CCM nambari wani

CCM nambari wani

CCM walianza na ngonjera ya ‘Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania’. Baada ya kuimba ngonjera hii kwa muda wa miaka 5 na kukosa muitikiaji, wakaamua kubalili mapigo na kuibuka na ngonjera mpya waliyoipa jina la ‘Ari mpya, Nguvu mpya na Kasi mpya’ (ANGUKA). Pamoja na usanii huu wote, maisha ya mtanzania yamezidi kuwa duni mwaka nenda mwaka rudi!

View attachment 175945 View attachment 175951 View attachment 175957

Tangu CCM washike madaraka nchi imekuwa haina mwelekeo. CCM inafanana na mtu mwenye jino moja. Mtu kama huyo hata umlishe namna gani hawezi kunenepa. Lazima atakufa kwa njaa kwa kuwa hana meno ya kutafunia chakula.

View attachment 175940

Nchi hii imejaliwa rasilimali nyingi za asili kama vile ardhi, maziwa , bahari na mito, madini, misitu, wanyama, nk. Lakini kwa kuwa CCM haina meno, imewaalika wenye meno (wawekezaji) waje watafune (wakavune) rasilimali hizo huku wakiiacha nchi ikiwa ikiwa tupu! Migogoro katika maeneo ya uchimbaji madini na maeneo yenye ardhi ya rutuba imekuwa ikitokea kila kukicha. Wananchi wamenyanganywa ardhi yao nzuri wamepewa ‘wawekezaji’. Watanzania wanyonge wamegeuka wakimbizi ndani ya nchi yao. Wananchi wamekata tamaa na utawala wa CCM. Hawana hamu nayo!

View attachment 175946 View attachment 175953

Huduma za jamii kama vile maji, umeme, barabara, elimu na afya imekuwa duni kiasi cha kukatisha tamaa. Wanafunzi kusomea chini ya miti ni suala la kawaida kabisa na wale wachache waliobahatika kupata kupata madarasa duni huketi chini ya sakafu ya vumbi au juu ya matofali! Hali hii mpaka lini hasa? CCM wala hawajali kwa kuwa watoto wao husomeshwa kwenye shule nzuri zenye walimu weledi na vifaa vya kufundishia vinavyotosheleza mahitaji.

View attachment 175947View attachment 175948 View attachment 175950 View attachment 175955 View attachment 175956

Mwalimu Nyerere alipokea uongozi wa nchi kutoka kwa wakoloni wakati nchi ikiwa taabani kiuchumi lakini hatukuwahi kushuhudia ugumu wa maisha kama tunavyoshuhudia hivi sasa. Ni lini hasa CCM na mafisadi wake wataboresha huduma za jamii na kuwafanya wananchi waishi maisha yenye utu?

CCM haina tofauti na mtu mzima aliyekabidhiwa kumlea mtoto mdogo badala yake akanywa maziwa ya mtoto na kumuacha mtoto akifa kwa njaa.

View attachment 175944

Hii maana yake ni kwamba CCM imeamimiwa na wananchi wakaikabidhi rasilimali zote wakitegemea iwaletee maendeleo lakini wanaonufaika na rasilimali hizi ni mafisadi wachache ndani ya chama na seerikali huku wananchi wakiishi maisha duni kupindukia.

CCM ni sawa kabisa na mtu mzima anayemtumia mtoto mdogo kama ngazi kwa manufaa yake binafsi. Mtu wa namna hiyo lazima anakuwa na hililafu kichwani mwake.

View attachment 175937

Vivo hivyo, CCM na mafisadi wake huwatumia walalahoi kama ngazi ya kupandia madarakani na wakishayapata hayo madaraka huuwaacha wananchi solemba. Sote ni mashahidi jinsi ambayo CCM inavyowakumbatia mafisadi na makuwadi wa mabeberu wanaokomba rasilimali za taifa na kuiacha nchi ikiwa kama jangwa.

CCM wameishiwa ubunifu wa kuitoa nchi hapa ilipo na kuipeleka mbele. Hata mcheza shoo anawazidi akili maCCM. Mcheza shoo hutumia mwili wake kama rasilimali ya kujiletea maendeleo kwa kuwaburudisha wateja wake na kuwakonga nyoyo zao.Kama vile mcheza shoo anayotumia rasilimali aliyonayo (mauno) kujiletea maendeleo, tulitarajia kwamba CCM watumie rasilimali zilizopo nchini kuwaletea wananchi maendeleo endelevu lakini wao bado wamelala usingizi wa pono.

