Rais hakutangaza kufuta ada ila alisema wanaangalia uwezekano wa kutoa elimu bure. Bado hiyo haijawa sera rasmi.
Wewe na wenzio wa aina yako hamjui historia ya Tz, aidha kwa bahati mbaya au kwa malengo. Wengi wa wazee watawala unaowapigia debe wanatokana na wazazi wakulima masikini. Isingekuwa sera ya TANU kutoa elimu bure wasingekuwa ktk ngazi yoyote ya uongozi, labda ubalozi wa nyumba kumi.
Wamejisahau, wanajilipa mishahara minono na marupurupu manene kama hizo laki tatu kwa siku vikao vya Bunge la Katiba, wanasomesha watoto wao vyuo ghali na ng'ambo; na BAADHI ya watoto wa masikini wanakopeshwa na wengi hawana kabisa uwezo wa kusomesha watoto wao hata kwenye hizi shule za kata!
Hali hii inapelekea kuwepo kwa tabaka maalum la watawala na pia tabaka lingine MAALUM la watawaliwa. Tunaposema kweli tunaitwa 'wapinzani'. Tunachotaka ni chama kurudi kwenye misingi ya asili ya kujali watu wanyonge. Kama wao waliwezeshwa kufika walipo kutokana na sera nzuri iweje leo wanadidimiza umma kwa kutumia madaraka waliyoyapata kwa hisani ya umma huo huo?
Si vyema kumuona kila msemakweli kuwa ni mpinzani wa CCM. Kama mtu si mwana CCM hana haki ya kuikosoa? Kwani si ndio wanaotunga sera na kutawala kwa sasa?