafikia majani popote yalipo lakini CCM wao wamelala usingizi huku wakitegemea kuombaomba misaada badala ya kutumia rasilimali tulizonazo kuwanufaisha watanzania wote.

View attachment 175935

Kama vile mcheza shoo anayotumia rasilimali aliyonayo (mauno) kujiletea maendeleo, tulitarajia kwamba CCM watumie rasilimali zilizopo nchini kuwaletea wananchi maendeleo endelevu. Nchi hii ina rasilimali lukuki ambazo kama zingetumika vizuri zingeleta manufaa kwa watanzania wote. Kinyume chake rasilimali zote wamekabidhiwa mabeberu (wanaopambwa kwa jina la ‘wawekezaji’) ambao wamemimika kutoka kila pembe ya dunia na kukimbilia kuvuma utajiri uliojaa tele nchini Tanzania.

View attachment 175934

Baada ya CCM kushindwa kuiendeleza nchi, wameamua kuwarubuni wananchi wenye njaa kwa lengo la kuwarejesha madarakani kila uchguzi mkuu uitishwapo. Mgao wa fedha wanazopata kutoka kwa mabepari waliowakabidhi rasilimali zetu, hutumikia kama chambo cha kuwarejesha madarakani kwa kuwapikia chakula, kuwapanga kama ng’ombe kwenye mistari na kuwalisha pilau.

View attachment 175933

Hii ndio kete ya mwisho iliyobaki. Mbinu nyingine zozote ziwazo zimeshindwa kufanya kazi. CCM wamewatia wananchi njaa kwa kutapanya rasilimali zao ili iwe rahisi kuwarubuni kwa kuwalisha chakula, kuwanunulia mbege, mataputapu, t-shirts, kanga, fulana, chumvi, sabuni, nk.

View attachment 175929 View attachment 175930View attachment 175952 View attachment 175978

Na kwa kuwa wananchi hawa wana njaa ya kutisha huamua kugawa kura zao kwa CCM, kisha hukaa na njaa na dhiki zao kwa miaka mingine mitano. Miaka mitano ikiisha CCM huwaendea tena na kuwalisha chakula na kuwapa vizawadi uchwara na hatimaye huwarejesha madarakani tena. Huu ni mzunguko hatari sana ambao kama usipodhibitiwa, wanachi wetu watazidi kutopea kwenye ufukara hadi Yesu atakaporudi. Wakati wa kutafuta kura kwa wananchi, wataingia hadi kwenye mahandaki lakini wakishapata hizo kura hawawakumbuki tena wananchi waliowapa kura.

View attachment 175928 View attachment 175979

Janja ya CCM ni sawa na mfugaji mpumbavu ambaye hamlishi ng’ombe wake lakini kila uchao utamkuta amening’inia kwenye chuchu akimkamua maziwa. Yuko radhi kukamua mpaka damu zitoke kuliko kumlisha na kumnenepesha ng’ombe wake ili apate maziwa mengi zaidi.

View attachment 175926 View attachment 175980

MaCCM hawaboreshi maisha ya wananchi lakini kila mwaka hupandisha kodi za bidhaa na huduma na kuyafanya maisha ya walalahoi yawe magumu zaidi. Kila bajeti isomwapo utasikia bia, soda, mkate, mafuta na bidhaa zingine zikipanda bei wakati uchumi wa watanzania bado upo pale pale!

View attachment 175924 View attachment 175925

Silaha ya mwisho kabisa waliyosalia nayo ni kuwabeba wananchi kwenye malori ya mchanga kuwapeleka kwenye mikutano yao ya siasa pamoja na kuwalipa posho uchwara ili kuwajazia mikutano yao ambayo siku za nyuma ilikuwa ikikosa wasikilizaji/wahudhuriaji. CCM wametufikisha hapa tulipo baada ya kuwafukarisha wananchi ili iwe rahisi kuwatawala.

View attachment 175923 View attachment 175958

Posho zenyewe wanzopewa ili kuhudhuria mikutano ya CCM huwa ni kidogo sana kiasi cha kupelekea wahudhuriaji kupigana ngumi na mateke wakigombea hayo makombo kidogo wanayoambulia kutoka kwa mafisadi. Hii ndio CCM zaidi ya mnavyoifahamu. CCM oyeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!

View attachment 175977 View attachment 175981

:israel:

Thread of the Year aiseee, nimeikosa quote nzima purposesly
 
Hivi mtu anapisimama na kuwaambia watu kuwa CCM imejenga barabara au kujenga shule za kata na mengineyo, ni chama ndio kimejenga kwa pesa zake au wananchi ndio wamelipa kodi zikajengwa? Kweli hizi CCM wanafaidika nazo sana hasa kwa wananchi wasio na uelewa mpana juu ya haki na wajibu wao
 
CCM itaendelea kuwa CCM .CHADEMA itaendelea kuwa CHADEMA.
SIMBA ataendelea kuwa SIMBA.NYANI ataendelea kuwa NYANI.
TEMBO hatakama akikonda vipi hawezi kuwa kama MBUZI.
Na MBUZI hata kama akinenepa vipi hawezi kuwa kama TEMBO.
 
Leo nilianza kuwa bored eti CCM wanataka Kinana aendelee kuwashawishi UKAWA warejee Bungeni na kuwa eti kuna mambo kama serikali za mitaa hazikuwekwa kwenye Rasimu, na kipengele cha Mahakama ya Kadhi iwekwe kwenye Katiba sasa! Nilikuwa najiuliza mbona mahakama ya kadhi waliwahi kuweka kwenye Ilani yao ya Uchaguzi na mpaka leo hakuna walichowafanyia cha maana Waislam wa nchi hii zaidi ya kuwabambika mikesi ya ajabu ajabu wanaharakati wote wa Kiislam?... Uzi huu umeniweka sawa sasa kuwa CCM wako tayari kufanya lolote ilimradi waendelee kuwaibia Watanzania ...
 
ccm ndio mama yenu,ccm isipokuwepo maisha ya watanzania yatakuwa magumu sana,ccm imewapa elimu leo mnakuja kuitukana humu jf.ccm imekuwa tunu kwa watanzania

MSWALIE MTUME wee jamaa , tunu ya ccm iko wapi hapa ? Kuna mzee amenitoa machozi aisee , kavaa mashati mawili lakini mbavu zote zinaonekana ! HAYA NDIO MAISHA BORA MLIYOTUAHIDI ?
 
uwepo wa ccm madarakani mwaka 2015 ni ndoto.

Nimebahatika kuweza kuonana na wananchi wa kata ya kibutuka katika wilaya ya liwale mkoani lindi; juu ya mabadiliko wamenihakikishia kuwa chadema itapata ushindi wa kishindo mwaka 2015.

Nilipowauliza kitu gani cha msingi kimewapelekea kuwa na matumaini hayo? Walijibu kama ifuatavyo; huku kusini chama cha chadema hakina nguvu kubwa na hata uwezekano wa kuchukua ubunge ni vigumu labda kwa jimbo la masasi. Sasa, hata kama cuf ndio yenye nguvu sana huku kusini lakini uwezekano na matumaini ya kushinda uraisi ni ndoto. Kwahiyo wananchi tunajipanga kuhakikisha kuwa tutafanya uchaguzi kwa kupigia kura cuf kwa mbunge na diwani, lakini kwakuwa hatuna matumaini ya uraisi hatuwezi kupigia kura cuf ila tutatia nguvukwa chadema ili ccm kuiondoa kabisa katika ulimwengu wa siasa. Nilifurahia sana msimamo wao huo. Mungi ibariki chadema.

ukawa oyeeee !
 
Back
Top Bottom