View attachment 175936

Hata mbuzi anawazidi CCM akili. Wakati wa kiangazi, mbuzi hutumia maarifa yote kuyafikia majani popote yalipo lakini CCM wao wamelala usingizi huku wakitegemea kuombaomba misaada badala ya kutumia rasilimali tulizonazo kuwanufaisha watanzania wote.

View attachment 175935

Nchi hii ina rasilimali lukuki ambazo kama zingetumika vizuri zingeleta manufaa kwa watanzania wote. Kinyume chake rasilimali zote wamekabidhiwa mabeberu (wanaopambwa kwa jina la ‘wawekezaji’) ambao wamemimika kutoka kila pembe ya dunia na kukimbilia kuvuma utajiri uliojaa tele nchini Tanzania.

View attachment 175934

Baada ya CCM kushindwa kuiendeleza nchi, wameamua kuwarubuni wananchi wenye njaa kwa lengo la kuwarejesha madarakani kila uchguzi mkuu uitishwapo. Mgao wa fedha wanazopata kutoka kwa mabepari waliowakabidhi rasilimali zetu, hutumikia kama chambo cha kuwarejesha madarakani kwa kuwapikia chakula, kuwapanga kama ng’ombe kwenye mistari na kuwalisha pilau.

View attachment 175933

Hii ndio kete ya mwisho iliyobaki. Mbinu nyingine zozote ziwazo zimeshindwa kufanya kazi. CCM wamewatia wananchi njaa kwa kutapanya rasilimali zao ili iwe rahisi kuwarubuni kwa kuwalisha chakula, kuwanunulia mbege, mataputapu, t-shirts, kanga, fulana, chumvi, sabuni, nk.

View attachment 175929 View attachment 175930View attachment 175952 View attachment 175978

Na kwa kuwa wananchi hawa wana njaa ya kutisha huamua kugawa kura zao kwa CCM, kisha hukaa na njaa na dhiki zao kwa miaka mingine mitano. Miaka mitano ikiisha CCM huwaendea tena na kuwalisha chakula na kuwapa vizawadi uchwara na hatimaye huwarejesha madarakani tena. Huu ni mzunguko hatari sana ambao kama usipodhibitiwa, wanachi wetu watazidi kutopea kwenye ufukara hadi Yesu atakaporudi. Wakati wa kutafuta kura kwa wananchi, wataingia hadi kwenye mahandaki lakini wakishapata hizo kura hawawakumbuki tena wananchi waliowapa kura.

View attachment 175928 View attachment 175979

Janja ya CCM ni sawa na mfugaji mpumbavu ambaye hamlishi ng’ombe wake lakini kila uchao utamkuta amening’inia kwenye chuchu akimkamua maziwa. Yuko radhi kukamua mpaka damu zitoke kuliko kumlisha na kumnenepesha ng’ombe wake ili apate maziwa mengi zaidi.

View attachment 175926 View attachment 175980

MaCCM hawaboreshi maisha ya wananchi lakini kila mwaka hupandisha kodi za bidhaa na huduma na kuyafanya maisha ya walalahoi yawe magumu zaidi. Kila bajeti isomwapo utasikia bia, soda, mkate, mafuta na bidhaa zingine zikipanda bei wakati uchumi wa watanzania bado upo pale pale!

View attachment 175924 View attachment 175925

Silaha ya mwisho kabisa waliyosalia nayo ni kuwabeba wananchi kwenye malori ya mchanga kuwapeleka kwenye mikutano yao ya siasa pamoja na kuwalipa posho uchwara ili kuwajazia mikutano yao ambayo siku za nyuma ilikuwa ikikosa wasikilizaji/wahudhuriaji. CCM wametufikisha hapa tulipo baada ya kuwafukarisha wananchi ili iwe rahisi kuwatawala.

View attachment 175958

Posho zenyewe wanzopewa ili kuhudhuria mikutano ya CCM huwa ni kidogo sana kiasi cha kupelekea wahudhuriaji kupigana ngumi na mateke wakigombea hayo makombo kidogo wanayoambulia kutoka kwa mafisadi. Hii ndio CCM zaidi ya mnavyoifahamu. CCM oyeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!

View attachment 175977 View attachment 175981

:israel:

Chama cha malori hahaha magamba
 
tpaul naomba uweke na yale mazuri ili tufanye uwiano.
 
Last edited by a moderator:
Kama Musa alivyowaongoza wana wa Israel kutoka Misri kwenda Nchi ya ahadi na ndivyo Chama Cha Mapinduzi siku moja kitatufikisha kule kwenye mito ya asili na maziwa. Hakuna mbadala wa CCM kwa wakati huu kumbukeni "usiache mbachao kwa msala upitao"
 
kp02092014.jpg

asante mkuu .
 
tpaul naomba uweke na yale mazuri ili tufanye uwiano.

