Hivi mtu anapisimama na kuwaambia watu kuwa CCM imejenga barabara au kujenga shule za kata na mengineyo, ni chama ndio kimejenga kwa pesa zake au wananchi ndio wamelipa kodi zikajengwa? Kweli hizi CCM wanafaidika nazo sana hasa kwa wananchi wasio na uelewa mpana juu ya haki na wajibu wao
Hizo barabara na shule zimejengwa kwa sera ya CDM? mbona mna roho ngumu sana kukubali yapo mazuri CCM imefanya?
Kweli yapo mazuri kama mikataba mibovu', kin mama kujifungulia chini, watoto kukalia mawe, watu kingolewa kucha, serikali isiyo penda uwazi. Etc etc
Hizo barabara na shule zimejengwa kwa sera ya CDM? mbona mna roho ngumu sana kukubali yapo mazuri CCM imefanya?
Hizo barabara na shule zimejengwa kwa sera ya CDM? mbona mna roho ngumu sana kukubali yapo mazuri CCM imefanya?
Nyie wakataa pema mnaona aibu kukiri kwamba kwa sera bora za Chama Cha Mapinduzi mnajua kusoma na kuandika hata kama ulisomea chini ya miti. Mjifunze kusema Ahsante hata kwa kile mnachokiona kidogo na si lolote.
asante , lakini ccm kwaheri .
Wewe unaamka unarara? Labda Kama mtaondoa ile rangi ya kijani ktk bendera ya taifa.
mkuu bendera ni matambara tu , kama ikiwapendeza wananchi , hatutafuta rangi ya kijani tu bali tutaitupa bendera yote !
niwie radhi mkuu Erythrocyte nipe sababu 3 tu za wewe kukichukia Chama Cha Mapinduzi kinachoaminiwa na kupendwa na takriban 95% ya watanzania wote.
Nashindwa kabisa kuelewa zinakopatikania baadhi ya data, kama hii 95% iliyotajwa hapa.
Wapiga kura ktk uchaguzi mkuu uliopita walikuwa chini ya 40% ya Watz wote. Sijui hii tafiti ilifanyikafanyika vipi na wapi. Taarifa na data kama hizi ndio hutufanya tuonekane wapiga debe. Haya mkuu, tusonge mbele!