Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
niwie radhi mkuu Erythrocyte nipe sababu 3 tu za wewe kukichukia Chama Cha Mapinduzi kinachoaminiwa na kupendwa na takriban 95% ya watanzania wote.
nimefanya random sampling
uongo wa takwimu zako ushahidi wake anao marehemu lewis makame , alishuhudia 2010 , tukija kwenye hili la sababu 3 za mimi kuichukia ccm , ukisoma vizuri uzi huu utagundua kwamba hakuna SABABU 3 TU PEKE YAKE , BALI KUNA MAMIA YA SABABU ZA KUYAPINGA MAGAMBA !
huu uzi umekaa kishabiki tu kweli yapo mambo machache CCM ilikosea . Lakini mazuri ya kujivunia yapo tena mengi sana legeza moyo wako
nimefanya random sampling
usithubutu kumuamini kijana yeyote wa lumumba , ni wasakatonge .Mkuu hii random sampling sio sahihi. Umetumia makundi gani ktk jamii kufanyia utafiti huu?
Tafakari data nyepesi kwa akili ya kawaida; kundi la vijana na watoto chini ya miaka 18 linaunda asilimia ngapi ya Watz wote, ukitilia maanani kwamba kundi hili halina chama? Una maana kundi hili ndio hiyo 5% uliyobakiza? Kama tutachukulia kuwa hiyo ndio hali halisi, je, wanachama wa upinzani wanaunda asilimia ngapi?
Muhimu naona ktk nyuzi nyingi hapa JF mambo ya siasa hukaa kishabiki na kiupofu zaidi kuliko hali halisi. Tunatarajia wadau maarufu na wakubwa kutengeneza na kuonyesha njia badala ya kuyumbisha na kupotosha ukweli kama hivi. Ukweli na uadilifu ndio utakaotujengea Tz bora, leo na kesho!
Eee bhana inasemekana nusu ya hawa wanaliojichora 2010 wanaokota machupa majalalani! Usicheze na Mungu mkuu .
ccm ndio mama yenu,amewazaa na kuwatunza toka nyerere mpaka sasa
Mkuu hii random sampling sio sahihi. Umetumia makundi gani ktk jamii kufanyia utafiti huu?
Tafakari data nyepesi kwa akili ya kawaida; kundi la vijana na watoto chini ya miaka 18 linaunda asilimia ngapi ya Watz wote, ukitilia maanani kwamba kundi hili halina chama? Una maana kundi hili ndio hiyo 5% uliyobakiza? Kama tutachukulia kuwa hiyo ndio hali halisi, je, wanachama wa upinzani wanaunda asilimia ngapi?
Muhimu naona ktk nyuzi nyingi hapa JF mambo ya siasa hukaa kishabiki na kiupofu zaidi kuliko hali halisi. Tunatarajia wadau maarufu na wakubwa kutengeneza na kuonyesha njia badala ya kuyumbisha na kupotosha ukweli kama hivi. Ukweli na uadilifu ndio utakaotujengea Tz bora, leo na kesho!
kipimo cha akili timamu si kuvaa nguo, kati 100% ya watanzania niliofanya nao mahojiano 95% wanatambua na kukubali mchango wa CCM ktk maendeleo ya taifa hili. Hawana imani na viongozi wa vyama vya upinzani na majibu utayapata 2015 :hail:
Maneno yako yamekaa kichwa chini miguu juu! Unajua tofauti ya siasa za TANU na siasa za CCM? Jambo usilolijua litakusumbua.
Kusoma University bure na kusoma kwa mkopo kunafanana? Na je, kutibiwa hospitali moja na waziri kunafanana na wewe kutibiwa hospitali ya Temeke na waziri kutibiwa South Africa? Naona kama uko usingizini vile!
wewe pia ni mnufaikaji wa mfumo mzuri wa ccm na sera za ccm imewezesha watanzania vijana kupewa elimu ya chuoni kusoma bure. juzi kikwete ametangaza kufuta ada za sekondari nchini watoto wenu wasome bure.ccm inawajali sana kama mama mzazi

leo umekubali kama hizo picha ni za nchi hii au bado unaamini kwamba ni za somalia ?
Rais hakutangaza kufuta ada ila alisema wanaangalia uwezekano wa kutoa elimu bure. Bado hiyo haijawa sera rasmi.
Wewe na wenzio wa aina yako hamjui historia ya Tz, aidha kwa bahati mbaya au kwa malengo. Wengi wa wazee watawala unaowapigia debe wanatokana na wazazi wakulima masikini. Isingekuwa sera ya TANU kutoa elimu bure wasingekuwa ktk ngazi yoyote ya uongozi, labda ubalozi wa nyumba kumi.
Wamejisahau, wanajilipa mishahara minono na marupurupu manene kama hizo laki tatu kwa siku vikao vya Bunge la Katiba, wanasomesha watoto wao vyuo ghali na ng'ambo; na BAADHI ya watoto wa masikini wanakopeshwa na wengi hawana kabisa uwezo wa kusomesha watoto wao hata kwenye hizi shule za kata!
Hali hii inapelekea kuwepo kwa tabaka maalum la watawala na pia tabaka lingine MAALUM la watawaliwa. Tunaposema kweli tunaitwa 'wapinzani'. Tunachotaka ni chama kurudi kwenye misingi ya asili ya kujali watu wanyonge. Kama wao waliwezeshwa kufika walipo kutokana na sera nzuri iweje leo wanadidimiza umma kwa kutumia madaraka waliyoyapata kwa hisani ya umma huo huo?
Si vyema kumuona kila msemakweli kuwa ni mpinzani wa CCM. Kama mtu si mwana CCM hana haki ya kuikosoa? Kwani si ndio wanaotunga sera na kutawala kwa sasa?
Mkuu, baadhi ya muda unashindwa kuelewa kama hawa watu ni Watz kwa kuzaliwa au wamenunua uraia!