Mazuri gani? Kama kuna mazuri uliyokaririshwa huko Lumumba hebu yaweke hapa tuyapime.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Mazuri gani? Kama kuna mazuri uliyokaririshwa huko Lumumba hebu yaweke hapa tuyapime.

ok naomba wewe mwenyewe uwe mfano rahisi kabisa, bila sera bora za chama cha mapinduzi ungejua kusoma na kuandika wewe?
Uhuru na demokrasia iliyopitiliza ulioletwa na chama cha mapinduzi watu kama wewe mnautumia vibaya mfano yule babu kichaa anatukana waasisi wa taifa hili, haya ni kati ya machache sana ya msingi. Tazama watu wanavyoumia kule Congo, Sudan, Somalia na sehemu nyingine wanaitaman amani kama hii tuliyonayo.
Nyinyi mnatuona sisi karunguyeye hatuyaoni hayo? Mnabwatuka lugha chafu na maneno ya uchochezi kila siku
we are watching you !!!!
 
ok naomba wewe mwenyewe uwe mfano rahisi kabisa, bila sera bora za chama cha mapinduzi ungejua kusoma na kuandika wewe?
Uhuru na demokrasia iliyopitiliza ulioletwa na chama cha mapinduzi watu kama wewe mnautumia vibaya mfano yule babu kichaa anatukana waasisi wa taifa hili, haya ni kati ya machache sana ya msingi. Tazama watu wanavyoumia kule Congo, Sudan, Somalia na sehemu nyingine wanaitaman amani kama hii tuliyonayo.
Nyinyi mnatuona sisi karunguyeye hatuyaoni hayo? Mnabwatuka lugha chafu na maneno ya uchochezi kila siku
we are watching you !!!!

MKUU WANGU SANA , HEBU TWENDE TARATIBU , hIVI HIZI HELA MNAZOIBA ( AMA KUPORA ) KWA MKUPUO NA MFULULIZO NAMNA HII , HUKU HUDUMA ZA WANANCHI ZIKIDOROLA KIASI CHA KUWAFANYA WAJUTE KUZALIWA , KAMA HIZO PICHA KIDOGO SANA ZINAVYOONYESHA HAPA ( NASEMA KIDOGO , MAANA TUNAANDA KONTENA LA PICHA MBALIMBALI ZIKIONYESHA DHIKI YA KUFA MTU ) , TUKIFICHUA UNAKUWA UCHOCHEZI NA MATUSI ?
 
MKUU WANGU SANA , HEBU TWENDE TARATIBU , hIVI HIZI HELA MNAZOIBA ( AMA KUPORA ) KWA MKUPUO NA MFULULIZO NAMNA HII , HUKU HUDUMA ZA WANANCHI ZIKIDOROLA KIASI CHA KUWAFANYA WAJUTE KUZALIWA , KAMA HIZO PICHA KIDOGO SANA ZINAVYOONYESHA HAPA ( NASEMA KIDOGO , MAANA TUNAANDA KONTENA LA PICHA MBALIMBALI ZIKIONYESHA DHIKI YA KUFA MTU ) , TUKIFICHUA UNAKUWA UCHOCHEZI NA MATUSI ?

Mwageni picha kamanda! !!!!!
 
MKUU WANGU SANA , HEBU TWENDE TARATIBU , hIVI HIZI HELA MNAZOIBA ( AMA KUPORA ) KWA MKUPUO NA MFULULIZO NAMNA HII , HUKU HUDUMA ZA WANANCHI ZIKIDOROLA KIASI CHA KUWAFANYA WAJUTE KUZALIWA , KAMA HIZO PICHA KIDOGO SANA ZINAVYOONYESHA HAPA ( NASEMA KIDOGO , MAANA TUNAANDA KONTENA LA PICHA MBALIMBALI ZIKIONYESHA DHIKI YA KUFA MTU ) , TUKIFICHUA UNAKUWA UCHOCHEZI NA MATUSI ?

Sikatai kuhusu mabaya je hakuna mazuri? Macho yako hayaoni mema yaliyofanyika?
 
Wacha kuongea kirahisi rahisi huu ni mustakabali wa watanzania zaidi ya milion40 .wewe ndio utajuta kuzaliwa kwa kufuata siasa za mkumbo.
 
mbona tayari nimejuta , usipotoa machozi kwa picha hizi , hakika wewe utakuwa si binadamu .

bado una ndoto ya kuwa mbunge Wa chadema kwa kumtukana mzazi wako ccm, laana ya kusaliti ccm haitakuacha kamwe unashabikia Uzi Wa kijinga kama huu
 
Back
Top Bottom